Kombe la Dunia 2022: Maswali sita yanayokabili timu za Afrika nchini Qatar

Achraf Hakimi na Edouard Mendy
Maelezo ya picha, Beki wa Morocco, Achraf Hakimi na kipa wa Senegal, Edouard Mendy ni miongoni mwa nyota wa soka barani Afrika wanaosaka ubingwa wa Kombe la Dunia.
Iliyochapishwa

Timu za Afrika zitapanda daraja mpya kwenye Kombe la Dunia mwaka huu huku nchi zote tano zilizofuzu kutoka bara hilo zikitua Qatar chini ya ukufunzi wa makocha wa nyumbani.

Wanne kati ya hao wanachukua usukani kwa mara ya kwanza katika fainali hizo, huku Msenegal Aliou Cisse pekee akiwa dimbani nchini Urusi miaka minne iliyopita.

Timu zote tano za Afrika zilitolewa katika hatua ya makundi mwaka wa 2018, hivyo kabarua kikubwa itakuwa kuondoa kikwazo hicho kabla ya hata kufikiria kuadikisha historia nchini Qatar kwa kufuzu hatua ya nane bora.

BBC Michezo Afrika inaangazia maswala makuu yanayozikabili timu hizo katika michuano ya Kombe la Dunia la kwanza kuandaliwa Mashariki ya Kati.

Je, kuna pande yoyote inaweza kufuzu robo fainali?

Timu za Afrika zilizofuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia zina hoja ya kuthibitisha kwani, kwa mara ya kwanza tangu 1982, hakuna timu kutoka bara hilo iliyofikia hatua ya mtoano mwaka wa 2018 - wakati Morocco, Senegal na Tunisia, ambazo zimefuzu tena, ziliwakilisha Afrika pamoja na Misri na Nigeria.

Cameroon na Ghana zinarejea ulingoni mwaka huu baada ya kustahimili kichapo cha Kombe la Dunia la 2014.

Baada ya kushinda Kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika mwezi Februari, matumaini makubwa ya Senegal yamelemazwa kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa mshindi wa pili wa Ballon d'Or Sadio Mane, ambaye penalti zake zilichangia nchi hiyo kushinda taji la bara na kufuzu Kombe la Dunia.

Licha ya kuwa na kocha ambaye alichukua nafasi hiyo miezi miwili tu iliyopita, Morocco inaweza kufanya maisha kuwa magumu katika Kundi F kuliko Ubelgiji, huku kikosi chao maarufu kikizidi kuzeeka, washindi wa pili wa 2018 Croatia na Canada huenda wanaazimia kuzingatia hilo kwa maslahi yao.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Cameroon walicheza kwa kasi na nguvu kubwa nyakati fulani walipokuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu lakini utabiri wa mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo aliyegeuka rais wa shirikisho, Samuel Eto'o kwamba Indomitable Lions, inayoongozwa na Rigobert Song na iliyofanya vibaya katika mechi za kirafiki za hivi majuzi, itaifunga Morocco katika hatua ya mwisho ya michuano hiyo.

Timu tatu pekee za Afrika zimefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia - kati ya ziara 49 - hakuna iliyokaribia kusonga mbele zaidi ya Ghana, ambayo kukosa penalti ya dakika za mwisho katika muda wa nyongeza dhidi ya Uruguay mwaka 2010 kutakuwa kila wakati akilini mwa timu hizo mbili zitakapokutana tena katika Kundi H.

Lengo la Senegal bado ni kuting nusu-fainali ya kwanza, lakini jeraha la Mane linaweza kuathiri azma hiyo kutokana na umuhimu wake kwa Simba hao wa Teranga, timu iliyoorodheshwa kuwa bora  zaidi barani Afrika tangu Novemba 2018.

Je, kocha Cisse wa Senegal atajaza vipi nafasi ya Mane?

Kocha Aliou Cisse aliiongoza Senegal kunyakua taji lao la kwanza la wakubwa la bara nchini Cameroon mnamo Februari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha Aliou Cisse aliiongoza Senegal kunyakua taji lao la kwanza barani Afrika nchini Cameroon mwezi Februari.

Cisse alikuwa sehemu ya kizazi cha wachezaji waSenegal ambacho kilifika hatua ya nane bora nchini Japan na Korea Kusini mwaka 2002 na, baada ya kuchukua uongozi miaka saba iliyopita, atakuwa akitumia uzoefu wake wote kuja na mpango mpya wa mchezo kwa muda mfupi.

Wenyeji hao wa Afrika Magharibi watamenyana na Uholanzi katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi A siku ya Jumatatu.

Nani atakuwa nyota wa Afrika badala ya Mane?

Hakim Ziyech

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hakim Ziyech amefunga mabao 18 katika mechi 43 alizoichezea Morocco, baada ya kuachana na soka ya kimataifa mwezi Septemba.

Kukosekana kwa Mohammed Salah na Riyad Mahrez baada ya Misri na Algeria kushindwa kufuzu, kuna nafasi ya nyota wengine kuibuka katika michuano ya Kombe hilo la Dunia.

Kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus anapigiwa upatu kushikilia nafasi hiyo iwapo ataendelea na kiwango chake cha kusisimua cha Ligi ya Mabingwa akiwa na Ajax.

Nayo Cameroon inajivunia washambuliaji mahiri Eric Maxim Choupo-Moting, Karl Toko Ekambi na Vincent Aboubakar, ambao waling’ara katika mechi saba kati ya nane za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Wakati Watunisia wakiwa na matumaini kuwa kiungo Aissa Laidouni anaweza kuendelea kuonesha kiwango kizuri, Hakim Ziyech atalenga kutimiza ndoto  yake baada ya sakata ya muda mrefu ya kuachwa nje ya kikosi cha Morocco.

Ugomvi kati yake na kocha wa zamani Vahid Halilhodzic ulishuhudia winga huyo wa Chelsea akiondolewa na kuachwa kwenye kikosi cha Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 - ambaye aliachana na soka ya kimataifa mwezi Februari - alikirudi ugani mara baada ya Mbosnia huyo kutimuliwa miezi mitatu iliyopita.

Je hali ya hewa itanufaisha timu za Afrika?

Muda wa kuanza kwa Kombe hili la Dunia ulibadilishwa kutoka wakati wake wa jadi ambao huwa Juni na Julai ili kuepusha joto la katikati ya mwaka nchini Qatar.

Hali ya hewa inaweza kuwa na athari kwa timu za Ulaya, ambapo Novemba na Desemba kwa kawaida hushuhudia halijoto ya nyuzi  27-30 na unyevunyevu unaoifanya kuhisi zaidi kama nyuzi joto 30 hadi 35, ingawa wenyeji wanaelezea hali ya hewa ya joto isiyo ya kawaida nchini Qatar kwa sasa.

Kiwango cha joto  hupungua nyakati za jioni na viwanja vilivyojengwa kwa ajili ya mashindano vimeundwa ili kuongeza kivuli, huku hali ya hewa pia ikitarajiwa kupunguza joto la uwanjani hadi nyuzi joto 21 zinazoweza kudhibitiwa zaidi.

Je wenyeji wataunga mkono timu mbili za Afrika Kaskazini?

Mashabiki wa Tunisia wanaweza kuwa na ndoto ya kupata taji la Kombe la Dunia - lakini Carthage Eagles hawajawahi kufika hatua ya mtoano katika mechi tano zilizopita kwenye fainali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Tunisia wanaweza kuwa na ndoto ya kupata taji la Kombe la Dunia - lakini hawajawahi kufika hatua ya mtoano katika mechi tano zilizopita kwenye fainali.

Qatar iliandaa Kombe la Mataifa ya  Kiarabu mwezi Desemba mwaka jana ili kutumia michuano hiyo kama tukio la majaribio kwa Kombe la Dunia, Tunisia ilipoteza mechi yake dhidi ys Algeria katika fainali.

Carthage Eagles walinufaika na mashabiki wao wengi nchini Qatar wakati wa mechi zao, na wanatarajiwa kunufaika na mazingira kama ya nyumbani watakaporejea katika mechi za Kundi D dhidi ya Denmark, Australia na mabingwa watetezi Ufaransa.

Timu hizo mbili za Afrika Kaskazini zinategemea usaidizi wa mashabiki wa Qatar wanapolenga kufikia hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika jaribio la sita.

"Nadhani kucheza Qatar kutatusaidia sisi, nchi za Afrika na hasa nchi za Kiarabu," nahodha wa Tunisia Wahbi Khazri aliambia BBC Michezo Afrika.

"Tunaenda kucheza kwenye bara tulilozoea, kuna jamii kubwa ya Watunisia nchini Qatar. Walionyesha uwepo wao kwenye Kombe la Mataifa ya Kiarabu ambapo viwanja vilijaa mashabiki wa Tunisia, na bila shaka wakijitokeza tena hatua hiyo inaweza kutusaidia kufanya vizuri sana."

Morocco pia, wanatarajia kunufaika na mazingira kama hayo ya Tunisiaikizingatiwa kwamba tamaduni zao ni sawa na wenyeji.

Je, ni wakati wa kocha wa Kiafrika kung'ara?

Otto Addo (Ghana), Rigobert Song (Cameroon), Walid Regragui (Morocco) na Jalel Kadri (Tunisia)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Otto Addo (Ghana), Rigobert Song (Cameroon), Walid Regragui (Morocco) na Jalel Kadri (Tunisia) wote watakuwa wakishiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kama wakufunzi.

Kwa mara ya kwanza tangu Afrika iwakilishwe na zaidi ya timu moja kwenye fainali hizo zilizofanyika miaka 40 iliyopita nchini Uhispania, wawakilishi wake wote wa Kombe la Dunia wanaongozwa na makocha wazawa.

Kwa sasa kocha mwenye uzoefu mkubwa zaidi ni Cisse wa Senegal, ambaye alichukua usukani mwaka 2015, kwani wanne waliosalia waliteuliwa mwaka huu.

Kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya mataiufa ya Africa AFCON iliyoandaliwa na Cameroon mapema mwaka huu, aliyekuwa mkufunzi a timu ya taifa ya Cameroon Toni Conceicao alifutwa kazi na badala yake Song akapatiwa usimamizi wa timu hiyo . Song anapendelea mbinu ya 4-2-2 uwanjani.

Nana Otto Addo ni meneja wa soka wa Ghana na mchezaji wa zamani aliyezaliwa nchini Ujerumani. Kwa sasa ni meneja wa timu ya taifa ya kandanda ya Ghana, na anafanya kazi kama mkufunzi wa vipaji katika klabu ya Borussia Dortmund.

Jalel Kadri ni kocha wa kandanda wa Tunisia ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya kandanda ya Tunisia.

Na Walid Regragui ni meneja wa kandanda wa Morocco na mchezaji wa kulipwa aliyestaafu ambaye alicheza kama mlinzi. Ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya kandanda ya Morocco.