Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni 'ushirikiano upi mpya' Ufaransa inataka kuimarisha na mataifa ya Afrika?
Siku moja kabla ya ziara katika mataifa ya Afrika Magharibi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizumzumzia kutoka Kasri la rais la Élysée kuhusu sera mpya na Afrika ambayo inalenga kuwa ya Ujumuishaji zaidi. Lakini tunaweza kujifunza nini kutokana na hotuba yake na hisia ilizoibua?
Hotuba ilitolewa mbele ya idadi kubwa maafisa ambao wanaandamana naye katika ziara yake katika mataifa ya Afrika ambapo jana alikuwa Libreville Gabon ambako alihudhuria kikao cha "One Forest Summit", kikao cha kuweka mikakati ya kulinda misiti ya maeneo ya joto, katika nyakati hizi za changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Ziara hii ya 18 ya Bw Macron katika mataifa ya Afrika itaendelea ambapo anatembelea Luanda, Brazzaville na Kinshasa wikendi hii.
Ziara yake inafanyika huku kukiwa na ongezeko la maoni ya chuki dhid ya Ufaransa katika mataifa yanayozungumza lugha ya kifaransa barani Afrika, hususan katika kanda ya Afrika Magharibi.
Ni kutokana na chuki dhidi ya Ufaransa, ambapo rais wa Ufaransa aliamua kuzungumzia sera mpya ya kigeni ya Ufaransa kwa mataifa ya Afrika, ikiwa na lengo la kujitenga na mwenendo wake wa zamani.
Katika sera hiyo Macron anazungumzia kuhusu njia nyingine ambayo haiiondoa Afrika katika hali ya ushindani na faida na kuzichukulia nchi za Afrika kama washirika ambao tumeshirikishana maslahi na wajibu. Na kimsingi , kujenga uhusiano mpya , wenye uwiano, na wenye uwajibikaji . »
Ushirika mpya
Jambo lingine ambalo jingine ambalo Rais Macron ambalo Macron anataka kulirejesha ni ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi yake na mataifa ya Afrika. Kulingana naye ni ukarabati wa ushirikiano wa pamoja.
“Inalenga kuona kwamba washirika wetu wa Afrika wanauna wazi kabisa jeshi lao na kuwa na mahitaji yao ya kiusalama, ambapo sisi tutawasisia katika mafunzo, na vifaa vya viwango vya juu ,” alisema.
"Lengo likiwa kwamba mtindo sasa hautakuwa wa kuweka ngome za kijeshi kama ilivyo kwa sasa ,"aliongeza Emmanuel Macron.
"Kipaumbele sasa kitapewa kwa uwepo ndani ya ngome, shule, vyuo ambavyo vitasimamiwa kwa ushirikiano , lakini kwa viwango vya chini na wafanyakazi wa kiafrika ambao wataweza kufanya kazi, kama washirika wetu wa Afrika watataka iwe hivyo na kwa sheria zao nchi nyingine pia ", alisema rais Macron.
Inaonekana Uraransa ilijifunza somo kutokana na uingiliaji wa jeshi lake katika Sahel, jambo lililopelekea kuondoka kwa vikosi vyake -Barkhane kutoka Mali, abaada ya miaka tisa ya uwepo wake nchini humo na lile la kumalizika kwa Operesheni ya Saber nchini Burkinafaso, kufuatia ombo la nchi hizo mbili za Afrika.
“Halikuwa jukumu la Ufaransa kutoa jibu la kisiasa pekee, ambalo lilikuwa ni matumizi ya kijeshi, hatahivyo, licha ya hayo sisi tulichukua wajibu, ”anatathmini Rais wa Ufaransa
Katika hotuba yake, rais huyo wa Ufaransa alidokeza kuwa nchi yake ni mshirika wa kwanza wa mafunzo ya kijeshi wa DRC.
Ubalozi wa Ufaransa katika DRC ulifahamisha hilo mwaka 2021, kama sehemu ya kujengea uwezo jeshi la DRC (FARDC). Ufaransa pia ilikuwa na ushirika wa kijeshi na Gabon(EFG)
''Hakuna la kukumbuka kuhusu ushirika baina ya Ufaransa na Afrika’’
Ufaransa haina mvuto tena kwa mataifa ya Afrika. Wawekezaji wa Kifaransa lazima wakubali ushindani wa kiuchumi barani, alisisitiza Rais Macron.
‘’Bado tuna mengi ya makampuni leo ambayo hayafanyi kazi bora kwa sababu ni Afrika. Haiwezi kuendelea tena. Na ninawaambia ukweli, sitatetea tena makampuni ambayo hayako tayari kupambana,” alitangaza Emmanuel Macron.
"Kwa upande wangu sina kumbukumbu nzuri ya uhusiano baina ya Ufaransa ‘’ aliongeza.
Jibu na matarajio
Ziara hii ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mataifa ya Afrika haionekani kuwa itafikia malengo ya Ufaransa barani Afrika.
Mjini Kinshasa, kituo cha mwisho cha ziara yake Macron, kuna ongezeko kubwa la matamshi ya chuki dhidi ya Ufaransa ambazo zilipungua wakati ambapo Ufaransa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alipoondoa vikwazo juu ya uagizaji wa silaha kwa DRC mwezi Disemba mwaka jana.
Hata kama kuna uhamasishaji wa maafisa wa Kinshasa kwa ajili ya makaribisho mazuri kwa Rais Macron na ujumbe wa Ufaransa , baadhi ya makundi ya kiraia, hususan lile la FILIMBI, la Mapambano ya kutafuta mabadiliko (LUCHA) na mashirika mengine Alhamisi asubuhi yalifanya maandamano ya kupinga ziara yake katika DRC.
"Rais Macron ni mmoja wa watu wa karibu zaidi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye anahusika na kuigawanya DRC. Sisi sio wajinga na Emmanuel Macron hakaribishwi hapa Congo,” alisema Maud-Salomé Ekila, ambaye alikuwa akizungumza nje ya ubalozi wa Ufaransa nchini DR Congo.
Christophe Lutundula, waziri wa mambo yan je wa DRC ana matumaini kuwa Ufaransa itatumia nafasi yake kuiambia Rwanda kucha kuunga mkono kuyumbishwa kokote kwa usalama wa DRC na kusambaratishwa kwa watu mashariki mwa nchi.
Shutuma za ghasia zimekuwa zikikanushwa kila mara na maafisa wa Rwanda ambao wanakanusha uhusika wowote katika kuyumba kwa hali ya usalama kunakoshuhudiwa DRC.
Mjini Luanda, suala la usalama wa chakula litajadiliwa, Ufaransa ikiwa ni nchi ya kwanza kutoa mafunzo ya kilimo nchini Angola ambapo nchi mbili zimeanzisha ushirikiano wa uzalishaji wa bidhaa za chakula.
Katika ajenda za Bw Macron, kuna mkutano na rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso, ambaye amekuwa rais wan chi hiyo kwa miaka 40, na mkutano mwingine ataufanya na Wafaransa wanaoishi Brazzaville.