Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Unazijua nchi zisizokuwa na jeshi la kudumu duniani?
Ili nchi iwe na vikosi vya kijeshi, vikosi hivi vinahitaji kuwa na sawa, ikiwa na vifaa vya kutosha, kutengewa bajeti kila wakati, na kuimarishwa na kusimamiwa kwa vikosi vya jeshi chini ya serikali.
Walakini, kuna nchi nyingi huru ambazo bado zinakataa kuunda vikosi vya kijeshi.
Jeshi linaundwa kwa lengo la kujihusisha na vita na kulinda nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje, lakini wakati mwingine linashiriki katika shughuli za kutoa msaada kama vile kusambaza chakula, maji na matibabu wakati nchi inapohitaji.
Muktadha wa jeshi linalozungumziwa hapa ni kama jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) au ni kama majeshi yanayopigana sasa baina na Urusi na Ukraine.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Shirika la kimataifa la kijajusi la Marekani, CIA, kuna makumi ya nchi ulimwenguni ambazo hazina uwepo wa kijeshi.
Uswisi na Austria, kwa mfano, zilikubali kuilinda Liechtenstein, huku Ufaransa na Hispania ziliilinda Andorra.
CIA iliongeza kuwa ingawa nchi hizi "hazina jeshi la kudumu", nchi kadhaa zina jeshi la polisi, ambalo linaweza kufanya kazi kama jeshi la kulinda nchi na mipaka yake.
Katika oroda hiyo nchi mashuhuri zisizo za kijeshi ulimwenguni ni pamoja na:
1. Mauritius
Mauritius ilivunja jeshi lake mwaka 1968, lakini ina Kikosi Maalumu kidogo, kilichofunzwa vyema. Wanashirikiana katika usalama na India.
Mauritius ni mojawapo ya nchi chache duniani ambazo hazina jeshi la kudumu la kulinda nchi. Hata hivyo, nchi hiyo ina maafisa wa polisi wapatao 10,000, ambao wana jukumu la kutekeleza kila kitu ambacho wanajeshi, polisi na vikosi vya usalama vingefanya.
Mauritius, nchi isiyo na bahari barani Afrika, ni kivutio maarufu cha watalii.
2: Andora
Andorra ni nchi ndogo ya milima iliyopo katikati ya Ufaransa na Hispania. Nchi hiyo haina jeshi la kudumu, hata hivyo, na ina makubaliano ya ulinzi na nchi za Hispania na Ufaransa.
Na bado ina askari wa kujitolea wasio na silaha, ambao huonekana kwenye sherehe maalum. Sheria za nchi zinatekelezwa na polisi wa kitaifa, ambao wanahusika na usalama wa nchi.
3: Costa Rica
Costa Rica ilivunja vikosi vyake vya kijeshi mnamo 1948, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kila mwaka tarehe mosi Desemba, nchi hiyo huadhimisha siku ya kuvunjwa jeshi.
Hata hivyo, nchi hiyo ina kikosi cha polisi kilichopewa mafunzo maalum na Marekani na Colombia, ambacho kinahusika na usalama wa ndani.
Nchi hiyo ya Amerika ya Kati iko karibu na ikweta na ina pwani zinazounganisha Bahari ya Carrebean na Bahari ya Pasifiki.
4: Liechtenstein
Nchi hiyo ilivunja jeshi lake mnamo 1868, ikiona kuwa na jeshi ni gharama kubwa.
Liechtenstein ina kikosi cha polisi kilicho na silaha ndogo ndogo, ambacho kinafanya shughuli za usalama wa ndani.
Inapokea usaidizi wa ulinzi kutoka Uswizi na Austria ikiwa wanahitaji usaidizi, kulingana na makubaliano yasiyo rasmi yaliyoafikiwa na nchi hizo tatu.
5: Panama
Jeshi la Panama lilivunjwa mwaka 1990 na sasa lina kikosi kidogo kilichofunzwa kijeshi, na nchi hii ina kile kinachoitwa Jeshi la Wananchi wa Panama, ambalo linahusika na usalama wa ndani na matatizo ya mpaka.
6: Iceland
Iceland ilikuwa na jeshi mnamo 1869, lakini tangu wakati huo nchi hiyo imeingia makubaliano na Marekani, ambayo kutoka 1951 hadi 2006 imekuwa ikisaidia Vikosi vya Ulinzi vya Iceland.
Mwaka 2006, Marekani ilitangaza kutoa msaada wa kiusalama kwa Iceland, kwa kuwa haikuwa na jeshi nchini humo.
Usalama wa nchi hii ni wajibu wa Muungano wa NATO (hasa Marekani, Norway, na Denmark).
Maeneo mengine yasiyokuwa na jeshi la kudumu duniani ni
Aruba Cayman Islands Cook Islands Curacao Falkland Islands Faroe Islands French Polynesia Greenland Grenada Kiribati Macau (China S.A.R)
Marshall Islands Federated States of Micronesia Monaco Montserrat New Caledonia Nauru Niue Palau St. Lucia St. Vincent and the Grenadines Samoa San Marino Sint Maarten Solomon Islands Svalbard Tuvalu and Vanuatu