Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 11.10.2024
Chelsea bado wanavutiwa na Victor Osimhen, Liverpool wanajiandaa kwa maisha bila Trent Alexander-Arnold, na Manchester United wanafikiria kumnunua tena Alvaro Fernandez.
Galatasaray hawana mpango wa kufanya uhamisho wa mkopo wa Mnigeria Victor Osimhen, 25, kutoka Napoli kuwa wa kudumu, lakini Chelsea bado wanavutiwa na mchezaji huyo. (Team Talk)
Mkurugenzi wa Napoli Mauro Meluso amethibitisha kuwa Osimhen yuko huru kuondoka klabuni hapo kwa bei sahihi mwezi Januari. (Metro)
Liverpool imewatambua Mholanzi wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 23, Vanderson wa Monaco, 23, na Mtaliano wa Fiorentina, Michael Kayode, 20 kama mbadala endapo watampoteza beki wao Trent Alexander-Arnold. (Caught Offside)
Hata hivyo, Liverpool wanapiga hatua katika mazungumzo yao ya mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Alexander-Arnold, 26. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, anaangazia mustakabali wake Arsenal licha ya kuhusishwa na uhaisho wa Saudi Arabia. (Caught Offside)
Manchester United wanatafakari iwapo wataanzisha kipengele cha kununua tena katika mkataba wa beki wa Uhispania Alvaro Fernandez, 21 na Benfica. (O Jogo - kwa Kireno)
Meneja wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel alitajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kuwa mrithi wa Erik ten Hag wakati uongozi wa soka wa Manchester United ulipokutana mapema wiki hii. (Independent)
Manchester City huenda wakamnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, ikiwa Barcelona watafanikiwa kumpata mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, kutoka Etihad Stadium. (Soka 365)
Newcastle wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 24, huku kukiwa na ushindani kutoka kwa wapinzani wa Ligi ya Premia. (Team Talk)
Liverpool wanapania kusaini mkataba mpya na mlinzi wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk huku kukiwa na uvumi ukiongezeka kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. (Football Insider)
The Reds wanaendelea kutathmini malengo ya uhamisho ili kuimarisha safu ya ulinzi ya Arne Slot, baada ya patia nafasi hiyo kipaumbele msimu ujao. Mfaransa wa Sevilla Loic Bade mwenye umri wa miaka 24 na mchezaji wa kimataifa wa Ureno Goncalo Inacio, 23, ni miongoni mwa wagombea. (Caught Offside)
Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekataa ombi la kujiunga na timu ya taifa ya Denmark kwa sababu yuko kwenye mazungumzo na klabu kubwa kuhusu nafasi ya kocha mkuu. (Tipsbladet)
Wolves wanafikiria kumnunua kocha wa Aberdeen Jimmy Thelin, iwapo wataamua kumfukuza Gary O'Neil. (Sun)
West Ham wameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na mlinda mlango wa Uingereza Fin Herrick, 18. (Football Insider)
Torino huenda wakamnunua mshambulizi wa Napoli Muargentina Giovanni Simeone, 29, kufuatia mchezaji wa Colombia Duvan Zapata mwenye umri wa miaka 33 jeraha la goti. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)
Kiungo wa kati wa Senegal Cheikhou Kouyate, 34, ni mmoja wachezaji wasio ikata Leeds United wanafikiria kusaini. (Yorkshire Evening Oost)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi