Kwa nini baadhi ya wachezaji chipukizi hupatwa na mshtuko wa moyo?

Damar

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Nyota wa kandanda wa Marekani Damar Hamlin ndiye mchezaji wa hivi punde zaidi kupata matatizo ya moyo wakati akiwa uwanjani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alianguka chini baada ya kugongana na mpinzani wakati wa mchezo wa awali.

Madaktari walithibitisha kuwa alikuwa amepatwa na mshtuko wa moyo - kumaanisha moyo wake ulikuwa umeacha kupiga vizuri na haukuweza kufanya kazi yake ya kusukuma damu kuzunguka mwili.

Ufufuo wa haraka ulihitajika uwanjani ili kuokoa maisha yake. Sasa yuko katika hali mbaya hospitalini. Madaktari wanaomtibu bado hawajaeleza sababu hasa ya msingi.

Uwezekano mwingine ni kiwewe kisicho cha kawaida, kuchochea kitu kinachoitwa commotio cordis.

Katika hali hii adimu, kupigwa moja kwa moja kwa kifua kunaweza kusababisha mshtuko wa moyo kwa kufanya moyo kwenda katika mdundo usio wa kawaida, unaotishia maisha.

Ni tofauti na mshtuko wa moyo, ambayo hutokea wakati usambazaji wa damu kwenye misuli ya moyo umekatwa.

Uwezekano mwingine wa kiwewe kisicho wazi ni uharibifu mkubwa wa kimuundo wa moyo kutokana na nguvu ya pigo.

Bado haijajulikana ni majeraha gani ya ndani ambayo Hamlin huenda alipata kutokana na tukio hilo na ikiwa kumekuwa na madhara makubwa kwenye moyo wake.

Hali nyingine inayoweza kuwa mbaya ya moyo inayoathiri baadhi ya wanariadha wachanga ni ugonjwa wa kijeni unaojulikana kama hypertrophic cardiomyopathy.

Maelezo ya video, Mambo muhimu kuhusu maradhi ya mshtuko wa moyo
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Watu walio na hali hii wanaweza kuonekana kuwa sawa kwa sababu hawaonyeshi dalili zinazoashiria wanakabiliwa na tatizo kubwa kama hilo.

Ni hali ambayo misuli ya moyo inakuwa imeongezeka au "hypertrophied".

Misuli ya moyo iliyoimarishwa inaweza kufanya iwe vigumu kwa moyo kusukuma damu.

Na kunaweza kuwa na matatizo yanayotishia maisha ya mdundo wa moyo pia.

Wanaharakati wa kupinga chanjo mtandaoni walikimbilia habari ya kuanguka kwa Hamlin na kulaumu chanjo za Covid bila ushahidi.

Akaunti moja inayotangaza filamu ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona iliyojaa madai ya kutiliwa shaka na yaliyokanushwa ilituma ujumbe kwenye Twitter kwamba kabla ya 2021, "wanariadha kuzimia uwanjani HAIKUWA tukio la kawaida. Hili linakuwa muundo usiopingika (na unaotia wasiwasi sana)"

Wanaharakati wa kupinga chanjo wamekusanya ripoti kadhaa zavisa vya vifo vya wanariadha ili kuimarisha madai yao.

Hata hivyo, kulingana na utafiti wa 2016, kuna takriban vifo 100 hadi 150 vya ghafla vinavyohusishwa na mshtuko wa moyo kila mwaka wakati wakati wa mashindano nchi Marekani pekee.

Hali ya chanjo ya Hamlin haijulikani. Mnamo Machi 2022, NFL ilisema kuwa karibu 95% ya wachezaji wa NFL walichanjwa dhidi ya Covid.

Sio mwanamichezo pekee aliyeanguka na kuzimia katika mchezo mkubwa.

Mwanasoka wa Denmark Christian Eriksen alipatwa na mshtuko wa moyo mwaka jana kwenye mechi ya Euro 2020 na alikaribia kufa uwanjani.

Madaktari walitumia kizuia moyo kushtua moyo wake na kuufanya ufanye kazi tena.

Tangu wakati huo amekuwa na kifaa kidogo, kinachoitwa ICD, kilichowekewa ili kuweka moyo wake sawa.

Eriksen amesema hakukuwa na historia ya ugonjwa wa moyo katika familia yake na, kama wanasoka wengine wa daraja la juu, alijaribiwa mara kwa mara katika maisha yake yote ya soka.

Mnamo 2012, mwanasoka mwingine, Fabrice Muamba, alianguka uwanjani wakati moyo wake ulipoacha kupiga vizuri. Alihitaji kufanyiwa CPR mishtuko 15 ya defibrillator kwa jumla.