Je, Sera ya kufanya kazi siku nne kwa wiki itawafanya wafanyakazi wengi kwenda ofisini?

Iliyochapishwa

Matarajio ya siku chache kufanya kazi bado inaendelea kushika kasi huku baadhi ya wafanyakazi wanaweza kujitolea kufanya kazi ili kupata siku ya ziada ya kupumzika.

Ofisi za mshauri wa mazingira Tyler Grange hujaa kila Jumatatu asubuhi. Mahudhurio sio lazima,Hamna tangazo lolote lilotolewa ya kurudi kufanya kazi ofisini, wala kwa wale wanafanya kazi nyumbani kuanza kufanya kazi ofisini siku ya jumatatu.

Lakini, tangu kuanza kutangazwa kuwepo kwa muswada wa kufanya kazi siku nne kwa wiki mwezi Juni 2022, wafanyakazi 100 wa Tyler Grange walio na ofisi binafsi nchini Uingereza huwa wanapenda saana kufanya kazi zao binafsi mara nyingi zaidi.

"Hapo awali, tulijitahidi kiwahimiza watu kuingia kazini mara moja au mbili kwa wiki ofisini ," anasema Simon Ursell, mkurugenzi mkuu katika ofisi ya Tyler Grange, huko Gloucestershire.

"Sasa, kwa ujumla tunakaa hadi siku tatu kwa wiki. Na Jumatatu sasa ni maarufu sana jambo ambalo halikua hapo awali.

Wakati wafanyikazi wa Tyler Grange wamekuwa na ratiba zinazobadilika kila wakati, Ursell anasema ukubwa wa wiki iliyofupishwa ya kazi hufanya ushirikiano wa kibinafsi kuwa muhimu.

"Mara tu unapoingia kwenye mdundo wa wiki ya siku nne, unagundua kuingia ofisini hufanya maisha yako kuwa rahisi.

Ushirikiano mara nyingi ni ngumu zaidi kufanya kazi kutoka nyumbani - kutengeneza kiasi cha kazi kinachohitajika katika wiki ya siku nne itakuwa ngumu sana.

Anasema Ursell, wafanyikazi wa kampuni hiyo wanafurahi na kujitolea kufanya kazi siku nne ofisini na baada ya siku nne huwa wanapata wikendi ndefu"

Jumatatu pia kuna shughuli nyingi ofisini, kwa sababu kila mtu anahisi kuwa katika mazingira mapya na kuwa tayari kukutana na wafanya kazi we zao baada ya kuwa na likizo ndefu.

Hali hii hata hivyo hufanya ufanyaji wa kazi nyumbani kuonekana kuwa jambo la kawaida .

Watu kuvutiwa na hatua ya kufanya kazi siku imekua kubwa . Wakati huo huo, kufanya kazi kwa mbali na kwa urahisi kumekuwa na mafanikio makubwa. Kwa hivyo, ni faida gani inayothaminiwa zaidi?

Ikiwa waajiri wangewaita wafanyikazi warudi ofisini, na kuwashawishi kwamba watakua wanafanya kazi kwa siku nne tu kazini, je, wafanyikazi wangekubali?

Data inayokua inaonyesha kuwa hata kukiwa na upinzani mkubwa wa wafanyikazi kurudi, wafanyikazi wengine wanaweza kuthamini wiki ambayo waningia ofisini siku nne tu kufanya kazi

Brendan Burchell, profesa wa sayansi ya kijamii katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alikuwa sehemu ya timu ya utafiti wa ubora wa miezi sita ya majaribio.

"Jambo la kawaida ambalo watu waliripoti ni kuweza kufurahiya siku ambazo wanakua nyumbani peke yao bila shinikizo la wakati," anasema.

"Wafanyikazi waliweza kuwa na wakati zaidi wa kuangazia upya utaratibu wa maisha yao ,kulea watoto na kupunguza majukumu mengine ya nyumbani."

Utafiti fulani unapendekeza idadi kubwa ya wafanyikazi sasa wanathamini wiki ya kazi ya siku nne zaidi ya kufanya kazi rahisi.

Data kutoka kwa tovuti ya kuorodhesha nafasi za kazi Hakika, iliotolewa na BBC Worklife, inaonesha kwamba utafutaji wa kazi katika ofisi ambazo watu wanafanyakazi siku nne kwa wiki iliongezeka maradufu nchini Uingereza na Marekani mnamo Februari 2023, wakati utafutaji wa majukumu ya mbali ulipungua.

Na katika uchunguzi wa Februari 2023 wa wafanyikazi 11,000 wa Uingereza na kampuni ya kuajiri ya Hays, 62% walisema wangependelea kufanya kazi kwa wiki fupi ya kazi kila siku ofisini kwa wiki ya siku tano katika muundo wa kawaida wa mseto.

Lakini , wakati ambapo asilimia kubwa ya watu wanaotaka kufanya kazi siku nne kwa wiki ikiingezeka ,matarajio bado hayapatikani kwa wengi.

Ni asilimia 5% tu ya washiriki wetu walifanya kazi kwa shirika ambalo ina mfumo wa kufanya kazi siku nne kwa wiki," anasema Gaelle Blake, mkurugenzi wa miadi ya kudumu huko Hays.

"Kwa hivyo, wakati waajiri wengine wameanza kujaribu wazo hilo, bado hatujaona likianza kwa upana zaidi.

Ingawa siku nne ya kufanya kwa wiki bado ni adimu, inaendelea kushika kasi. Na inaweza kuwa mbinu kwa wamiliki wa kampuni kuwarudisha wafanyakazi mahali pa kazi huku mipango ya kurudi ofisini ikikwama.

Ingawa uchunguzi wa Hays ulionyesha kuwa asilimia 58 ya waajiri walisema hawakuzingatia kutekeleza kazi siku nne kwa wiki ya , asilimia 34 walisema kuwa wangekuwa na uwezekano mkubwa ikiwa wafanyikazi watatumia siku zote nne mahali pa kazi.

"Inaonesha watu wanazidi kuwa wazi kwa uwezekano wa kufanya kazi siku nne," anasema Blake. "Kwa hivyo, inaweza kuwa kesi ya wataalamu kubadilishana muda zaidi ofisini kwa wiki fupi ya kazi."

Kinyume na kulazimisha watu kurudi ofisini, Ursell anasema wiki fupi ya kazi inawahimiza wafanyikazi kurudi ofisini.

"Inampa kila mtu maana ya kawaida ya kusudi na kuendesha kuwa na tija zaidi: wanataka kubadilika ili kuifanya ifanye kazi, kujifunza michakato mipya na kushirikiana zaidi kibinafsi."

Ursell anaamini kwamba wafanyakazi kwa upana zaidi wako tayari kurejea ofisini badala ya wiki ya siku nne kwa sababu ya malipo yake muhimu: wakati.

"Unawapa kitu ambacho pesa haiwezi kununua - siku ya ziada ya kupumzika," anasema Ursell.

"Ikilinganishwa na kufanya kazi nyumbani, ambapo lazima uendelee kuwa na tija kwa siku tano kwa wiki, bila shaka hii ni mabadiliko makubwa kwa maisha ya watu wengi zaidi."