Nini kimefanya Jamii ya Neanderthals kutoweka: vurugu au kujamiiana?

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzao wa ndani na Homo sapiens huenda kulichangia kutoweka kwa Neanderthals, utafiti mpya umegundua. Hatua hiyo ilipunguza idadi ya Neanderthals kuzaliana kwa kila mmoja, na hatimaye kusababisha kutoweka kwao, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Palaeo Anthropology.
"Kwa muda mrefu, fikra kuu ilikuwa ni kwamba kumekuwa na ushindani mkubwa wa rasilimali kati ya Homo sapiens na Neanderthals," Dk Lucile Crete aliiambia BBC.
Lakini utafiti mpya ambao Dk Crete aliandika pamoja na profesa Chris Stringer, mtafiti mkuu katika Jumba la Makumbusho la historia ya asili huko London, unaonyesha kwamba haikuwa vurugu, lakini ni kule kuingiliana (mchanganyiko) wa watu ambao ulidhoofisha kundi la jeni la Neanderthals.
"Tabia hii ingeweza kusababisha kutoweka kwa Neanderthal ikiwa wangekuwa wakizaliana mara kwa mara na Homo sapiens, ambapo ingeweza kuharibu idadi yao hadi kutoweka," profesa Stringer alisema baada ya utafiti kuchapishwa.
DNA ya Neanderthal inaweza kupatikana kwa kila mtu aliye hai leo, ikiwa ni pamoja na watu wa asili ya Kiafrika, ambao mababu zao hawafikiriwi kuwa walikuwa na mahusiano ya moja kwa moja na jamii hii.
Jamii za Neanderthals na Homo sapiens ziliibuka katika maeneo tofauti kote ulimwenguni baada ya kutofautiana karibu miaka 600,000 iliyopita.
Wakati Homo sapiens iliibuka barani Afrika, Neanderthals waliishi Ulaya na Asia. "Ugunduzi wa hivi majuzi unaonyesha Jamii ya Homo sapiens ilikuwa Ulaya miaka 50,000 au 60,000 iliyopita, ambayo ina maana kwamba walikuwa Ulaya kama ilivyo kwa Neanderthals lakini kwa muda mrefu zaidi kuliko tulivyofikiri hapo awali," Dk Crete alielezea.
Tunachojua kuhusu uzao wa Homo sapiens na Neanderthals

Chanzo cha picha, Reuters
Jeni za Neanderthal zilifanyiwa uchunguzi katika jeni za Homo sapiens, lakini si kinyume chake, utafiti unasema "Inaonekana kuna ubadilishaji wa jeni lakini kwa njia moja tu," alielezea Dk Crete. Tayari tulijua kwamba spishi mbili ziliunganishwa - ikiwa ulizaliwa nje ya Afrika, karibu 2% ya jeni zako inatokana na Neanderthals.
Lakini Dk Crete na Dk Stringer waliangalia zaidi suala hilo kwa kuchanganua kile kinachojulikana kuhusu jeni 32 za Neanderthal ambazo zimegunduliwa hadi sasa. Wanasayansi hao wawili wanapendekeza kwamba ikiwa kuzaliana kulifanikiwa ilitegemea jozi halisi iliyokuwa ikizaliana. "Lakini hatujui namna ya kuelezea hilo," Dk Crete alisema.
"Kwa aina fulani za ndege na wanyama, muingiliano huu wakati mwingine haufanyi kazi kwa njia zote mbili: inaweza kuwa vigumu kwa aina moja kuzalisha watoto wenye kustawi."

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Nadharia nyingine ambayo Dk Crete na Dk Stringer waliweka katika utafiti wao ni kwamba sio matukio yote ya kujamiiana yanaweza kuwa ya makubaliano.
"Labda Homo sapiens walikuwa wakienda kutafuta wanawake au njia nyingine na nguvu ilitumika kupata wanawawake wa kundi lingine," alisema Dk Crete.
Anaeleza kuwa tabia ya aina hiyo inaweza pia kuonekana katika baadhi ya sokwe. "Kama wanaume hawana wanawake wa kutosha wa kuzaa nao katika kundi lao, wanaweza kwenda kwwenye kundi lingine na kuwaiba ili kuendelea kujitanua," alisema.
Lakini ni kiasi kidogo inafahamika kuhusu kukutana kwa namna hiyo. Wanasayansi wanaamini kuwa haikuwa rahisi kwa Neanderthals na Homo sapiens kuwasiliana kwa kuwa walikuwa jamii tofauti kabisa.
"Labda wasingeweza kutoa sauti za aina moja, hawakuwa na usemi wa aina moja, ubongo wao ulikuwa na muundo tofauti," Dk Crete aeleza. Muonekano wao wa kimwili pia ulikuwa tofauti. "Neanderthal walikuwa imara kabisa, wamejengwa kwa nguvu na mikono na miguu mifupi na sehemu ya juu ya paji la uso juu ya macho yao," Dk Crete anaelezea.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lkini, bado haijulikani wazi jinsi Neanderthals wa kiume na wa kike walikuwa tofauti. "Mifupa kawaida hugawanyika na kuvunjika, na hatuna namna nyingi za kulinganisha na kutofautisha kati ya jamii hizo mbili," Dk Crete anasema.
Licha ya mambo mengi yasiyojulikana, Dk Crete anafurahia uvumbuzi unaowezekana wa siku zijazo. "Njia mpya ziliwezesha mambo ambayo hatukuweza hata kufikiria hapo awali," Krete alisema. "Ni kama chemshabongo kubwa. Wakati mwingine inakuwa kubwa zaidi na ugunduzi mpya unapobadilisha namna tunavyofikiri."












