Kwa nini akina mama wa sasa huhangaika 'kurudisha miili' baada ya kujifungua

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kupata mtoto, kinamama wanakabiliwa na shinikizo la kurudi kwenye miili yao waliokuwanayo kabla ya kupata mtoto.
Ina athari wakati mwingine hatari.
Mara tu Sharon Oakley alipojifungua mnamo 2017, marafiki walimpongeza, "Oh, unaonekana mzuri sana !" anasema watu walimwambia ndani ya miezi kadhaa baada ya kupata mtoto wake.
Huenda alionekana kama 'amerejea kwenye mwili wake wa zamani'. Lakini ukweli ulikuwa tofauti.
Ingawa alikuwa amepunguza uzito mwingi ambao alikuwa nao wakati wa ujauzito, kimwili, alikuwa akiteseka.
Mwanariadha mahiri, Oakley, raia wa Canada anayeishi Yorkshire, Uingereza, alipenda kukimbia pamoja na mwanawe kwenye kigari cha miguu, utaratibu ambao alichukua miezi sita baada ya kujifungua.
Lakini alikuwa akitokwa mkojo njia nzima. Kurudi kazini, alianza kupitia shida hiyo ofisini pia.
Baada ya safari ngumu ya uchunguzi iliyojumuisha kusubiri kwa miezi sita kwa rufaa ya mtaalamu wa viungo, Oakley aligunduliwa kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo kitaalamu rectocele na uterine prolapses yaani misuli ya sakafu ya nyonga na mishipa inapodhoofika.
Miaka minne baadaye, hali yake imekuwa nzuri. Lakini bado anavuja mkojo mara kwa mara. Hutembea akiwa na sodo kila mahali, huwa ana hofu anapokimbia Kwa muda, alifikiri kwamba angelazimika kuacha kazi yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Ni sehemu ya ajabu sana ya utamaduni wetu ambapo tunapima kipindi cha baada ya kujifungua kwa mwanamke kulingana na jinsi anavyoonekana, badala ya jinsi anavyohisi," anasema Oakley. "Naonekana sawa - lakini nina majeraha haya ambayo bado ninayapitia kila siku."
Hadithi kama za Oakley ni za kawaida zaidi kuliko zinazozungumzwa hadharani.
Ingawa si mara zote, prolapse ya kiungo cha fupanyonga pekee huathiri hadi 90% ya wanawake baada ya kujifungua.
Ukosefu wa haja ndogo, ambao unaweza pia kusababishwa na sakafu ya nyonga yenye kubana sana, tishu zenye kovu au uharibifu wa neva, hupatikana kwa karibu theluthi moja.
Diastasis recti, ambapo misuli ya tumbo inayojitenga ili kutoa nafasi kwa tumbo linalokua bado haijaunganishwa pamoja - kitu ambacho kinaweza kufanya tumbo kuonekana kama linavimba na kusababisha maumivu, kuvimbiwa na kuvuja kwa mkojo, na pia kufanya kutembea au kuinua kitu . kuwa vigumu - huathiri 60%.
Na hata kwa kukosekana kwa ujauzito au majeraha ya kuzaliwa, mabadiliko makubwa ya kisaikolojia yanayotokea wakati wa ujauzito, leba na baada ya kuzaa - kutoka kwa homoni zinazouambia mwili kushikilia mafuta, shinikizo kwenye sakafu ya nyoga, hadi virutubishi vinavyochujwa nje ya mlo wa mama kulisha kijusi au mtoto anayenyonyesha - inamaanisha kwamba inachukua muda kupona.
Lakini wanawake wengi huona kwamba, mara mtoto anapozaliwa, ujumbe anaopata si wa kupumzika na kupona. Ni 'kujirudisha katika hali ya zamani' katika miili na tabia waliyokuwa nayo kabla ya kupata ujauzito.
Mabadiliko yasiyoepukika
Kuwa mama kunamaanisha zaidi ya kuingia katika hatua mpya ya maisha.
Ni mabadiliko ya maisha ya mtu, mawazo, hata utambulisho.
Kwa wanawake wengi, kuna uwezekano kuwa ni mara ya kwanza wao kuwajibika kikamilifu kwa mtoto mchanga, aliye katika mazingira magumu - ambaye anawahitaji karibu kila mara.
Pia inaweza kuwa mara ya kwanza hawajafanya kazi au wanategemea mshirika kifedha. Hasa katika nchi ambazo hazina likizo ya kutosha ya wazazi au sera za usaidizi wa malezi ya watoto, huenda zinakabiliwa na matatizo ya kifedha.
Na wakati, au kama, wanarudi kwenye taaluma zao, akina mama mara nyingi huhisi shinikizo la kutoa picha ambayo uzazi haujawabadilisha - mara nyingi ili kuepuka 'adhabu ya uzazi', ambapo wanawake huona mishahara yao na matarajio ya kazi yakitatizika.
Ingawa inajulikana kuwa kuwa mzazi hakuathiri tu vipaumbele vya watu, bali hubadilisha ubongo. Yote haya yanatokea, bila shaka, wakati ambapo wanawake wengi wamechoka zaidi kuliko vile walivyowahi kuwa.
Na zaidi ya robo wanakabiliwa na changamoto za afya ya akili kama vile unyogovu baada ya kuzaa au PTSD. Bado mafadhaiko haya yote yaliyopo kila mahali, akina mama wanashindana na shinikizo la 'kurudisha maumbo yao ya awali'. Tamaduni nyingi, hasa katika nchi za Magharibi, zinaweka shinikizo kubwa kwa wanawake kubadili miili yao baada ya kuzaa tena kwa haraka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwanza, bila shaka, kuna kupata uzito. "Unapokuwa mjamzito, una ziada ya homoni hizi zote zinazotuambia kushikilia uzito huu kwa sababu tunauhitaji," anasema Jenna Perkins, muuguzi wa afya ya wanawake na mtaalam wa magonjwa ya nyonga anayefanya mazoezi huko Washington DC. "Tunahitaji hifadhi hizi za mafuta karibu na tumbo ili kulinda uterasi yetu nyeti na mtoto anayekua ndani."
Wakati huo huo, misuli katika tumbo na sakafu ya nyonga imeinuliwa kwa karatasi-nyembamba. Kubeba kiumbe, na mkazo wa kuzaa kwa uke, huongeza uzito na shinikizo kwenye sakafu ya nyonga.
Hata mifupa husogea: wakati wa ujauzito, nyonga inainama na inakuwa, kwa wastani, karibu upana wa 2.5cm.
Mabadiliko haya yote na matokeo yanayoweza kutokea, wanasema wataalam, inamaanisha kuwa wazo kwamba wanawake wanaweza kurudi kisaikolojia kwa mwili wao wa kabla ya ujauzito ndani ya wiki baada ya kujifungua sio sahihi hata kidogo, hatari zaidi.
Huko Indiana, Marekani, Shelby Alley anasema alianza kukumbana na shinikizo la kiutamaduni la kurejea kwenye umbo lake la awali kabla hata ya kujifungua mwaka wa 2022.
"Mwajiri wangu wakati huo, hata kabla sijapata mtoto wangu, alikuwa ananiuliza, 'Je, unafurahia kupata mtoto wako? unafikiria kurejesha mwili wako?' Na hilo lilikuwa wazo la ajabu sana kwangu, kwa sababu mimi nilikuwa na kiumbe tumboni. Mwili wangu ni wangu zaidi kuliko hapo awali. Lakini ndipo nilipohisi shinikizo hilo kwa mara ya kwanza, "anasema.
Alifikiria maana ya ujumbe ule- na akabadilisha jinsi alivyoutendea mwili wake kama matokeo. "Mara mtoto wangu alipokuwa hapa, ilikuwa kama," Sawa, sihitaji kuendelea kulisha mwili wangu kwa sababu sina kiumbe tumboni. Ninaweza kuanza kupunguza mlo wangu," anasema. Lakini alipoanza kupunguza kalori, jambo la kwanza aliloona ni kwamba unyonyeshaji wake ulipungua.
"Nilitoka kwenye kupata maziwa mengi na kufikia hatua ya kukamua maziwa kidogo, kumpatia mtoto maziwa ya kutosha ilikuwa shida. Alikuwa akimnyonyesha kila saa; hakuonekana kushiba," anasema.
Alianza kukosa usingizi kutokana na maisha na mtoto mchanga, alihisi uchovu zaidi. Hamu yake ya ulezi ilibadilika.
Alley hajizuii tena kula chakula, lakini bado anahisi ana "hatia" wakati mwingine kwa sababu ya kutofanikiwa kupungua uzito wote kutokana na ujauzito wake. "Ilikuwa ngumu kupatanisha kile ulimwengu unataka uwe, dhidi ya kile asili inahitaji wewe kuwa," anasema.
Mkazo wa kupoteza uzito baada ya kujifungua unatokana na mambo kadhaa. Lakini moyoni mwake, utamaduni wa kurudisha mwili unatokana na mawazo yetu ya uzazi wa kisasa kwa ujumla, asema Sophie Brock, mwanasosholojia wa masomo ya akina mama huko Sydney, Australia na mtangazaji wa podikasti The Good Enough Mother.
"Akina mama wako chini ya sheria fulani za kijamii na matarajio kwa njia "Shinikizo la kitamaduni. 'Kurejesha mwili' ni mfano wa hilo.
Akina mama wanatarajiwa kuwa na uwezo wa kufuta ushahidi wowote wa kuwahi kupata watoto, huku wakijaribu kutimiza shinikizo na mahitaji yanayoshindana. nini maana ya kuwa mama/mke/mfanyakazi kamili.” Lakini, anaongeza, "haiwezekani - tunaombwa kutimiza maadili yanayoshindana na kamwe hatuwezi kufanya vya 'kutosha'".















