Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Masuala muhimu yatakayojadiliwa katika meza ya mazungumzo kati ya Rais William Ruto na Raila Odinga
Na Abdalla Seif Dzungu
Mazingira ya utulivu yamerejea tena nchini Kenya baada ya wiki mbili za hali ya tumbo joto kutokana na maandamano ya upinzani yalioongozwa na kiongozi wa azimio Raila Odinga dhidi ya serikali ya rais William Ruto.
Wakati wa maandamno hayo yaliofanyika kila Jumatatu na Alhamisi, Maafisa wa Polisi walikabiliana na waandamanaji kwa kuwarushia vitoa machozi , huku não waandamanaji wakiwarushia maafisa wa polisi mawe.
Katika ghasia hizo takriban watu watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi na raia wawili walipoteza maisha yao huku mali yenye thamani ya isiojulikana ikiharibiwa ikiwemo msikiti na na kania ,shamba la rais mstaafu Uhuru Kenyatta la Northlands pamoja na kampuni ya Spectre ya Raila Odinga.
Mamia ya waandamanaji walikamatwa wakati wa ghasia hizo ambazo zilivutia shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa baada ya baadhi ya maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kuwashambulia waandishi habari waliokuwa wakizipeperusha habari hizo moja kwa moja.
Na kufuatia hatua hiyo baadhi ya viongozi wa kimataifa ikiwemo makanisa walianzisha shinikizo za kuwataka viongozi wawili wakuu rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kurudi nyuma kila mmoja kukaa katika meza ya majadiliano.
Hatahivyo viongozi hao wawili walionyesha misimamo mikali inayoungwa mkono na pande pinzani huku Raila akisema kwamba hayuko tayari kufanya handishake na serikali haramu, naye Rais William Ruto akisisitiza kwamba serikali yake haitakubali kushinikizwa kuingia katika makaubaliano ya handshake.
Na maandamano hayo yalipoendelea kuathiri uchumi kupitia kuwatia hofu wafanyabiashara na hata wawekezaji , hatimaye Rais William Ruto alikubali kuwasiliana na mwenzake Raila Odinga kuweka tofauti zao kando na kuanzisha majadiliano ili kusuluhisha mgogoro uliopo.
Hatahivyo kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliwasilishwa katika meza ya majadiliano baadhi ya masuala nyeti aliyotaka kuangaziwa katika mazungumzo hayo yatakayoongozwa na kamati ya bunge isiopendelea upande wowote.
Yafuatayo ni baadhi ya mahitaji yaliowasilishwa na Kinara wa Muungano wa Azimio Raila Odinga katika meza ya majadiliano.
Kuundwa kwa tume ya Uchaguzi ya IEBC isioegemea upande wowote
Raila aliyeunga mkono kamati hiyo ya bunge isiopendelea upande wowote pia alisisitiza kurudishwa kazini kwa makamishna wanne .
Akizungumza na vyombo vya habari katika afisi yake ya Capitol Hill, alisema kwamba sio haki kwa Juliana Cherera, Francis Wanderi ,Justus Nyagaya, na Irene Masit kutumika vibaya kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa 2022.
Watatu kati ya makamishna hao wa IEBC walilazimika kujiuzulu huku mmoja wao Iren Masit akiondolewa katika wadhfa wake na jopo lililobuniwa kuchunguza utendakazi wao katika uchaguzi wa 2022.
Hatua hiyo inajiri baada ya makamishna hao wa zamani kutofautiana na wenzao wawili wakiongongozwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chabukati wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Makamishna hao wa zamani walitofautiana na matokeo ya mwisho ya urais yalioonesha kwamba Rais Willima Ruto ndiye aliyeshinda uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga.
“Hatutaki kuona unyanyasaji wa makamishna 4 waliotolewa kafara. Tunataka makamishna hao warejeshwe kazini ili tuweze kuhamia kama nchi kwa njia moja na ya umoja,” alisema bwana Odinga.
Mkurugenzi wa idara ya jinai kusitisha uchunguzi na kukamatwa kwa waandamanaji
Akiunga mkono hatua ya rais William Ruto kuitisha majadiliano Raila pia alimtaka Mkurugenzi wa Idara ya Jinai nchini DCIO kusitisha uchunguzi na ukamataji wa waandamanaji wakat iwa maandamnao hayo ya upinzani.
"Katika kukubali wito wa mazungumzo, tunaomba kwamba kukamatwa na mashtaka yote yanayohusiana na maandamano yetu kukomeshwa mara moja," alisema.
Polisi katika Kaunti za Kisumu na Migori walikuwa wamewakamata washukiwa 14 kuhusiana na ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano ya kupinga serikali
Mkurugenzi wa idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika taarifa yake alisema kwamba washukiwa wawili wanadaiwa kuwa sehemu ya majambazi waliovamia duka moja kubwa huko kisumu..
Wawili hao tayari walikuwa wamefikishwa katika Mahakama ya Kisumu na wapelelezi walipewa amri ya kuwazuilia kwa siku 10 zaidi huku wakiendelea na uchunguzi.
Washukiwa wengine 12 walikamatwa katika eneo bunge la Suna Mashariki baada ya kudaiwa kuweka vizuizi kwenye barabara kuu na kuwaibia wananchi pesa.
Kupunguzwa kwa gharama ya maisha
Kabla ya kuanza kwa maandamano wiki mbili zilizopita kiongozi wa upinzani Raila Odinga alitoa makataa ya wiki mbili kwa serikali ya rais William Ruto kupunguza gharama ya maisha mbali na kukabiliana na kiangazi ambacho kimewaacha takriban Wakenya milioni 5.4 wakiwa wanakabiliwa na baa la njaa. Kiongozi huyo aliyesema kwamba maandamano hayo yatakuwa ya amani pia aliitaka serikali ya kupunguza kodi katika baadhi ya bidhaa na kurejesha mbinu ya ruzuku katika chakula kama vile unga, mafuta ya kupikia, petroli na umeme ili kuwapunguzia wakenya gharama ya maisha.
Katika hoja yake Raila anamtaka rais William Ruto kurudisha ruzuku katika biudhaa hiyo ambayo anadai ilitumia na serikali iliopita ili kupunguza bei za bidhaa. Rais William Ruto amekuwa akisema kwamba ruzuku iliotolewa katika bidhaa na serikali iliopita haikusaidia kupunguza bei za bidhaa na kwamba fedha hizo zilikuwa zikienda katika mifuko ya watu binafasi. Hatahivyo upinzani umeshikilia kwamba ni mbinu hiyo pekee ambayo ingepunguza bei za bidhaa muhimu nchini.
Kufunguliwa kwa Seva ya tume ya Uchaguzi IEBC
Wiki moja baada ya tume ya uchaguzi IEBC nchini Kenya kutanagaza matokeo ya uchaguzi wa 2022, ambapo ilimtangaza rais William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi huo, Muungano wa upinzani ukiongozwa na Raila Odinga ulikwenda mahakamani kupinga matokeo hayo kwa madai kwamba matokeo ya uchaguzi huo wa urais yaliingiliwa na watu aliodai kuwa raia wa kigeni.
Wakati wa kesi hiyo, Upinzani ulidai kwamba raia wa Venezuela Jose Camargo alikuwa akipakua matokeo ya fomu 34A za uchaguzi katika seva ya IEBC. Wakili wa Upinzani Julie Soweto alihoji jukumu la raia huyo wa Venezuela akidai kwamba ni yeye aliyeamua matokeo ya urais .
Vilevile Upinzani uliomba kufunguliwa seva za Tume hiyo ili kuchunguza kilichokuwa kikiendelea, agizo ambalo lilikubaliwa na ,mahakama ya juu lakini wakati wa uchunguzi uliokuwa ukiendelea katika seva hizo , wamiliki wa kampuni iliokuwa ikimiliki seva hizo walikata kuonyesha kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika seva hizo wakidai kwamba hatua hiyo ingehujumu kazi yao.
Suala hilo lilizua wasiwasi mkubwa miongoni mwa viongozi wa upinzani waliotaka IEBC kufunga seva hizo iwapo ni kweli Rais William Ruto alishinda uchaguzi huo kwa haki.