''Safari ya kumtafuta baba yangu''

Maelezo ya video, Safari ya Mkenya kumtafuta baba yake mzazi ambaye hajawahi kumuona
Iliyochapishwa

Nchini Kenya, zaidi ya theluthi moja ya watu hukua katika familia za mzazi mmoja. Africa Eye inafuatilia safari ya kibinafsi ya mwanahabari Namukabo Werungah, ambaye hajawahi kumjua baba yake na ameamua kutafuta sehemu hii ya utambulisho wake. Hajui ikiwa yu hai au amekufa, lakini harusi yake inakaribia, ameamua kuwa ni wakati wa kujua historia yake. Je, atampata mwanaume ambaye alitakiwa kumwita baba? Na ikiwa atafanya hivyo, atamtaka maishani mwake?