Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Man United Wamlenga kiungo wa Crystal Palace

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wanafikiria iwapo watawasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 21. (Talksport).

Inter Milan wamekataa dau la euro 50m (£43m) kutoka kwa Chelsea kumnunua mlinzi wa Italia Alessandro Bastoni, 26. (La Gazzetta dello Sport)

Kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 22, ameiambia klabu hiyo kwamba anataka uhamisho wa kwenda Chelsea, licha ya kutakiwa na Bayern Munich na Manchester City. (ESPN)

AC Milan wana nia ya kusukuma dili la euro 35m (£30.2m) kwa mshambuliaji wa Denmark na Manchester United Rasmus Hojlund, 22, lakini pia wanamfikiria fowadi wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 25, kama mbadala wake. (La Gazzetta dello Sport)

Beki wa kulia wa Manchester City na England Rico Lewis, 20, anasema hana nia ya kuondoka katika klabu hiyo licha ya Nottingham Forest kumtaka. (Mail)

Kipa wa Cameroon Andre Onana, 29, aliachwa nje katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Manchester United dhidi ya Arsenal huku klabu hiyo ikifikiria kuchukua hatua ya kushtukiza kumrejesha mlinda lango wa Uhispania David de Gea, 34, katika klabu hiyo kutoka Fiorentina. (The sun).

Hata hivyo, United wamekabidhi pesa zao za uhamisho kwenye nyadhifa nyingine baada ya kuuliza kuhusu kipa wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 32, na mlinda lango wa Paris St-Germain na Italia Gianluigi Donnarumma, 26. (Telegraph - subscription Required).

Mshahara wa Jadon Sancho ndio kigezo muhimu katika uhamisho wa £20m kutoka Manchester United kwenda Roma. Winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 ana hamu ya kuona kama klabu nyingine yoyote itaingilia kati na kufikia mshahara wake wa kila wiki wa takriban £250,000. (TeamTalks)

Roma pia wamefanya mawasiliano na Manchester United kuhusu dili la beki wa kushoto wa Uholanzi Tyrell Malacia, 26, ambaye pia anavutia Besiktas. (Fabrizio Romano)

Atalanta wanatumai kufutilia mbali mkataba na Fulham kumsaini fowadi wao Mbrazil Rodrigo Muniz, 24, kwa takriban euro 40m (£34.5m) Jumatatu. (TeamTalks),

Mshambulizi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, amekubali kukatwa mshahara ili kujiunga na Juventus kutoka Paris St-Germain, kwa mkataba wa takriban euro 60m (£51.8m). (Corriere dello Sport In Italy)

Tottenham wanafikiria kumnunua winga wa Real Sociedad na Japan Takefusa Kubo mwenye umri wa miaka 24 huku Thomas Frank akijaribu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Fichajes - In Spanish)

Burnley na Sunderland wote wanavutiwa na beki wa kati wa FC Copenhagen Mbrazil Gabriel Pereira, 25. (Teamtalk).

Arsenal wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona Frenkie de Jong, 28, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ukitarajiwa kumalizika msimu ujao wa joto. (Fichajes - In Spanish)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla