el - Clasico: Je Barcelona itafurukuta mbele ya Real Madrid Jumapili?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mechi kati ya El Classico
Iliyochapishwa

Barcelona wanaingia kwenye mchuano wa Jumapili kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu sawa na Real Madrid wakiwa kileleni mwa La Liga na wakiwa wameruhusu bao moja pekee la ligi msimu mzima.

Maoni yaliibuka wakati kilabu kilipotumia euro 145m msimu wa joto kununua wachezaji, licha ya ugumu wa kifedha uliothibitishwa, lakini kwa mtazamo wa takwimu zingeonyesha kuwa ununuzi huo ulikuwa ukilipa uwanjani.

Takwimu katika soka wakati mwingine zinapaswa kuhojiwa

Mechi zao sita zilizopita za La Liga, ambazo hawajaruhusu hata kidogo hata bao moja, zimekuwa dhidi ya Real Valladolid, Cadiz, Elche na Real Mallorca - timu ambazo hazijulikani kwa umahiri wao wa kufunga mabao.

Takwimu pia hazioneshi kwamba ni mchezo mzuri wa kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen unaowazuia wapinzani.

Msimu huu, Barcelona tayari wameruhusu mabao saba katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakipoteza mawili, sare moja na kushinda moja.

Sare ya Jumatano ya 3-3 dhidi ya Inter Milan, inayopendwa na wasioegemea upande wowote lakini inayochukiwa na kocha wa Barcelona Xavi, huenda ina maana kwamba hivi karibuni watalazimika kuanza kupanga kampeni yao ya Ligi ya Europa.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Benchi la ukufunzi la Barcelona likiongozwa na Xavi

Inter wanahitaji tu kuifunga Viktoria Plzen ambao hadi sasa wameruhusu mabao 16 katika mechi nne ili kuhakikisha Barcelona haifuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa pili mfululizo.

Kinachofuata ni Clasico, na Real Madrid, ambao katika mashindano ya 'big boy' wako katika nafasi yao ile ile dhidi ya obora wa klabu zingine kubwa.

Ikiwa Barcelona itapoteza dhidi ya Real, itakuwa balaa.

  Habari mbaya kwa Barcelona

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Pande hizo mbili ziko kileleni mwa jedwali baada ya kuanza bila kufungwa msimu huu huku zikidondosha pointi mbili pekee kutoka pointi 24 zinazowezekana.

Kuna kitu cha kutoa na dalili za ni wapi hilo litafanyika zilikuwepo kwa wote kuona katika michezo yao ya hivi majuzi ya Ligi ya Mabingwa.

Real Madrid walisafiri hadi Warsaw kukabiliana na Shakhtar Donetsk na walihitaji bao la kichwa la dakika za mwisho kutoka kwa Antonio Rudiger ili kupokonya pointi moja.

Pande hizo mbili zimekabana koo katika kilele cha jedwali la ligi baada zote mbili kuandikisha matokeo mazuri katika mechi za kwanza za za msi ambapo zilipoteza pointi mbili kila moja kati ya 24.

Real madrid inaelekea Warsaw kukabiliana na klabu ya Shakhtar Donetsk na ilihitaji bao la kicha la dakika za mwisho  kutoka kwa Antonio Rudiger kupata pointi moja.

Wanaelekea Poland na pointi tisa mkobani, huenda kulikuwa na uzembe katika matkeo yao mbali na kubadilishwa kwa wachezaji.

Katika klabu ya Barcelona , Xavi aliwaongoza wachezaji wake , alipotaja mechi yao kama fainali na katika dakika arobaini na tano za kwanza kila kitu kilionesha kana kwamba mechi hiyo ingekuwa kama ilivyopangwa.

Kuanzia wakati Gerard Pique alisahau kuwazuia washambuliaji wa Inter na bao la kwanza likakubaliwa, mchezo ulibadilika na Pique, Eric Garcia na Marcos Alonso hawakuweza kukabiliana na hilo.

Mchezo huo ulichezwa na Barcelona kana kwamba ilikuwa imesalia dakika moja. Mechi hiyo ikawa ya bahati nasibu na bora kipa Ter Stegen aliyeokoa mikwaju miwili hatari karibu na mwisho kulinamaanisha kwamba timu hiyo ilikuwa na nafasi ndogo zaidi katika mechi ijayo

Kwahiyo tulichonacho sasa ni Barcelona ambayo inaweza kufanya anachotaka Xavi kwa dakika 45 tu, timu ambayo haiwezi kumudu mashambulizi ya timu nyengine .

Timu ambayo ina njia mbili za kufikiria juu ya kile kinachohitajika kufanywa - Xavi anataka udhibiti lakini wachezaji wanapendelea kushambulia haraka.

Kusafiri hadi Poland na pointi tisa tayari benki, kunaweza pia kuwa na kipengele kidogo cha kuridhika katika utendaji wao, pamoja na mzunguko wa kikosi.

Huko Barcelona, ​​Xavi alikusanya vikosi, akielezea mchezo kama "fainali ya kombe" na kwa dakika 45 za kwanza kila kitu kilionekana kama kinaweza kupangwa.

Kwa hivyo ni mambo gani muhimu katika el Clasico ya Jumapili hii?

Ter Stegen amesaidia kufifisha ukweli mkali wa kile kinachotokea kwa sasa na bila yeye ni vigumu kufikiria klabu ingekuwa wapi.

Hakuna aliye na uhakika ni nani atakuwa upande wa upinzani, huku Thibaut Courtois akiwa nje kwa mechi tatu zilizopita kutokana na jeraha la mgongo na bado hawezi kufanya mazoezi.

Andriy Lunin amechukua nafasi ya Mbelgiji huyo kwa tofauti lakini kwa namna fulani hawezi kabisa kushawishi ushindi wa mechi, imani ya kuleta tofauti ambayo Courtois anaileta. Lakini basi - mbali na huyo - ni nani angeweza?

Sahau kuwa mlinda mlango tu - Courtois ni mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa msimu huu.

Vipi kuhusu hali ya ulinzi?

Ligi ya Mabingwa imetuonyesha kuwa hii ni timu ya Barcelona ambayo haijirekebishi vya kutosha kwa mashambulizi ya kaunta ya wapinzani wake. Wanapodhibiti mchezo, wana uwezo wa kujilinda kama timu, lakini wanaporejea kwenye soka la box-to-box wanazembea.

Karim Benzema, Vinicius Junior, Rodrygo, Federico Valverde au yeyote atakayecheza ni tegemeo la kutisha kwa timu hii ya Barcelona inayoonekana kutetereka kwa sababu Real Madrid ni mojawapo ya timu bora zaidi duniani

  Je Rodrigo ndio Benzema mpya?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rodrygo

Rodrygo ni mzuri lakini hayuko kwenye kiwango cha Karim Benzema - bado, sio kwa chaki ndefu. Lakini angalau Real Madrid wanajua kuwa ndani yake wana mtu ambaye anaweza kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa.

Anashirikian vyema na wachezaji wenzake, anaweza kuwakokota mabeki, anaweza kushuka chini wakati mwingine na anaweza kufunga mabao. Dhidi ya Atletico Madrid kabla tu ya mapumziko ya kimataifa, alikuwa mchezaji bora kabisa.

Anaweza kuaminiwa kucheza kwa upana au kubainisha sehemu ambazo ataleta matatizo zaidi kwa mpinzani wake, ikiwa ni pamoja na nafasi ya kati inayokaliwa na Benzema.

Ni nani atakayelaumiwa Barcelona

Kwa Barcelona, El ​​Clasico ya Jumapili inaweza kuwa njia inayofuata ya kujifunza wanapojitahidi kutafuta utambulisho wao kwasababu Inaweza kuwa safari ngumu.

Ikiwa mechi hiyo itakasa kuzaa matunda , wa kwanza kukosolewa watakuwa wachezaji, haswa wakongwe walio na uzoefu kama vile Pique na Sergio Busquets ambao hawafanyi vizuri. Watu wengi wameanza kusema kuwa hawako tayari kucheza katika kiwango hiki tena.

Kisha, kulingana na kile kitakachotokea Jumapili, atakayefuata atakuwa meneja ambaye atashutumiwa haraka kwa kutopata matokeo bora kutoka kwa kikosi kilichoboreshwa kwa usaidizi wa karibu euro 145m katika majira ya joto.