Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Michael Olise kusalia Bayern Munich mpaka 2029?
Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl anasema winga wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 Michael Olise, ambaye amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa, hana kipengele cha kutolewa katika mkataba wake, ambao utaendelea hadi Juni 2029. (Talksport)
Newcastle United wanatathmini uwezekano wa kumrejesha kiungo wa kati wa Uingereza Elliot Anderson, 22, kwenye klabu, baada ya kumuuza kwa Nottingham Forest mwaka jana. (i Paper - usajili unahitajika)
Manchester United bado wana nia ya kumsajili kiungo wa Ujerumani Angelo Stiller, 24, lakini ada itakayotolewa na klabu ya Stuttgart kwa mchezaji huyo wa miaka 24 inatarajiwa kuwa zaidi ya €50m (£43.5m). (Sky Sports Germany)
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Conor Gallagher pia analengwa na Manchester United, ambao wanamwona mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20. (Football Insider)
Beki wa timu ya taifa ya England Harry Maguire huenda akaondoka Manchester United bila malipo mkataba wake utakapomalizika msimu ujao kwani klabu hiyo ya Old Trafford bado haijampa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 mkataba mpya. (Mail - usajili unahitajika)
Aston Villa na Newcastle United ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania mshambuliaji wa Porto na Uhispania Samuel Omorodion, 21, ambaye anakaribia kujiunga na Chelsea inawa amefanya mazungumzo na klabu ya Nottingham Forest pia. (A Bola - kwa Kireno)
Beki wa England Fikayo Tomori anajadiliana na AC Milan kuhusu mkataba mpya, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akisema hana nia ya kukihama klabu hiyo ya Serie A. (Fabrizio Romano)
Mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, huenda akahama klabu ya Crystal Palace na anatarajiwa kuelekea katika klabu ya Manchester United, Newcastle United na Tottenham. (Caught offside)
West Ham wanamtaka mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, na wanaweza kujaribu kumsajili kwa mkopo kutoka Manchester United mwezi Januari. (i Paper)
Borussia Dortmund, wanaweza kumtoa kwa mkopo mwezi Jnuari kiungo wa kati Muingereza Jobe Bellingham, 20, ambaye walimsajili kutoka Sunderland msimu uliopita. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi