'Kuwapoteza watoto wangu wachanga hivi ilinisikitisha’  

Khurshid Aman

Chanzo cha picha, Khurshid Aman

Maelezo ya picha, Zubaida  alisikitika sana baada ya kumpoteza mtoto wake mchanga kwa mara ya pili
Iliyochapishwa

Mimba zote za Zubaida ziliishia kuwa kujifungua watoto waliokufa. Aliishi katika mojawapo ya maeneo yenye joto sana duniani. Wanasayansi wamebaini kuwa wanawake wajawazito wanaoishi katika maeneo ya joto kwa vipindi virefu wana hatari kubwa ya kupata matatizo, ikiwa ni pamoja na kuwapoteza watoto wao wachanga.   

"Nilikuwa na vifo viwili vya watoto wanaozaliwa wakiwa wamekufa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita ", anasema Zubaida.

Zubaida mwenye umri wa miaka 30 anaishi kilomita 80 magharibi mwa miji wenye hali ya hewa ya joto zaidi duniani : Jacobabad, katika jimbo la pakistan la Sindh.

"katika mara zote, mkunga wetu wa asili katika jamii yetu alinisaidia," Zubaida aliiambia BBC.

"Wakati nilipompoteza mtoto wangu mchanga mwaka jana, nililia bila kukoma kwa siku kadhaa."

 Mume wake, Abdul Aziz, anakumbuka jinsi ilivyotokea. " Mimba ilikuwa karibu inakaribia kabisa kutimiza miezi tisa, lakini mtoto wetu wa kiume akafia tumboni."

‘’Alikasirika sana na alikuwa na wasi wasi kwamba huenda asiwahi kuwa na mtoto ". Nilimfariji na ndugu zetu wengi walikuja na kuzungumza naye ,"aliongeza.

Jacobabad  ni moja ya maeneo ya makazi yenye joto zaidi duniani. Wakati wa kiangazi, viwango vya joto hupanda hkuliko 50C.

Viwango vya juu vya joto na uzazi wa watoto aliokufa   

Ripoti iliyochapishwa hivi karibuni katika jarida la  kitabibu la Uingereza  ilikusanya nyaraka za tafiti kuhusiana na hali ya hewa ya joto na hatari za uzazi watoto wanaozaliwa bila muda wao kutimia, uzito wa chini wa watoto wanapozaliwa, na uzazi wa watoto waliokufa.   

Khurshid Aman

Chanzo cha picha, Khurshid Aman

Maelezo ya picha, Zubaida alikuwa amesafiri kilomita 80 kupata usaidizi wa matibabu yanayofaa  kutoka kwa daktari Khurshid Aman

Ulibaini hili kuwa moja ya visa vilivyochunguzwa, inaonekana kuwa kuna uzazi wa watoto wafu, wakati kunapokuwa na hali ya hewa ya joto zaidi .

Lakini watafiti walibaini kuwa ni vigumu kuelea ni vipi hasa joto linaweza kusababisha uzazi wa mtoto aliyekufa na matatizo mengine kama kuzaliwa kwa mtoto kabla ya muda.  

Daktari

Kwa sasa anapata ushauri kutoka kwa Dkt Khurshid kusaidia kuongeza fursa ya kujifungua mtoto mwenye afya. Madaktari wanasema kila wiki wanashuhudia walau wagonjwa watatu ambao walikuwa na uzazi wa watoto waliokufa.

 ''Katika eneo hili, yharibikaji wa mimba na uzazi wa watoto waliokufa  ni jambo la kawaida. Idadi yao huongezeka wakati wa miezi ya joto ," anasema Dkt Khurshid Aman.

 Anasema yote haya yanaweza kuwa na athari  juu ya mimba salama na watoto wachanga wenye afya. Aziz anasema ukosefu wa huduma za matibabu ni tatizo kubwa.

 

Joto na uzaidi wa watoto waliokufa   

Mwaka huu, watafiti wa Chuo kikuu cha  California walichapisha matokeo ya utafiti kuhusu watoto wanaozaliwa wanaozaliwa kabla ya muda na wnaozaliwa wakiwa  wamekufa katika nchi     14 za kipato cha chini na cha kati: Angola, Benin, Burundi, Ethiopia, Haiti, Malawi, Nepal, Nigeria, Philippines, Afrika Kusini, Tajikistan, East Timor, Uganda, na  Zimbabwe.

Jacobabad pia inakabiliwa uhaba wa kudumu wa maji 

Ukitazama ripoti ya hali ya jewa na utafiti binafsi wa wanawake, walibaini hilo. 

"Tulibaini kuwa hatari ya kujifungua mtoto aliyekufa inaongezeka kwa wanawake wanaoishi katika maeneo ya viwango vya joto kati ya 20-30C  kuelekea mwisho wa mimba zao, ikilinganishwa na wale wanaoishi katika maeneo ya joto la 20C . Hatari za uzazi wa mtoto aliyekufa huongezeka hadi mara mbili ,"Kiongozi wa uandishi wa utafiti huo, Sara McElroy, aliiambia BBC.

Usiku na mchana

Utafiti pia ulibaini kwamba wakati kuna utofauti  wa joto  mchna na usiku wa chini ya  16C kunakuwa na uzazi wa watoto waliokufa zaidi katika nchi walizofanyia utafiti.   

Licha ya ushahidi wa hali ya hewa ya joto kusababisha matatizo ya kiafya, Jacobabad bado haina uwezo wa kukabiliana na joto.

Zubaida na mume wake wanataka kuwa wazazi karibuni

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jacobabad pia inakabiliwa uhaba wa kudumu wa maji 

"Wanapaswa kujenga hospitali nzuri hapa. Hakuna lolote," anasema Aziz.

Nyumbani, ameweka mfumo wa nishati unaosaidia kukifanya kiyoyozi kiendelea kufanya kazi wakati umeme unapokatika 

Joto linawezaje kusababisha mwanamke kujifungua mtoto aliyekufa?   

Huduma za afya nchini Uingereza zinasema kuwa wakati wa vipindi vya joto, "idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa wakiwa wamekufa ambao vingenevyo wangezaliwa wenye afya hutoke, na sababu mara nyinyi haiwezi kuelezeka ."

Zubaida na mume wake wanataka kuwa wazazi karibuni

Chanzo cha picha, Khurshid Aman

Maelezo ya picha, Zubaida na mume wake wanataka kuwa wazazi karibuni  

"Wanapaswa kujenga hospitali nzuri hapa. Hakuna lolote," anasema Aziz.

Nyumbani, ameweka mfumo wa nishati unaosaidia kukifanya kiyoyozi kiendelea kufanya kazi wakati umeme unapokatika. 

Joto linawezaje kusababisha mwanamke kujifungua mtoto aliyekufa?   

Huduma za afya nchini Uingereza zinasema kuwa wakati wa vipindi vya joto, "idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa wakiwa wamekufa ambao vingenevyo wangezaliwa wenye afya hutoke, na sababu mara nyinyi haiwezi kuelezeka ."

Akina mama hupata changamoto ya kuendelea kuwakinga watoto wao dhidi ya joto lenye madhara

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Akina mama hupata changamoto ya kuendelea kuwakinga watoto wao dhidi ya joto lenye madhara  

 Sababu zinazofahamika  ni pamoja na matatizo ya kondo la nyuma la uzazi – kiungo ambacho huunganisha usambazaji wa damu ya mama kwa mtoto na kumlisha mtoto ndani ya kizazi   

"Mojawapo ya mambo yanayodhaniwa kusababisha tatizo hili ni ukosefu wa maji unaosababisha kuongezeka kwa joto unaoweza kuhamisha upelekeji wa damu kutoka kwa kijusi kinachokua hadi kwenye ngozi ya mama , kupoza joto la ndani ya mwili. Kuwa katika mazingira ya joto pia kunaweza kusababisha  hali inayofahamika kama hyperthermia ( kupanda kwa joto la mwili kusiko kwa kawaida) na kuharibu seli zinazowezesha mtoto kuzaliwa akiwa mwenye afya," anasema Dkt Sindana Ilango, mwandishi mwenza wa makala.

Mtoto

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mkulima mwenye umri wa miaka  17-  Waderi akimpungia mtoto wake wa kiume Amar Kumar kwa kiyoyozi,  katika wimbi la joto viungani mwa Jacobabad  

Katika mwaka  2020, ripoti ya kwanza kabisa kuwajhi kutolewa  na Umoja wa mataifa kuhusu uzazi wa vifo vya watoto waliokufa ilibaini kuwa visa milioni 1.9 vilitokea duniani mwaka 2019. Idadi hiyo ni sawa na mtoto mmoja kwa kila baada ya sekunde  kumi na sita. Nchini Pakistan, zaidi ya asilimia tatu ya viffo vya uzazi ni vya watoto wanaozaliwa wakiwa wamefariki.

 Tumaini

Katika  Jacobabad, Dkt. Khurshid ameona matumaini katika hospitali inayoendeshwa na serikali ya mtaa na na kujengwa kwa hospitali za kibinafsi.  Pia anatiwa moyo na ukweli kwamba wanawake wengi zaidi wa vijijini wanatafuta matibabu. 

Baada ya kupata ushauri w daktari, Zubaida kwa sasa anaepuka kwenda nje wakati wa mchana.      

Zubaida  hana tatizo lolote la kudumu la kiafya

Chanzo cha picha, Kurshid Aman

Maelezo ya picha, Zubaida  hana tatizo lolote la kudumu la kiafya  

Hana ukakika ni nini kilichosababisha ajifungue watoto waliokufa, pamoja na bwaba yake, anataka kupata mtoto mchanga.

 "Tuna matumaini kwamba kwa  matibabu yanayofaa  tunaweza kuw wazazi ,"anasema.

Zubaida kwa sasa anakula matunda na mboga zaidi  na anakaa ndani ya nyumba kadri awezavyo.   

 "Ni dhaifu kidogo na amepewa baadhi ya madawa na vyakula mbadala. Pia aliombiwa awe anakwenda hospitalini kupata ushauri wa daktari wa mara kwa mara.    

"Kwa baraka ya Mungu, Nina uhakika tutaweza kupata ujauzito karibuni na kuwa mama."