Israel - Hamas: "Baba, tuko vitani.' Ilikuwa mara ya mwisho kumsikia"

sax

Chanzo cha picha, COURTESY OF FAMILY.

Maelezo ya picha, Ivonne Rubio na Antonio Macías, wana ndoa kutoka Colombia hawajuulikani walipo
Iliyochapishwa

Ndugu wa walioteweka kutoka Amerika Kusini - wakati wa shambulio la wanamgambo wa Palestina, Hamas dhidi ya Israel siku ya Jumamosi, wamekata tamaa huku wakifanya juhudi zote za kuwatafuta wapendwa wao.

Hawaonekani hadi sasa, si katika hospitali au kwenye orodha ya marehemu. Mamia wameuwawa na maelfu kujeruhiwa huku kundi hilo likidai lina mateka zaidi ya 100 huko Gaza.

Kadiri saa zinavyopita na mashambulizi ya Israel huko Gaza yakiongezeka, wana mgambo wa Hamas, brigedi ya Al-Qassam, ilitangaza Jumatatu hii kwamba "itaanza kuwauwa mateka raia wa Israel kwa kila shambulio jipya la bomu ambalo Israel itafanya kwenye makazi ya raia bila kutoa taarifa ya awali ya onyo."

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na serikali ya Argentina, kuna zaidi ya raia kumi na mbili wamepotea na takribani saba wamekufa.

Serikali za Mexico, Brazili, Peru na Chile pia ziliripoti kutoweka kwa raia waliokuwa Israel wakati shambulio hilo lilipotokea. Ni tukio la vurugu zaidi katika eneo hilo katika miaka 50 iliyopita.

Raia wa Argentina, Itzik Horn, ambaye wanawe, Lair na Eitan, hawajapatikana tangu Jumamosi. Horn anadhani watoto wake walichukuliwa mateka na wanamgambo wa Hamas.

"Waliingia nyumba kwa nyumba katika eneo la Kibbutz, anakoishi mwanangu mkubwa. Wale ambao wangeweza kuchukuliwa, waliwachukua na wale ambao hawakuweza, waliwaua," aliiambia BBC kutoka mji wa Sderot, kilomita moja mpakani na Gaza.

Mwanawe mdogo alikwenda kumtembelea Lair wakati shambulio la kushtukiza lilipotokea. Kwa kuwa walikuwa hawapokei simu na hakuna mtu katika jamii aliyejua walipo, baba yao alianza msako.

"Watoto wangu hawaonekani. Hawako hospitalini, hawako kwenye orodha ya waliofariki. Nadhani walitekwa nyara."

Pia hapakuwa na ushahidi wa vurugu ndani ya nyumba hiyo. “Hakuna damu sakafuni wala chochote,” ishara inayothibitisha imani yake kwamba wao ni mateka.

"Niko tayari Hamas waniite, waniambie kuwa wana watoto wangu. Nataka kujua kwamba wako hai."

"Baba, baba, tuko vitani"

dcs

Chanzo cha picha, FACEBOOK

Maelezo ya picha, Raia wa Argentine, Ronit Rudman Sultan ni miongoni mwa waliouwawa

Takriban miili 260 ilipatikana katika eneo la tamasha karibu na mpaka na Gaza.

Katika sherehe hiyo kulikuwa na wanandoa wa Colombia ambao bado hawajapatikana. Ivonne Rubio (26) na Antonio Macías (29). Babake Ivonne, Julio Rubio, alisema familia "imevunjika moyo."

"Binti yangu alinipigia simu na kusema, 'Baba, baba, tuko vitani. Nitakimbia na kutafuta pakujificha.' Hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya mwisho kuzungumza naye."

"Ni ngumu kuishi wakati hujui binti yako yuko wapi," alisema katika mahojiano na BBC kutoka Jerusalem.

"Walikuwa ni vijana kwenye tafrija, hawahusiki, hakuna sababu ya kushambuliwa namna hiyo. Waliwapiga risasi wote, wakaacha mamia ya miili na wengine walichukuliwa mateka," aliongeza.

Kijana mwingine ambaye alikuwa na wanandoa hao alipatikana hospitalini, Rubio anasema, lakini hadi sasa hajaweza kusema lolote kwa sababu ameumia vibaya.

"Marafiki wa binti zangu wamefariki"

sd

Chanzo cha picha, COURTESY OF ITZIK HORN.

Maelezo ya picha, Ndugu wawili kutoka Argentine, Lair na Eitan Horn bado hawajaonekana
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Moja ya miji iliyoshambuliwa na Hamas ni Ashkelon, upo kilomita 20 kutoka kizuizi kinachotenganisha Israel na Ukanda wa Gaza. Watu wengie wa Amerika Kusini wanaishi huko.

Ana Harari, raia wa Colombia aliyehamia Israeli zaidi ya miaka 30 iliyopita - anafanya kazi katika kampuni ya kutengeneza vitu vya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo.

Harari alizungumza kwa simu na BBC kutoka Ashkelon kuhusu jinsi shambulio hilo lilivyotokea. Siku mbili baadaye, anasema, bado hajui kinachoendelea katika mitaa ya jiji lake.

"Hatujui kama kuna magaidi mitaani, hatujui ni kwa kiwango gani serikali inadhibiti eneo hili. Wakati wote tunasikia milipuko na ving’ora vinavyotuonya kuhusu makombora,” alisema huku baadhi ya milipuko ikisikika kwa nyuma.

"Kuna marafiki wa binti zangu ambao wamekufa na kupotea. Wanajeshi wenzake mwanangu, ambaye amemaliza utumishi wake wa kijeshi, pia wamekufa. Ni jambo la kutisha tunalopitia."

Mwaka mmoja uliopita, Harari aliyezaliwa katika manispaa ya Colombia ya Garzón, aliamua kuhamia Ashkelon, jiji lenye watu 132,000 kwenye pwani ya Israeli ya Mediterania.

"Kwa sababu tuko karibu sana na Gaza, sisi ndio mji wa kwanza ambapo makombora hufika wakati Hamas inaposhambulia," alisema.

"Shambulio hilo lilichukua muda mrefu zaidi. Na tulianza kusikia kwamba kuna uvamizi wa magaidi kupitia nchi kavu, majini, pamoja na milipuko ya mabomu."

Harari anasema alianza kusikia makombora yakipita juu ya nyumba yake. Na kisha wakaanza kugonga karibu na nyumba yake.

"Waliharibu gari langu, gari la majirani. Nyumba za watu wengine ninaowafahamu wanaoishi karibu ziliharibiwa vibaya," alisema.

Bila gari hakuweza kutoroka, kwa hiyo ilimbidi abaki katika nyumba yake bila maji au mahitaji muhimu kwa siku mbili.

"Tunachopitia ni cha kutisha. Hatujui kama wataingia kwenye nyumba zetu na kutuua kama walivyofanya katika maeneo mengine," alisema.

Mkazi mwingine karibu na Ukanda huo, Jessica Sharon, raia wa Argentina anayeishi katika mji wa Beit Oved.

Sharon ameishi Israeli miaka 20 iliyopita na ni msanii mzuri na mwalimu wa uchoraji.

"Tunasikia kwamba kuna mashambulizi. Tumefungiwa hapa na nataka tu kuondoka (nchini), kwa sababu hali itazidi kuwa mbaya," alisema.