Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Putin na bosi wa Wagner Prigozhin: Urafiki wa muda mrefu uliovunjika ghafla
Uhusiano wao ulikuwa kutoka kwa ulimwengu wa giza ambapo huduma za usalama za serikali ya Urusi zilijihusisha na ulimwengu wa wahalifu.
Wakati kampuni ya kijeshi ya Yevgeny Prigozhin's Wagner ilikua na kuwa moja ya miundo yenye ushawishi mkubwa nchini Urusi, Vladimir Putin alizidi kutegemea mafanikio yake ya uwanja wa vita huko Ukraine.
Lakini wawili hao walikutana mapema miaka ya 1990 huko St Petersburg kwa mara ya kwanza, baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti.
Wote wawili wanatoka mji wa pili wa Urusi na mji mkuu wa kitamaduni.
Nyumbani kwa jumba la makumbusho la sanaa la Hermitage na Imperial Winter Palace, unachukuliwa kuwa mji mkuu wa uhalifu wa Urusi na msingi wa magenge yenye nguvu.
Mazingira halisi ya kukutana kwao mara ya kwanza hayajulikani, lakini Prigozhin alikuwa ametoka jela na Bw Putin alikuwa amerejea hivi majuzi kutoka misheni huko Ujerumani Mashariki kama afisa wa idara ya usalama ya Soviet, KGB, na alikuwa akitafuta njia ya kuingia katika siasa.
Akihukumiwa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17, Prigozhin hakuwa mgeni kenye uhalifu. Baada ya hukumu iliyosimamishwa ya wizi mwishoni mwa miaka ya 1970, alipewa kifungo cha muda mrefu jela kwa wizi wamabavu mnamo 1981.
Yeye na wengine wawili walikuwa wamemshika mwanamke shingoni barabarani na kujaribu kumnyonga, kabla ya kukimbia na buti na vipuli vyake wakati wa msimu wa baridi.
Alipotoka gerezani mnamo 1990, Urusi ilikuwa mahali tofauti sana. Badala ya kiongozi wa zamani wa Sovieti, Leonid Brezhnev, kiongozi wa mageuzi Mikhail Gorbachev alikuwa madarakani, Ukuta wa Berlin ulikuwa umeanguka na perestroika (urekebishaji upya) ulikuwa ukiendelea.
Prigozhin alianza kama muuzaji wa chakula aina ya hot dog huko St Petersburg, lakini kufikia katikati ya miaka ya 1990 alikuwa amefungua mgahawa. Jumba la Kitamaduni la Zamani ndio mahali ambapo wanaume hao wawili walikutana kwa mara ya kwanza.
Menyu ya foie gras na oysters iliwavutia wakuu wa uhalifu wa eneo hilo pamoja na meya mwenye uwezo mkubwa wa jiji hilo, Anatoly Sobchak. Vladimir Putin, wakati huo akiwa na umri wa miaka 40, alienda huko pia kama naibu wa Sobchak.
Mgahawa mmoja wa Prigozhin ukawa mkubwa na wateja wake walijumuisha wanasiasa kutoka mbali zaidi ya St Petersburg.
Kufikia mwanzoni mwa karne, wakati Bw Putin alipokuwa rais, watu hao wawili walikuwa wameshirikiana sana na jina la utani la Prigozhin, mpishi wa Putin, lilianza wakati huu.
Picha inaonyesha Prigozhin akiwahudumia chakula cha jioni yeye na Rais George W Bush.
Kwa mtu kama kiongozi mpya wa Urusi, ilikuwa ni lazima kuwa na mpishi wa kibinafsi ili kuhakikisha chakula chake kilikuwa salama kwa matumizi.
Akiwa na akili ya kutiliwa shaka ya KGB, pia aliwahi kuwa mkuu wa mrithi wake, FSB.
Pia ilikuwa rahisi kuwa na mtu ambaye angejua siri zake za ndani na ambaye angeweza kumshawishi.
Vladimir Putin akiwa Kremlin, huduma za usalama za Urusi polepole zilianza kuchukua udhabiti. Prigozhin alichukua majukumu mbalimbali ya Kremlin, hasa yale yaliyo nje ya uwezo wa huduma za usalama.
Uhusiano wao ulikuwa una kikomo, kwa hivyo Putin angeweza kukana kuhusika.
Prigozhin alianzisha himaya ya vyombo vya habari iliyolenga kueneza habari potofu ndani ya Urusi na nje ya nchi. Hadithi ilizobuni mara nyingi zilikuwa za kustaajabisha sana hivi kwamba hakuna chombo cha propaganda cha serikali ambacho kingethubutu kuzieneza.
Mitandao ya kijamii ilipoanza kupata ushawishi, alianzisha "kiwanda" ambacho athari yake kuu ilikuwa kuwaacha Warusi na hisia kwamba hakuna ukweli na hakuna maana ya kuutafuta.
Ilichukua muongo mwingine kabla ya kukubali kuwa mmiliki wa "Shirika la Utafiti wa Mtandao".
Baada ya Mapinduzi ya Ukraine 2013-14 na Urusi kuinyakua Crimea, ripoti za kwanza za kampuni ya kijeshi ya kibinafsi ya Wagner ziliibuka.
Wagner iliunga mkono wafuasi wa kujitenga wanaounga mkono Urusi huko Crimea na mashariki mwa Ukraine.
Mashirika ya mamluki yamepigwa marufuku na sheria za Urusi, ingawa Prigozhin na mamluki wake walikuwa wamezidi kuwa muhimu kwa kuimarisha mamlaka ya Rais Putin.
Kwa hivyo hadi mwishoni mwa msimu wa joto wa 2022, Kremlin ilisisitiza kuwa haina uhusiano naye.
Wagner pia ilichukua jukumu kubwa nchini Syria - na huu ndio wakati kamanda wake mkatili, Dmitry Utkin, alipoonekana kwa mara ya kwanza kama mshirika wa karibu wa Prigozhin.
Kundi la mamluki limekuwa likifanya kazi kwa miaka mingi katika nchi kadhaa za Afrika, kutoka Libya na Mali hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Lakini rasmi, Prigozhin hakuwa na uhusiano maalum na rais.
Bw Putin au katibu wake wa vyombo vya habari Dmitry Peskov angesema tu kwamba walikuwa na ufahamu wa kuwepo kwa "mfanyabiashara binafsi" wa Kirusi ambaye alihusika katika shughuli hizo. Lakini ilikuwa wazi shughuli kama hizo hazingeweza kufanywa bila idhini ya Kremlin.
Rais Putin alikiri tu mwezi Juni kwamba Wagner aiikuwa imepokea ufadhili mkubwa wa serikali kwa miaka mingi na kwamba mamluki wake walipigana vita kwa ushujaa. Na kwa sababu makampuni ya kijeshi ya kibinafsi yalikuwa haramu alisema kuwa kama kikundi, hayakuwepo.
Haikuwa hadi majira ya joto ya 2022 ambapo ripoti ziliibuka kuhusu mapigano ya Wagner nchini Ukraine.
Katika muda wa majuma machache, Prigozhin alikuwa akitembelea magereza ya Urusi, akiwaandikisha wafungwa kwa ajili ya vita.
Msemaji wa Kremlin alizungumzai juu yake kama mtu "ambaye moyo wake unauma kwa kile kinachotokea" na ambaye alikuwa "akitoa mchango mkubwa".
Prigozhin alifungua Kituo cha Wagner huko St Petersburg mnamo Novemba na ukosoaji wake kwa jeshi la Urusi na wizara ya ulinzi ulizidi kuongezeka.
Wakati vikosi vya Urusi vilipolazimika kurudi nyuma nchini Ukraine, ukosoaji wake ulifikia kilele.
Alilalamika kwamba kamandi ya jeshi ilikuwa ikikataa kutambua mchango wa mamluki katika juhudi za vita.
Baadaye, alimshutumu waziwazi Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Majenerali, Valery Gerasimov, kwa kutowapatia Wagner risasi wakati kundi hilo lilikuwa likipoteza maelfu ya wapiganaji wake katika vita vya Bakhmut mashariki mwa Ukraine.
Wakati mmoja, Prigozhin hata alilenga ukosoaji wake kwa rais, akitumia neno la Kirusi la babu kumtaja .
"Tunawezaje kushinda vita wakati Babu ni mjinga?"
Hakumtaja Putin, lakini Warusi waliachwa bila shaka kwamba alikuwa akimhusisha moja kwa moja.
Kremlin haikutoa tamko lake juu ya uhasama uliokua, lakini ilikuwa tamko ambalo lingetikisa uongozi wa Urusi kwa msingi wake na hatimaye kumwangusha Prigozhin.
Alikataa ombi la wizara ya ulinzi kuweka vikundi vyote vya mamluki chini ya udhibiti wake. Hali ilipozidi kuchemka, alithubutu kuhoji malengo hasa ya vita.
Mnamo Juni 23, alitangaza "maandamano ya haki" kuelekea Moscow.
Vyanzo vya habari vimeiambia BBC kwamba uasi wake ulikuwa ishara ya kukata tamaa kwa Prigozhin na jaribio la kuvutia hisia za Rais Putin kwenye mzozo wake na jeshi la Urusi.
"Alikuwa na wasiwasi juu ya kupoteza uhuru wake," chanzo kimoja kilichomjua Prigozhin kilieleza.
Mamluki wa Wagner walidungua helikopta mbili za kijeshi na ndege na kuwaua hadi wanajeshi 15 wa Urusi.
Bila kumtaja yeye binafsi, Rais Putin alimtaja Prigozhin kama msaliti ambaye "aliidungu Urusi kisu kutoka nyuma ".
Uasi huu ulikuwa ndio mpasuko wa mwisho kati yao.
Siku chache baada ya uasi huo kumalizika bila mafanikio, Vladimir Putin alikutana na mshirika wake wa zamani huko Kremlin kwa saa tatu, pamoja na makamanda zaidi ya 30 wa Wagner.
Vladimir Putin hakuwa na haja naye tena, lakini bado kulikuwa na maswali juu ya hatima ya wanajeshi wake.
Prigozhin aliamini wazi mustakabali wake ulikuwa barani Afrika na inasemekana video yake ya mwisho mtandaoni ilirekodiwa katika uwanja mmoja Afrika ambapo alidai: "Sisi hapa, tunaweka hofu ya Mungu kwa Isis, al-Qaeda na majambazi wengine."
Lakini hadithi yake inaonekana kumalizika hivi karibuni, kufuatia msururu sawa na mifano mingine katika historia ya Urusi.
Mtu aliyekabidhiwa jukumu la kutekeleza sera za kikatili za Kremlin mwenyewe aliadhibiwa kikatili na hatimaye kuuawa.
Au katika tathmini ya Vladimir Putin mwenyewe: "Alikuwa mtu mwenye hatima ngumu na alifanya makosa makubwa katika maisha."