Lisandro Martinez: Mfahamu beki 'katili' wa Man United

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamekubali kumsaini beki wa Ajax na Argentina Lisandro Martinez, aliyepatiwa jina la Utani 'Butcher of Amsterdam'.
Hivyobasi tunauliza watarajie nini?
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 , alishinda mataji mawili ya ligi ya Uholanzi katikia kipindi misimu mitatu chini ya kocha Erik ten Hag akiichezea Ajax na kwasasa ndio mchezaji bora wa mwaka na amemfuata mkufunzi huyo Old Trafford.
Licha ya kuwa nimo cha urefu wa Futi tano na nchi 9, alifamikiwa kushinda mipira mingi hewani katika ligi hiyo zaidi ya harry maguire msimu uliopita na alifanikiwa kuwapokonya mipira washambuliaji mara nyingi zaidi ya beki yeyote yule.
Je ubora wake ni wa kiwango gani?

Takwimu za pasi
Takwimu za Martinez zinalinganishwa vyema na wachezaji wenzake wapya, ingawa hilo linafaa kuthibitishwa na ukweli kwamba alicheza katika Eredivisie ya Uholanzi, ligi iliyoorodheshwa ya saba na Uefa.
Alitumia msimu mzima uliopita kama beki wa kati lakini kampeni zake mbili za kwanza akiwa Ajax, baada ya kuhama kutoka Argentina 2019, zilimfanya ashiriki katika nafasi za beki wa pembeni na kama kiungo mkabaji.
Martinez aliorodheshwa juu zaidi ya mabeki wengine wa United kwa dakika 90 za ligi kwa pasi za mbele, pambano la angani aliloshinda, kuingilia kati na kupokonya mpira msimu uliopita. Pia alishinda makabiliano mengi na kukamilisha chenga nyingi zaidi kuliko mabeki wa kati wa United.
Licha ya kuwa mfupi kwa inchi saba kuliko Maguire - na kucheza mechi chache sita za ligi kwa sababu ya jeraha - Martinez bado aliweza kushinda mapambano 80 ya angani dhidi ya 75 ya Maguire.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mtaalamu wa kandanda wa Uholanzi James Rowe alisema: "Martinez amepata umaarufu mkubwa Amsterdam tangu kuhamia Ajax kutoka timu ya Defensa y Justicia na alifanikiwa kuwa sehemu ya timu iliyoshinda PSV 2-0 kwenye kombe la Johan Cruyff la 2019.
"Kilichojitokeza mara moja ni utulivu wakeanapogusa mpira, kujiamini katikati ya safu ya ulinzi na utoaji wake wa pasi nyingi.
"Amsterdam kwa kweli imekuwa nyumbani kwa Martinez. Hakika si rahisi kuhama kutoka Amerika Kusini hadi soka la Uholanzi na tofauti zote za kitamaduni zinazotokana na hilo ndani na nje ya uwanja, lakini Lisandro amechukua kila kitu katika juhudi zake. Pia amefikia kilele chakebaada ya kuchaguliwa na nchi yake, akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Venezuela mnamo 2019.
"Anaondoka Ajax akiwa na sifa chungu nzima, mataji mawili ya Eredivisie na Kombe moja la Uholanzi - na jinsi anavypendwa na mashabiki wa Ajax.
"Sababu kubwa ya kuhamia United itakuwa ni Ten Hag, ambaye amekuwa na imani naye kila wakati. Ten Hag anapenda wachezaji wake kutafuta suluhu uwanjani wakati wowote ili kupata nafasi nzuri ya kushinda mechi, na amempata beki wa kati ambaye atafanya hivyo.
"Wengine wanaweza kuashiria urefu wake wa futi 5 na inchi 9, lakini atazoea haraka mahitaji ya Ligi Kuu na atafurahia changamoto zake. Pia itakuwa ni hali ya kifahari kwa kijana kutoka Gualeguay ambaye alipitia timu ya vijana. A lijipanga na kucheza kwa mara ya kwanza akiwa Newell's Old Boys na amefanikiwa kufika Ligi Kuuya Uingereza.
"Nina uhakika kama mlinzi atazidi kuimarika katika ngazi ya klabu na kimataifa."
Martinez alihusika katika mabao manne (bao moja na asisti tatu), nyingi kama walinzi wowote wa United.
Licha ya jina lake la utani, alionyeshwa kadi sita pekee za njano katika mechi 36 za mashindano yote msimu uliopita, ikiwa ni chini ya Luke Shaw (11) na Maguire (tisa) na sawa na Diogo Dalot. Raphael Varane, alipewa kadi mara moja tu.
Katika nukuu zilizoripotiwa kwenye gazeti la Mirror mwezi huu, Martinez alisema: "Naitwa carnicero - Butcher - wa Amsterdam. Sisi Waajentina tunafanya kila kitu kwa mapenzi na ninapokuwa uwanja napigania kila mpira. Ikibidi kukanyaga maiti, mimi hufanya hivyo.
"Nataka kushinda kila pambano la 50-50 kwa sababu najua kwamba ninapigania chakula kwa kila mwanafamilia yangu na marafiki zangu. Hiyo ndiyo hisia niliyo nayo - na kila Mwargentina anayo. Ni aina ya motisha ambayo siwezi. kueleza."

Je ni wapi atacheza vyema United?
Martinez anakuwa mmoja wa mabeki sita wakuu wa kati Old Trafford, akiwemo nahodha Maguire, Varane, Victor Lindelof na Eric Bailly ambaye amekuwa na majeruhi mara kwa mara na Phil Jones, ambaye alicheza mechi nne za Premier League kila msimu uliopita.
Kuwasili kwa Martinez huenda kukasababisha mabadiliko katika safu ya ulinzi ya United . Ten Hag anapendelea mbinu ya 4-3-3 , hivyobasi kuna uwezekano mkubwa akacheza na beki wawili pekee wa kati.
"Tayari inaonekana kuwa vitendo vinazungumza zaidi kuliko maneno kwa kocha Ten Hag," alisema Simon Stone wa BBC Sport.
"Hajasema mengi kuhusu Maguire. Amethibitisha Muingereza huyo ataendelea na unahodha lakini hajaeleza kwa hakika mawazo yake, wala sifa anazoziona kwa Maguire.
"Hata hivyo, tayari amefanya mabadiliko muhimu sana ambayo yanaonyesha kile kitakachojiri.
"Kwa muda wake wote Old Trafford, Maguire amecheza upande wa kushoto wa safu ya ulinzi ya watu wawili, mara nyingi Lindelof akiwa upande wa kulia.
"Katika ushindi wa mechi ya kirafiki siku ya IJumaa dhidi ya Melbourne Victory walibadilishana nafasi. Hakuna maelezo yaliyotolewa lakini sababu yake inaonekana wazi.
"Lisandro Martinez ni beki wa upande wa kushoto. Ni nafasi hiyo ndio aliocheza chini ya Ten Hag huko Ajax. Njia inaonekana kuwa safi kwake kuja moja kwa moja kwenye timu."












