Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Al-Hilal wamtolea macho Bruno Fernandes

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Saudi Pro League, Al-Hilal, imempa nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, 30, ofa ya mkataba na kumwambia kiungo huyo wa Ureno ana saa 72 kufanya uamuzi. (Mail)

Manchester City wameingia katika mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 wa Lyon, Rayan Cherki, ambaye pia amehusishwa na vilavu vya Liverpool na Chelsea. (Telegraph)

Tottenham wamepewa fursa ya kumsajili winga wa Bayern Munich na Ujerumani, Leroy Sane, 29, ambaye atakuwa huru mwishoni mwa mwezi ujao. (Sky Sports)

Everton wamejiunga na Leeds United katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United na England mwenye umri wa miaka 33, Callum Wilson, ambaye mkataba wake unamalizika mwezi ujao. (The Sun)

Manchester United wamekubali mpango wa malipo ya Liam Delap kwa Ipswich Town na sasa wanasubiri mshambuliaji huyo wa England kuamua hatua yake inayofuata. (ESPN)

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 40, anatarajiwa kuondoka Al-Nassr ya Saudi Pro League na kusaini mkataba na klabu mpya kucheza Kombe la dunia la klabu, ambalo litaanza Juni 15 nchini Marekani. (Telegraph)

Aston Villa wanaonekana kuwa tayari kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 18 wa Feyenoord, Zepiqueno Redmond, kwa uhamisho huru msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Arsenal wamefanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Sporting, Viktor Gyokeres, huko Lisbon na kutoa ofa ya pauni milioni 58.7 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden. (Correio da Manha)