Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: 10.12.2022

Iliyochapishwa

Msimu wa nahodha wa Ujerumani na Bayern Munich Manuel Neuer umekamilika baada ya mlinda mlango huyo kuvunjika goti lake wakati anateleza kwenye theluji.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, ​​ambaye timu yake ilishindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar, alisema ‘’nilikuwa najaribu kuondoa mawazo’’, katika safari hiyo.

Neuer alifanyiwa upasuaji kwa kuvunjika mguu sehemu ya chini, akisema upasuaji huo wa siku ya Ijumaa ‘’ulikwenda vizuri’’.

‘’Mwisho wa mwaka ungekuwa bora zaidi,’’ aliandika kwenye Instagram.

‘’Inauma kujua kwamba msimu wa sasa umekwisha kwangu.’’

Bayern wako kileleni mwa Bundesliga na wametinga hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa, ambapo watacheza na Paris St-Germain mnamo 14 Februari.

Klabu hiyo ya Ujerumani pia huenda ikamkosa mlinzi Lucas Hernandez, ambaye alipasuka mshipa wa goti lake la kulia akiichezea Ufaransa kwenye Kombe la Dunia.

Arsenal wanaweza kufufua hamu yao ya kumnunua mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 22, kufuatia jeraha la goti alilopata Gabriel Jesus, 25, alipokuwa akiichezea Brazil Kombe la Dunia. (Calciomercatoweb - in Italian)

Hata hivyo, Juventus watakuwa tayari kumtoa Vlahovic kwa Atletico Madrid katika mpango wa kubadilishana kiungo wa Ureno Joao Felix, 23. (Calciomercatoweb - in Italian)

Arsenal ni chaguo kwa winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane ikiwa mchezaji mwenye umri wa miaka 26 hatasaini nyongeza ya mkataba mwanzoni mwa msimu ujao. (Bild - in German)

Atletico Madrid inamstaajabia meneja wa zamani wa Uhispania Luis Enrique, 52, kama mrithi anayewezekana wa Diego Simeone - lakini wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Manchester United kwa huduma yake. (AS - in Spanish)

Manchester United itafungua mazungumzo ya kandarasi na Diogo Dalot, 23, atakaporejea kutoka Kombe la Dunia kufuatia beki huyo wa kulia kuonyesha uthabiti kwa Ureno. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Fiorentina Mfaransa Randal Kolo Muani, 24, ambaye thamani yake ni pauni milioni 26, anafuatiliwa na Liverpool, Tottenham na Atletico Madrid. (Fichajes - in Spanish)

Real Madrid wamekaribia Benfica kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wao wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21. (O Jogo - kwa Kireno)

Kiungo wa kati wa Poland Mateusz Klich, 32, yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya DC United, inayofundishwa na Wayne Rooney, kuhusu uwezekano wa kuhama kutoka Leeds United. (MLS Soccer)

Juventus wako tayari kumuuza Weston McKennie, 24, na wamemthamini kwa pauni milioni 26, huku Chelsea na Tottenham zikihusishwa na kiungo huyo wa Marekani. (Calciomercato via Metro)

Mlinzi wa Inter Milan wa Italia Alessandro Bastoni, 23, anasema meneja wa zamani Antonio Conte alijaribu kumsajili Tottenham msimu wa joto. (Corriere dello Sport via 90 min)

Everton wanatafuta uhamisho wa £35m kwa winga wa Watford Msenegal Ismaila Sarr, 24. (Mirror)

Meneja wa Newcastle United Eddie Howe anataka kuongeza kandarasi ya kipa wa Ujerumani Loris Karius, 29, mwezi Januari.

Kipa huyo wa zamani wa Liverpool, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Al Hilal siku ya Alhamisi, alisaini mkataba wa muda mfupi mwezi Septemba. (Chronicle Live)

Chelsea itamsajili kiungo wa kati wa Dynamo Moscow na Urusi Arsen Zakharyan iwapo vikwazo vya michezo na uhamisho wa pesa vilivyowekwa katika nchi ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 vitabadilika. (Nizaar Kinsella via Championat - in Russian)