Liz Truss au Rishi Sunak kutangazwa kuwa Waziri Mkuu mpya ajaye wa Uingereza

Iliyochapishwa

Mrithi wa Boris Johnson kama waziri mkuu wa Uingereza atajulikana baadaye wakati mmoja kati ya Liz Truss au Rishi Sunak atakapoteuliwa kuwa kiongozi ajaye wa Conservative ambaye atakuwa waziri mkuu pia mpya.

Saa 8 mchana leo atatangazwa mmoja kati ya hao kshika kiti hicho kabla ya kuanza kazi kesho Jumanne. Waziri Mkuu mpya anakwenda kurithi uchumi unaoendelea, na mfumuko wa bei wa juu kabisa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Waziri wa Mambo ya nje Liz Truss anayepigiwa chapuo kushinda kiti hicho, ameahidi kusaidia zaidi katika kuwalinda walaji ndani ya wiki moja baada ya kuchukua nafasi hiyo.

Kisha anapanga kutoa £30bn kufidia punguzo la kodi kupitia Bajeti ya dharura baadaye mwezi huu, akisema mzigo wa kodi wa Uingereza unafifisha ukuaji.

Mpinzani wake, kansela wa zamani Bw Sunak, anayeashiria kushindwa, akisema kazi yake "sasa ni kuunga mkono serikali ya Conservative".

Bi Truss bado hajatoa maelezo ya kina ya mpango wake wa gharama ya maisha zaidi ya kusema kuwa ataondoa kwa muda ushuru wa kijani kwenye bili za nishati na kubadilisha ongezeko la Bima ya Kitaifa iliyoletwa wakati wa uongozi wa Bw Johnson.

Bw Sunak alitangaza malipo ya £15bn kama kansela, ikiwa ni pamoja na malipo ya £400 kwa kaya zote, lakini wagombea wote wamesema msaada zaidi utahitajika baada ya utabiri wa gharama kuongezeka zaidi katika majira ya joto.

Siku ya Jumapili waziri wa mambo ya nje alikataa kusema kama msaada zaidi utakuwa wa wote au utaelekezwa kwa wahitaji zaidi, akisema atahitaji muda ofisini ili kutoa maelezo ya mpango wake.

Alikiri kutochagua kupanda kwa Bima ya Kitaifa kutawanufaisha watu wa kipato cha juu zaidi, lakini alisema ni haki kwa sababu kutakuza uchumi kwa ujumla.

Vyama vya Labour, Liberal Democrats na SNP wametoa wito kwa serikali kusimamisha bei ya nishati kupitia ruzuku ya mabilioni ya pauni, wakati Greens wamependekeza kutaifisha wasambazaji watano wakubwa wa Uingereza.

Bi Truss hapo awali ameelezea wazo hilo kama "plasta ya kubandika" na anasema inahitaji kufanywa zaidi ili kusaidia Uingereza kuongeza vyanzo vyake vya nishati.

Alisema msaada wowote zaidi utalazimika kwenda "bega kwa bega" na juhudi za kuongeza nishati ya nyuklia, na uchimbaji zaidi wa mafuta na gesi katika Bahari ya Kaskazini.

Pamoja na kupunguzwa kwa kodi, Bi Truss ameahidi kutoa maeneo ya uwekezaji yenye masharti nafuu na kuleta kuwekeza zaidi kwenye eneo la

Kinyang'anyiro hicho cha wiki saba cha uongozi kinamaliza msukosuko wa miaka mitatu ya Bw Johnson madarakani, na kumewafanya wagombea hao kuskosoana sera zao mara kwa mara sera.

Bw Johnson alilazimishwa kuachia ngazi mwezi Julai kufuatia msururu wa kashfa, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili na nusu tu baada ya kuongoza chama chake na kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa 2019.

Sehemu ya awali ya wagombea 11 ilipunguzwa hadi kubakia wawili katika kufuatia kura za wabunge, huku duru ya pili itaamuliwa na wanachama, ambao wanafikia takriban 160,000.

Ingawa Bw Sunak aliungwa mkono zaidi na wabunge wa chama hicho, lakini yuko nyuma ya Bi. Truss kwenye kura za maoni za mashinani za chama.

Bw Johnson anatarajiwa kutoa hotuba ya kuaga baada ya kung'atuka madarakani Jumanne, kabla ya makabidhiano ya mamlaka kufanyika.

Kawaida kiongozi wa aina hii hupewa baraka za uteuzi wake na Malkia katikakasri la Buckingham lakini safari hii atakayechaguliwa itamlazimu kusafiri mpaka Kasri la Balmoral huko Scotland ili kuteuliwa na Malkia ambaye sasa yuko huko.