Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Juventus yamtaka nyota wa Man City Bernardo Silva
Juventus watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 31, kwa uhamisho wa bila malipo wakati mkataba wake wa Manchester City utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Tuttosport - In Itali)
Manchester City wanafikiria kumnunua mchezaji wa Manchester United Kobbie Mainoo, ingawa wana uwezekano wa kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle na Chelsea kumnunua kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 20. (TeamTalks)
Chelsea bado wanavutiwa na Morgan Rogers licha ya kukasirishwa na hesabu ya Aston Villa ya pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 23, msimu wa joto. (The Sun)
Kipengele katika mkataba wa Ruben Amorim kinamaanisha kwamba angepokea malipo ya pauni milioni 12 iwapo Manchester United itamfukuza kazi kabla ya kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kuteuliwa kwake tarehe 1 Novemba. (Mail - Subscription Required)
Matokeo ya hivi majuzi ya kifedha ya Manchester United yamewapa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Brighton na Cameroon Carlos Baleba, 21. (Mirror),
Mkopo wa Crystal Palace kwa Christantus Uche kutoka Getafe utakuwa mkataba wa kudumu moja kwa moja ikiwa mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 ataanza mechi 10 msimu huu. (Marca in Spanish)
Liverpool wako tayari kutoa euro 50m (£43.35m) kwa mlinzi wa Barcelona Ronald Araujo, 26, ingawa Tottenham pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay. (Fichajes - in Spanish)
Birmingham wana nia ya kumfunga kipa Alfie Smith mwenye umri wa miaka 14 wa England chini ya umri wa miaka 15 kwenye mkataba mpya ili kuzuia nia ya Chelsea, Manchester United, Arsenal, Liverpool na Manchester City. (Mail)
Chelsea ndio klabu ya hivi punde zaidi kueleza nia ya kutaka kumsajili beki wa kati wa England mwenye umri wa miaka 25 Marc Guehi mkataba wake wa Crystal Palace utakapokamilika msimu ujao. (Football Insider)