Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 24.06.2024
Bayern Munich wanavutiwa na Bernardo Silva na Borussia Dortmund wanakaribia kufikia makubaliano ya Pascal Gross, huku Arsenal na Chelsea wakimlenga Nico Williams.
Bayern Munich wana nia ya kumsajili winga wa Ureno Bernardo Silva, 29, ambaye ana kipengele cha kumnunua cha £50m katika kandarasi yake huko Manchester City, ambayo bado ina miaka miwili kukamilika. (Star)
Borussia Dortmund wanakaribia kufikia makubaliano ya mdomo na kiungo wa kati wa Brighton kutoka Ujerumani Pascal Gross, 33, ambaye amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake. (Sky Sport Germany)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anaweza kukasirisha baadhi ya wachezaji wake waandamizi ikiwa klabu hiyo itamnunua winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, kutokana na mahitaji ya mshahara ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Express).
Chelsea pia wanavutiwa na Williams, ingawa ni miongoni mwa wanaolengwa na Paris St-Germain baada ya kuondoka kwa fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, kwenda Real Madrid. (TeamTalks).
Manchester United na Liverpool zote zimewasilisha ombi la kumnunua Leny Yoro wa Lille lakini beki huyo wa Ufaransa, 18, anataka kujiunga na Real Madrid. (Marca – In).
Liverpool, Manchester City na Arsenal ni miongoni mwa klabu tano ambazo bado zinawania kumnunua Joshua Kimmich iwapo kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 29, ataondoka Bayern Munich. (Sky Sport Germany).
Mshambulizi wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy ameombwa kuwa sehemu ya jopo la ukufunzi la kocha Erik ten Hag. (Fabrizio Romano).
Newcastle United wanapanga kumuuza Callum Wilson, 32, ikiwa watakubali dili la kumsaini mshambuliaji mwenza wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, kutoka Everton. (Football Insider).
Lyon wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Gambia Yankuba Minteh, 19, kutoka Newcastle. (Fabrizio Romano)
Minteh anaripotiwa kuafikiana na moja ya klabu nyingi ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili. (chronicle).
Nottingham Forest wameanza mazungumzo na Aston Villa kuhusu mpango wa kumnunua beki wa Uholanzi Lamare Bogarde, 20. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla