Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 08.03.2024

Iliyochapishwa

Thomas Tuchel amelenga kurejea kama kocha wa Chelsea atakapoondoka Bayern Munich majira ya joto, lakini kocha huyo wa Ujerumani pia anavutiwa na Manchester United na Barcelona. (Sky Sports)

Wamiliki wa Liverpool walikutana na Michael Edwards Jumapili katika majaribio yao ya kumshawishi mkurugenzi wa zamani wa michezo wa klabu hiyo kuunda nafasi mpya baada ya Jurgen Klopp huko Anfield. (Mail)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema kiwango cha kuvutia cha timu yake mbele ya lango hakitabadilisha mipango ya klabu hiyo ya uhamisho, huku The Gunners bado wakitarajiwa kusajili mshambuliaji katika majira ya joto. (ESPN)

Mlinzi wa kushoto wa Arsenal Oleksandr Zinchenko analengwa na Newcastle United na Bayern Munich, huku The Gunners wakitaka euro 38.5m (£32.9m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, 27. (Football Transfers)

Wakala wa winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia anasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ataondoka Napoli ikiwa klabu hiyo ya Italia itapokea ofa ambayo haiwezi kukataa. (Gazzetta dello Sport )

Mabosi wa Manchester United wanatarajiwa kumzuia Mason Greenwood kwenda Marekani kwa ziara ya kujiandaa na msimu mpya baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza, 22, kurejea kutoka Getafe alikokuwa kwa mkopo. (Star)

Greenwood yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa na Barcelona, ambao tayari wameshapiga hatua kuelekea mkataba wa bei nafuu msimu huu wa joto. (Sport )

Chelsea itategemea mauzo ya faida msimu huu ili kufadhili mipango yao ya uhamisho, huku bodi ya The Blues ikilenga kuwaondoa wachezaji wa nyumbani kama vile kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, na mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 22. (Team talks)

Chelsea wameweka winga kuwa moja ya vipaumbele vyao, huku mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi chini ya umri wa miaka 21 wa Leeds United Crysencio Summerville, 22, akiwa mmoja wa walengwa wao wakuu. (Team Talks)

Wamiliki wa Chelsea wako chini ya shinikizo kutoka kwa kundi la mashabiki wa Strasbourg kubadili mkakati wao wa uhamisho baada ya kuwa na msimu mbaya tangu kundi la BlueCo lipate hisa nyingi katika klabu hiyo ya Ufaransa Juni mwaka jana. (90 min)

Manchester United wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo kufuatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kuwa na kiwango kizuri msimu huu. Manchester Evening News)

Vilabu vingi vya ligi ya Primea na vilabu vya kigeni vinamfuatilia mshambuliaji wa Birmingham City aliye na umri wa chini ya miaka 16, Tobey Ugorji (Football Insider)

Everton wako katika nafasi nzuri ya kumsajili fowadi wa Ireland Mason Melia, 16, kutoka St Patrick's Athletic. (Football Insider)