Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: 09.12.2022, Garnacho, Sommer, Endrick, Ziyech, Leao
Real Madrid wanavutiwa na winga wa Manchester United Alejandro Garnacho - Muargentina mwenye umri wa miaka 18 ambaye alifunga bao lake la kwanza la Premier League dhidi ya Fulham mwezi uliopita. (Revelo - in Spanish)
United pia wanashughulikia mpango wa kumsajili kipa wa Borussia Monchengladbach na Uswizi Yann Sommer, 33, kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (ESPN)
Real Madrid wamekubali mkataba wa miaka sita wenye thamani ya karibu £62m kumsajili kijana wa Brazil Endrick kutoka Palmeiras, lakini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 16 hatajiunga na klabu hiyo hadi Julai 2024 atakapokuwa na umri wa miaka 18. (Fabrizio Romano )
AC Milan wako tayari kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Hakim Ziyech, 29, ambaye amefanya vyema kwenye Kombe la Dunia akiwa na Morocco. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)
AC Milan itampa changamato mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 23, Januari - kusaini mkataba mpya au kuondoka. (Calciomercato - in Italian)
Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 25, anaweza kutafutwa na klabu hiyo ya Ufaransa msimu ujao. (Sky Sports)
Akiwa tayari amefunga mabao matatu kwenye Kombe la Dunia, Muingereza Rashford anasema hakuna kitu zaidi ya kuifungia nchi yake. (Mirror)
Al-Khelaifi pia alisema ana uhakika mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, angeongeza muda wake wa kukaa Paris watakapojadili mustakabali wake Januari. (Sky Sports)
Arsenal "itaangalia machaguo yaliyopo" baada ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus kupata jeraha la goti kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar, anasema meneja Mikel Arteta. (Football London)
Kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 26, ndiye anayelengwa na Newcastle katika uhamisho wa Januari. (90 min)