Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 25.02.2024

Iliyochapishwa

Real Madrid wameanza kutathmini upya uwezekano wa kumsajili tena beki wa Ufaransa Raphael Varane, 30, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, ambaye klabu hiyo ya Uhispania ilimuuza kwa Manchester United.(Fichajes - kwa Kihispania.)

Rais wa La Liga Javier Tebas anasema kuna "uwezekano 99%" kwamba mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, atajiunga na Real Madrid baada ya kuondoka Paris St-Germain msimu wa joto. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Manchester City wameweka bei ya pauni milioni 100 kwa kiungo Kevin de Bruyne, 32, baada ya kutakiwa na Saudi Arabia. (Talksport)

Tottenham walijadiliana na Chelsea kumhusu kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher mwezi Januari na Spurs wanapanga kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 msimu huu wa joto. (Football Insider)

Liverpool wamewaorodhesha wachezaji Ruben Amorim wa Sporting Lisbon, 39, na Mjerumani Julian Nagelsmann, 36, kama njia mbadala iwapo watashindwa kumpata mkufunzi wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso kuchukua nafasi ya kocha anayeondoka wa Reds Jurgen Klopp. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco anasema klabu hiyo inanuia kuwabakisha kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 26, na mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 24, katika klabu hiyo licha ya wawili hao kuhusishwa na uhamisho. (Goal)

Beki wa AC Milan na Ufaransa Theo Hernandez, 26, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Bayern Munich kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies, 23, ambaye atauzwa na klabu hiyo ya Ujerumani msimu wa joto ikiwa hatasaini mkataba mpya. . (Sky Germany)

Leeds United wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips katika klabu hiyo iwapo watapandishwa daraja hadi Ligi ya Premia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa yuko kwa mkopo West Ham kutoka Manchester City.(Football Insider)

Arsenal, Manchester United na Tottenham wanatazamiwa kuwania saini ya kiungo wa kati wa Fenerbahce Sebastian Szymanski msimu wa joto, huku AC Milan na Inter Milan pia zikimuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 24. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 22, anataka kusalia Getafe, kulingana na rais wa klabu hiyo Angel Torres. Mshambulizi huyo kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Uhispania. (Metro)

Beki wa Uholanzi Denzel Dumfries, 27, ameanza tena mazungumzo na Inter Milan kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya Italia zaidi ya 2025. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano).

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi