Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 23.02.2024
Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 30 na beki wa kati wa Uingereza Harry Maguire, 30, ni miongoni mwa wachezaji 11 ambao wanaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kitakachofungishwa virago msimu huu. (ESPN)
Mwekezaji wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe, ambaye ameweka kipaumbele katika kuhakikisha soka la Ligi ya Mabingwa Ulaya ni jambo la kwanza, anataka kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua kuhusu mustakabali wa meneja Erik ten Hag. (Star)
Kazi ya meneja wa Manchester United inamvutia Thomas Tuchel, ambaye ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu. (Sky Germany)
Liverpool walikataa mpango wa Chelsea kumnunua mshambuliaji wao wa Uruguay Darwin Nunez, 24, msimu uliopita wa joto. (Times – Subscription Required)
Arsenal wamedhamiria kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji na Everton Amadou Onana, 22, msimu huu. (TeamTalks)
Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim anapigiwa upatu kuinoa Liverpool iwapo watakosa kumleta kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp msimu ujao. (Independent)
Mlinzi wa Tottenham na England Eric Dier, 30, huenda akasalia Bayern Munich zaidi ya msimu wa joto huku timu hiyo ya Ujerumani ikiwa na wasiwasi juu ya kiwango chake cha mchezo. (PPicture via Mail)
Manchester City wanakaribia kumfunga mshambuliaji wa Norway Oscar Bobb, 20, kwa kandarasi mpya ya muda mrefu. (Mail)
Tottenham haitarajii kiungo wa kati Pierre-Emile Hojbjerg, 28, kusalia katika klabu hiyo msimu huu huku timu kadhaa za Serie A zikiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark. (Football Insider)
Arsenal wanakaribia kumnasa nyota wa Rangers Alexander Smith mwenye umri wa miaka 15, huku kiungo huyo mkabaji mzaliwa wa Scotland akiwa na uraia wa nchi mbili, akiwa ameiwakilisha Marekani chini ya umri wa miaka 15 na timu ya U16 ya Scotland. (Sun)
Juventus wanamtaka mlinda lango wa Monza Michele di Gregorio na wanamwona Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 27 kama anayewezekana kuchukua nafasi ya nambari moja kwa sasa, Wojciech Szczesny, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland akiwa na umri wa miaka 33. (La Gazzetta dello Sport – In Itali)
Brighton na Celtic ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtazama mshambuliaji wa Charlton Athletic raia wa Ireland, Patrick Casey, mwenye umri wa miaka 18. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 30, anasema alikuwa na ofa ya kuhamia Saudi Arabia lakini anataka kusalia na Inter Milan. (DAZN, kupitia Gazzetta dello Sport)