Tunachokifahamu kuhusu uwezekano wa kunyongwa kwa mwanasoka Amir Nasr-Azadani wa Irani

Amir

Chanzo cha picha, FIFPRO

Iliyochapishwa

Mwanasoka wa kulipwa wa Irani Amir Nasr-Azadani, 26, anakabiliwa na uwezekano wa kunyongwa baada ya kushiriki maandamano kuhusu haki za wanawake nchini mwake.

Lakini pia anashutumiwa kuwa mwanachama wa kundi lenye silaha lililohusika na mauaji ya maafisa watatu wa usalama mnamo Novemba 16 katika mji wa Isfahan (katikati mwa Iran), kwa mujibu wa Idhaa ya Kiajemi ya BBC.

Maafisa wa Marekani wamesema alikiri kufanya uhalifu huo na wana kanda za televisheni na ushahidi mwingine dhidi yake na washtakiwa wenzake ambao wako tisa kwa jumla.

Pia walisema kuwa hukumu dhidi ya mwanamichezo huyo bado haijatolewa. Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu ya Iran, hukumu yake inaweza kuwa na adhabu ya kifo iwapo itathibitishwa kuwa mshtakiwa alitumia silaha (bunduki).

 

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ujumbe huu wa Shakira unaungana na ile ya watu wengi, wanamchezo na watu mashuhuri kutoka kote ulimwenguni ambao wamekuwa wakitoa wito kwa siku kadhaa asinyongwe. 

Ukiacha mwanasoka wa Uhispania Marc Bartra, mchezaji wa soka wa Colombia Radamel Falcao aliandika kwenye Twitter "Hii haikubaliki.

Wote tunasimama na Amir Nasr-Azadani". Wakati huo huo, muungano wa wanasoka wa kulipwa duniani FIFPRO uliandika kwamba "umeshtushwa na kuchukizwa na habari kwamba mchezaji wa kulipwa Amir Nasr-Azadani anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa nchini Iran baada ya kufanya kampeni ya haki za wanawake na uhuru wa kimsingi katika nchi yake." 

"Tunasimama kwa mshikamano na Amir na tunataka adhabu yake ibatilishwe mara moja."

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Amir Nasr-Azadani ni nani?

Nasr-Azadani alizaliwa Februari 1996 huko Isfahan katikati mwa Iran. Alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Sepahan Sport ya Isfahan, ambayo inacheza katika ligi ya Iran (Pro League), ligi ya juu zaidi ya soka ya kulipwa nchini Iran. 

Mwaka 2014 alijiunga na timu ya Tehran Rah-Ahan, moja ya vilabu vikongwe nchini Iran ambayo kwa sasa inacheza Ligi ya Azadegan, ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini humo. Mwaka mmoja baadaye alijiunga na Klabu ya Tractor, kutoka jiji la Tabriz, kaskazini-magharibi mwa Iran, ambako alidumu hadi 2019. Baadaye, akawa sehemu ya timu ya Gol Reyhan Alborz.

Kukamatwa kwa Azadani  

Amir Nasr-Azadani anakabiliwa na hukumu yenye uwezekano wa kunyongwa mara tu kesi yake itakapofanyika.   Mfumo wa mahakama wa Jamhuri ya Kiislamu unaweza kumnyonga kwa uhalifu unaoitwa "moharebeh."

Mnamo Novemba 17, 2022, kifo cha Kanali Esmaeil Cheraghi wakati wa maandamano kote nchini kilikuja kujulikana.  

Siku tatu baadaye, tarehe 20 Novemba, shirika la utangazaji la serikali IRIB lilionyesha video iliyoonyesha kulazimishwa kukiri kwa watu watatu waliodai kushiriki katika mauaji ya Cheraghi.

Kufuatia video hiyo, mamlaka baadaye ilitoa jina la mchezaji wa Iran Amir Nasr-Azadani kama mmoja wa washukiwa, pamoja na Saleh Mirhashmi na Saeed Yaghoubi.  

Habari za ndani zilidai kuwa ni kweli Azadani alishiriki katika maandamano hayo, lakini kuhusika kwake na mauaji ya ofisa huyo wa jeshi hilo ni uongo kwa sababu hakuwepo eneo alikofia mtu huyo.  

"Chuki dhidi ya Mungu" 

Katika wiki za hivi karibuni, Iran tayari imetekeleza hukumu mbili za kunyongwa kwa watu wanaohusishwa na maandamano dhidi ya serikali yaliyoendelea katika miezi ya hivi karibuni ambapo raia wameasi utawala wa Kiongozi Mkuu Ali Khamenei. 

Maandamano ya kupinga kuanzishwa kwa makasisi wa Iran, yakiongozwa na wanawake, yalizuka baada ya kifo cha Mahsa Amini, mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikamatwa na polisi wa maadili mnamo Septemba 13 kwa madai ya kuvaa hijabu yake vibaya.

Iran

Chanzo cha picha, Reuters

Katika muktadha huo huo, hivi majuzi timu ya taifa ya soka ya Iran iligoma kuimba wimbo wa taifa wakati wa mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia nchini Qatar dhidi ya England. 

Viongozi wa Iran wameyataja maandamano hayo kuwa ni ghasia zinazochochewa na maadui wa kigeni wa nchi hiyo. Hata hivyo, idadi kubwa ya waandamanaji wamekuwa hawana silaha na wana andamana kwa amani. 

Kwa sasa, takriban watu 26 "wako katika hatari kubwa ya kunyongwa kuhusiana na maandamano hayo ya nchi nzima, baada ya mamlaka ya Iran kuwanyonga watu wawili kiholela baada ya kesi zisizokuwa za haki katika jaribio la kuzua hofu miongoni mwa watu na kumaliza maandamano," Amnesty International, iliandika katika taarifa yake. 

Kati ya watu hao 26, angalau 11 wako kwenye hukumu ya kifo na 15 wako kwenye mashtaka ya kifo na wanangojea kesi au kufikishwa mahakamani, shirika hilo lilisema. 

Ni nani walikuwa wa kwanza kunyongwa?

Mamlaka ilimnyonga hadharani Majidreza Rahnavard, 23, alfajiri ya Jumatatu, Desemba 12, katika jiji la Mashhad, mahakama ilitangaza.

Mahakama ilimtia hatiani kwa "chuki dhidi ya Mungu" baada ya kumpata na hatia ya kuwachoma visu hadi kuwaua wanachama wawili wa kikosi cha kijeshi cha Basij Resistance Force. Rahnavard alinyongwa siku 23 tu baada ya kukamatwa "mbele ya kundi la raia wa Mashhadi."

Katika video iliyoonyeshwa kwenye runinga ya serikali mnamo Novemba 19, baada ya kukamatwa kwake, Rahnavard anaonekana akiwa amezibwa macho na mkono wake wa kushoto ukiwa na plasta.

Khamenei

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maafisa wakuu wa Iran akiwemo Ali Khamenei wanaamini kuwa maandamano hayo yanachochewa kutoka nje ya nchi.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wanaharakati wanaeleza kuwa vyombo vya habari vya serikali mara kwa mara huonyesha video za wafungwa wanaokiri uongo baada ya kulazimishwa kusema hivyo kufuatia mateso ya kikatili. 

Wakati huo huo, kunyongwa kwa mara ya kwanza kwa muandamanaji kulifanyika tarehe 8 Desemba, na kusababisha shutuma nyingi za kimataifa. 

Mohsen Shekari, 23, pia alipatikana na hatia ya "chuki dhidi ya Mungu" baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia mwanachama wa Basij kwa panga huko Tehran. 

Shirika la habari la Mizan hapo awali lilisema alikuwa ameshtakiwa kwa kuwachoma visu na kuwaua watu wawili wa kundi la Basij kwenye mtaa wa Mashad mnamo Novemba 17. 

Kundi la Basij ni kikosi cha kujitolea ambacho mara nyingi hutumwa na mamlaka ya Iran ili kukabiliana na upinzani. 

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa waandamanaji wanahukumiwa kifo katika mahakama zisizo halali bila kufuata utaratibu. 

Mahmood Amiry-Moghaddam, mkuu wa shirika la Haki za Kibinadamu la Norway nchini Iran, alisema kwenye Twitter kwamba hukumu ya Rahnavard ilitokana na "kukiri kwa lazima, kufuatia kesi isiyo ya haki na kesi ya maonyesho."