Raheem Sterling: Kwanini Man City wanamuuza na kwanini Chelsea wanamsajili?

Chanzo cha picha, Getty Images
Raheem Sterling atakuwa mchezaji wa pili msimu huu kuondoka Manchester City na kujiunga na mojawapo ya timu kuu sita katika ligi ya Uingereza baada ya kuafikia makubaliano ya kibinafsi na Chelsea.
Baada ya pia kumuuza Gabriel Jesus kwenda Arsenal na kumsaini Halaand kutoka Borrusia Dortmund, City itakuwa tofauti katika safu ya mbele.
Chelsea pia itakuwa na muonekano mpya, huku mshambuliaji wa England Raheem Sterling akijiunga na miamba hiyo baada ya Romelu Lukaku kurudi Inter Milan.
Hivyobasi tunauliza Sterling amewacha nini City , kwanini anaondoka na ni nini atapeleka Chelsea?
Je, atakumbukwa vipi akiwa City?

Chanzo cha picha, BBC Sport
City wameshinda mataji 29 makubwa katika historia yao, 12 kati ya hayo Sterling akiwa huko - ikiwa ni pamoja na mataji manne kati ya manane ya ligi, matano kati ya nane ya Kombe la Ligi na moja la Kombe la FA.
Anaondoka akiwa na mabao 131 na asisti 74 katika mechi 339 katika misimu saba baada ya kuhama kutoka Liverpool.
Pia amekuwa sehemu muhimu sana ya uongozi wa Pep Guardiola, akimchezea (292) raia huyo wa Catalan kuliko mtu mwingine yeyote.
Ni Lionel Messi (211) na Sergio Aguero (124) pekee ambao wamefunga mabao mengi zaidi wakimchezea Guardiola kuliko 120 ya Sterling. Pia ni wa tatu kwa asisti, akiwa na 66, nyuma ya Kevin de Bruyne (105) na Messi (80).
"Amekuwa mchezaji muhimu sana katika misimu hii yote, mwenye mabao na pasi za mabao, na anapojiamini ni mchezaji muhimu sana," alisema Guardiola msimu uliopita.
Lakini pamoja na hayo, Sterling hajawahi kujionyesha kama gwiji machoni mwa mashabiki wa City.
"Sterling hajawahi kuwa kipenzi cha watu wengi, jambo ambalo ni gumu kulielezea kwani kwa sasa ameshinda mataji mengi ya Ligi Kuu ya England kuliko mchezaji yeyote asiye wa Manchester United isipokuwa John Terry na Fernandinho," alisema Simon Stone wa BBC Sport.
"Ubora wake umekuwa wa kusuasua. Wakati mwingine anaonekana kuwa mzuri sana, mara nyingine anaweza kupotea kabisa na bado anakosa nafasi mbele ya lango. Hata hivyo anabaki kuwa hatari akiwa na mpira miguuni mwake na siku zake bora bado zinaweza kuwa mbele.
"Anaweza kuwa mmoja wa wachezaji ambao wakati wao katika City unathaminiwa zaidi katika kumbukumbu kuliko ilivyokuwa wakati huo."
Kwanini ManCity inamuachilia kuondoka?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kiwango kikubwa cha mafanikio ya Sterling katika City kinazua swali la wazi - kwa nini wanamruhusu kuondoka na kujiunga na mpinzani anayewa kutoa ushindani mkubwa ?
Kuna mambo mawili makubwa. Moja ni ukweli kwamba mkataba wake unakamilika msimu ujao kwa hivyo hii ilikuwa nafasi ya mwisho ya kujipatia pesa – Jambo jingine ni usajili wa Haaland.
City mara nyingi wamecheza bila mshambuliaji halisi katika misimu michache iliyopita huku Aguero akijeruhiwa, na kisha kujiunga na Barcelona.
Lakini usajili wa pauni milioni 51 wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Haaland, ambaye amefunga zaidi ya mabao 150 akiwa na umri wa miaka 21, hakika utabadilisha yote hayo.
Ni mechi tisa tu kati ya 47 za Sterling msimu uliopita ambazo zilikuwa kwenye safu ya kati , lakini Phil Foden - ambaye alikuwa mshambuliaji wa kati mara 19 - alichukua nafasi ya winga muda mwingi.
Sterling alianzishwa mechi 23 pekee za Ligi Kuu msimu uliopita - na hiyo ilikuwa bila Haaland katika klabu hiyo.
"City haikutaka aondoke na ingefurahi kusalia kwake," aliongeza Stone. "Lakini pia alitaka kuwa sehemu muhimu ya timu inayoshindana katika kiwango cha juu. Pep kamwe asingeweza kuhakikisha hilo.
"Kwa kweli, wangeuzwa kwa klabu isiyo ya Ligi ya Premia. Hata hivyo, kama Chelsea wangekuwa tayari kulipa zaidi ya mtu mwingine yeyote kwa mchezaji ambaye angeweza kuondoka bure katika muda wa miezi 12, kifedha, ni jambo la maana."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Je atachezeshwa katika nafasi gani Chelsea?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kitu kimoja ambacho Chelsea watakuwa wakipata ni mabao na pasi za mabao, kitu ambacho wamekikosa licha ya mafanikio waliyopata hivi karibuni.
Mara ya mwisho kwa mchezaji wa Chelsea kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja kuliko Sterling - katika ligi na katika mashindano yote - alikuwa Diego Costa mnamo 2016-17.
"Kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao, Sterling anaweza kuonekana kuwa bora zaidi kwa wale ambao tayari wapo na kufidia upungufu ulioachwa na Lukaku," alisema mtangazaji wa BBC Sport Alistair Magowan.
"Pia anawakilisha taarifa ya nia kutoka kwa wamiliki wapya, ambao wanaeleweka kuwa na mipango kabambe katika soko la uhamisho.
"La muhimu zaidi, ni usajili wa kwanza kufanywa na Tuchel tangu apewe mamlaka zaidi chini ya mmiliki mwenza na mkurugenzi wa muda wa michezo Todd Boehly kufuatia kuondoka kwa mshauri wa kiufundi na utendaji Petr Cech na mkurugenzi Marina Granovskaia, ambao walishughulikia mazungumzo."
Tangu 2017-18, mshambuliaji huyo wa Uingereza amefunga mabao 110 na kutengeneza mengine 51 katika mashindano yote akiwa na City.
Olivier Giroud (39) - sasa yuko AC Milan - na Eden Hazard (38) wanasalia kuwa wafungaji bora wa Chelsea katika muda huo. Hazard aliondoka kwenda Real Madrid miaka mitatu iliyopita. Willian, aliyeondoka miaka miwili iliyopita, ndiye msaidizi wao bora akiwa na 31.
Sterling anaweza kuingia kama nambari tisa wa uongo, mfumo ambao kocha wa Chelsea Tuchel anaonekana kuupendelea. Kuna uwezekano mkubwa zaidi Chelsea kucheza bila mshambuliaji sahihi baada ya kumtuma mfungaji bora wa msimu uliopita Lukaku kwa mkopo kwenda Inter Milan.
Msimu uliopita Sterling aliangushwa mara nyingi zaidi kwenye eneo la kisanduku cha wapinzani (8.93) kwa dakika 90 kuliko mshambuliaji yeyote wa Chelsea ambaye amesalia kwenye klabu hiyo.
Pia alijaribu na kukamilisha chenga nyingi zaidi kuliko washambuliaji wowote wa Blues. Hakim Ziyech na Mason Mount walicheza pasi nyingi kuliko Sterling na - licha ya kufunga mabao mengi - Sterling alipiga mashuti machache kuliko Ziyech, Timo Werner, Mount na Kai Havertz kwa dakika 90.
Chelsea tayari wana chaguo mbadala kwenye safu ya ushambuliaji, lakini wanahitaji mtu ambaye hutengeneza na kufunga mabao mara kwa mara.
"Kuwasili kwa Sterling kutasababisha maswali kuhusu mustakabali wa washambuliaji wa pembeni Werner, Christian Pulisic na Ziyech," alisema Magowan.
"Wote walisajiliwa kabla ya Tuchel kuteuliwa katikati ya msimu wa 2020-21.
"Pamoja na Sterling, shinikizo la ziada litakuwa kwa Tuchel. Meneja atahitaji magoli kurejeshwa, lakini mafanikio ya usajili yanaweza pia kutegemea Werner, Pulisic au Ziyech pia kuondoka kwenye klabu, ambayo itaepuka kuchanganyikiwa kwa muda wa kucheza na kusaidia kusawazisha vitabu vilivyo chini ya umiliki mkubwa wa hisa za kibinafsi."












