Kombe la dunia 2022: Yanayoendelea Qatar yanafurahisha

Iliyochapishwa

Michuano ya kombe la dunia inaendelea huko Qatar. Akitafuta bingwa wa dunia katika toleo la 22 la mashindano haya makubwa ya soka duniani.

Matokeo ya mechi za jana

Kundi E

Ujerumani 1 Japan 2

Hispania 7 Costa Rica 0

Kundi F

Morocco 0 Croatia O

Ubelgiji 1 Canada 0

 

Ratiba mechi za leo

Kundi G

Switzerland v Cameroon – saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki

Brazil v Serbia – saa 4:00 Usiku

 

Kundi H

Uruguay v Korea Kusini – Saa 10:00 jioni

Ureno v Ghana – Saa 1:00 usiku

Ujerumani imetengeneza ‘chatu’ wake na kumezwa

Japan imeweka historia kwa kuichapa Ujerumani 2-1 jana mchezo wa kundi E. Wachezaji watano kati ya 11 waliocheza jana dhidi ya Ujeruamni wanacheza soka nchini Ujerumani wakiwemo Ritsu Doan wa Freiburg na Takuma Asano wa Bochum, ambaye alitokea benchi na kufunga.

Koch awa Japan amesema "Tunaamini ligi hizi (ikiwemo bundasliga ya Ujerumani) zimesaidia kuwajenga wachezaji wa Japan, tunaheshimu hilo. Haijalishi mpinzani gani, tunapambana kushinda’.

Gavi afikia rekodi iliyowekwa miaka 64 na Pele

Akiwa na miaka 18 na siku 110 days, Gavi ni mchedzaji kinda zaidi kuwahi kuichezea Hispania katika michuano ya kombe la dunia nagoli lake tamu alilofunga jana dhidi ya Costa Rica limemfanya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga kwenye historia ya michuano hiyo, tangu afanye hivyo gwiji la Brazil, Pele miaka 64 iliyopita, kwneye kombe la dunia la mwaka 1958.

Ujerumani kutopigwa faini kwa kuziba midogo

Wachezaji wa Ujerumani walifunika kwa mkono midomo yao, wakati wa picha rasmi za kabla ya mchezo wao dhidi ya Japan, ili kupinga kunyamazishwa na Shirikisho la soka duniani, Fifa. Kabla ya kuanza mashindano Fifa, ilitaka timu zinazoshiriki zijielekeze kwenye mechi zao na sio kuzungumza  masuala mengine. Hilo linapingwa na wengi.

Mwenyeji Qatar ananyooshewa kidole kwa kuminya haki za binadamu, ikiwemo na namna wanavyohukuliwa watu wanaojihusishwa na mapenzi ya jinsia moja, kuuawa kwa wafanyakazi wahamiaji wakati wa ujenzi wa viwanja na mengine. Katika kupinga hilo manahodha wa timu za Ulaya walipanga kuvaa kitambaa kilichoandika OneLove. Fifa imekataa

"Ilikuwa ishara, na tulitaka kufikisha ujumbe. Tulitaka kufikisha ujumbe kwamba Fifa inatunyamazisha," alisema kocha wa Ujerumani Hansi Flick baada ya kipigo cha kushangaza cha mabao 2-1 toka kwa Japan.

Fifa imesema haitaiadhibu Ujerumani kwa ilichokifanya.