Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 12.10.2024
Arsenal wanapanga kuwasilisha dau la kumnunua beki wa kushoto wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, mwenye umri wa miaka 20, na winga wa Cherries Antoine Semenyo mwenye umri wa miaka 24, mchezaji wa kimataifa wa Ghana. (CaughtOffside)
Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe, mwenye umri wa miaka 46, hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo licha ya kuwa miongoni mwa watu walioorodheshwa kwa ajili ya kazi ya kuinoa England ambayo iko wazi. (Telegraph - subscription required)
Kiungo wa kati wa England Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 19, anakaribia kukubali mkataba mpya katika klabu ya Manchester United. (Manchester Evening News)
Barcelona na Real Madrid zina nia ya kumsaini beki wa kushoto wa Uhispania Alvaro Fernandez, 21, ambaye Manchester United ilimuuza Benfica msimu uliopita. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 32, anatarajiwa kujiunga tena na klabu yake ya zamani Ajax wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao. (Sun)
Beki wa zamani wa Liverpool na taifa la Kameruni Joel Matip, 33, anafikiria kustaafu. (Ruhr Nachrichten S04 on X - in German), external)
Everton wamejiwekea malengo ya kumsajili winga wa Stuttgart na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Silas Mvumpa, mwenye umri wa miaka 26, mwezi Januari. (Football Insider)
Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, mwenye umri wa miaka 51, anafanya mazungumzo na "klabu kubwa" kuhusu kurejea katika kazi ya umeneja baada ya kukataa mazungumzo zaidi kuhusu kuionoa timu ya taifa ya Denmark. (Tipsbladet - in Danish), external)
Liverpool wamepangia kumchukua beki wa kati wa Palmeiras Vitor Reis, mwenye umri wa miaka 18, kama mchezaji wanayeweza kumsajili kwa siku za zijazo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ana kifungu cha kuvunja mkataba cha pauni milioni 84. (Football Insider)
Klabu ya River Plate ya Argentina inataka kuongeza muda wa mkopo wa mshambuliaji wa Manchester City. Echeverri mzaliwa wa Argentina, mwenye umri wa miaka 18, alisaini mkataba na City mnamo Januari 2024 kwa makubaliano kwamba angesalia katika River Plate kabla ya kuhamia Uingereza mnamo Januari 2025. (TYC Sports - in Spanish)
River Plate wanataka kuongeza muda wa mkopo wa mshambuliaji wa Manchester City Claudio Echeverri. Echeverri mzaliwa wa Argentina, mwenye umri wa miaka 18, alisaini mkataba na City mnamo Januari 2024 kwa makubaliano kwamba angesalia katika River Plate kabla ya kuhamia Uingereza mnamo Januari 2025. (TYC Sports - in Spanish)
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na dinah gahamanyi na kuhaririwa na Athumani Mtulya