Kombe la Dunia Qatar 2022: Jamal Musiala - Je huyu ndio Messi ajaye?

Iliyochapishwa

Akiwa kijana aliyekosa thamani na rika lake, kijana wa Ujerumani Jamal Musiala sasa ana sifa ya kuwa "Lionel Messi ajaye".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alichukua nafasi muhimu katika kuwasukuma vijana wa Hansi Flick kufikia hatua muhimu Jumapili walipokuwa wakipigania mustakabali wao wa Kombe la Dunia katika sare ya 1-1 na Uhispania.

Na, wakati mchezo wa mabingwa hao mara nne wa dunia katika shindano hilo ukitiliwa shaka, umahiri wa kibinafsi wa kijana Musiala umesisitiza kipaji chake cha kusisimua.

Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, ambaye alitumia muda mwingi wa utoto wake nchini Uingereza lakini akachagua kuichezea nchi yake ya kuzaliwa, amekuwa taa ya Ujerumani nchini Qatar.

Wakiwa mkiani mwa Kundi E  na pointi moja, Ujerumani sasa wanahitaji kuifunga Costa Rica siku ya Alhamisi huku wakitumai viongozi Uhispania wataishinda Japan ili kukwepa kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika Kombe la Dunia.

Lakini nahodha wa zamani wa Ujerumani Lothar Matthaus anasema Musiala ni muhimu kwa matumaini yao sasa na siku zijazo.

"Anaweza kuwa Messi wa siku zijazo, ni mzuri sana," Matthaus, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka wa 1990, aliiambia BBC Sport. “Nimempenda kwa miaka miwili iliyopita, napenda mchezo wake na napenda utu wake.

"Ana umri wa miaka 19, anafanya vitu ambavyo vitamfanya kuwa mwanasoka wa hali ya juu. Ana pasi nzuri, ni mwerevu wa kufikiri na anapenda soka.

"Musiala anaweza kuwa Messi anayefuata kwa sababu Messi alipokuwa na umri wa miaka 17/18, nilikutana naye kwa mara ya kwanza alipocheza dhidi ya Hungary [timu niliyoiongoza wakati huo] na akatolewa nje baada ya sekunde 40.

"Aliingia uwanjani na kujaribu kuonyesha anapenda soka, ana mapenzi na soka, 'Nashukuru kuwa hapa ', na huyu pia ni Musiala. Nimekuwa shabiki wake mkubwa tangu miaka miwili iliyopita mara ya kwanza alipogunduliwa."

Takwimu za kuvutia za Musiala Jumapili usiku zilijumuisha usahihi wa pasi 84%, pasi 100% zikiwa zimekamilika, mipira saba ya makabiliano ardhini, pasi tatu muhimu na pasi ya mwisho ya iliosaidia kikosi cha Niclas Fullkrug kusawazisha.

Jamal Musiala alijiunga na Bayern Munich mwaka wa 2019, akiwa na umri wa miaka 16

Musiala tayari ndiye mfungaji mabao chipukizi zaidi wa Bayern Munich, mfungaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi wa Ujerumani na ndiye mwenye umri mdogo zaidi kuichezea Ujerumani kwenye michuano mikubwa aliposhiriki Euro 2020.

Sasa anapendekezwa kuwa athari kubwa zaidi kwenye jukwaa la ulimwengu.

Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino aliiambia BBC One: "Kwangu mimi, Jamal Musiala ni mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji.

"Akiwa na Gavi, akiwa na Jude Bellingham, Pedri, ni vipaji vikubwa. Nadhani atakua wakati wa Kombe la Dunia. Nadhani Ujerumani inaweza kushangaa."

Meneja wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann aliongeza: "Nadhani Musiala alikuwa mchezaji bora wa Ujerumani katika umri mdogo kama huu.

"Amejaa vitu vya kushangaza, haogopi. Ni mchezaji mchanga mzuri ambaye anakua kupitia mfumo wa Bayern. Ni Kombe lake la kwanza la Dunia na ataimarika zaidi na zaidi."Jamal Musiala

Jamal Musiala aliiwakilisha England katika kiwango cha timu za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 15, 16, 17 na 21.

Nini kitafuata kwa kijana huyo mzaliwa wa Stuttgart, ambaye alijiunga na Bayern mwaka wa 2019 akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kuingia katika shule ya mafunzo ya soka ya Chelsea na kuichezea Uingereza katika viwango vya vijana?

Mkataba wake utaendelea hadi 2026 huko Bayern na mwandishi wa habari wa Ujerumani Archie Rhind-Tutt anaamini kuwa hanunuliki kwasababu thamani yake ni zaidi ya Euro Milioni 400.

Aliiambia BBC Radio 5 Live: "Nadhani hii ni nafasi ya kweli kwake kutangaza kuwasili kwake kwenye jukwaa kubwa na kuona iwapo anaweza kuiburuza timu hii kwa mafanikio ya siku sijazo hivi karibuni. Ningesema. hii ni nafasi ya kweli kwake kuimarisha sifa yake.

"Kumekuwa na mazungumzo kwenye vyombo vya habari vya Ujerumani kwamba hawezi kuuzwa katika Bayern hadi kufikia kiwango ambacho hata euro 400m hazingetosha kwa Jamal Musiala.

"Hivi ndivyo anavyozungumziwa, yeye ndiye mustakabali wa klabu hii. Kuna mambo mengi sana kwenye mchezo wake ambayo yanamfanya awe mzuri. Hata wapinzani wanapojaribu kumkata kama wanavyomfanyia Lionel Messi kwenye mchezo kwa miaka mingi, hawachi soka . Yeye ni kiuongo muhimu kabisa."