Watoto mapacha wanazaliwa wengi zaidi sasa tofauti na wakati mwingine

Chanzo cha picha, Getty Images
Watoto mapacha wamezaliwa wengi zaidi kwa miaka ya hivi karibuni ,watafiti wamesema.
Watoto mapacha wapatao milioni 1.6 wanazaliwa kila mwaka duniani kote, katika watoto 42 wanaozaliwa kuna mapacha kati yake.
Kuchelewa kuzaa na teknolojia za kitabibu kama vile IVF zimeongeza idadi ya mapacha kuzaliwa tangu miaka ya 1980.
Lakini inawezekana kuwa inaanza kushuka kuanzia hapa wakati watu wakilenga kupata ujauzito wa mtoto mmoja, ambalo ni jambo lisilo na hatari kubwa.
Kwa mujibu wa utafiti, jarida la the journal Human Reproduction, idadi hiyo imeongezeka kwasababu ya ongezeko la watoto mapachha katika maeneo mbalimbali kwa zaidi ya miaka 30 - kutoka ongezeko la 32% barani Asia mpaka 71% Marekani ya Kaskazini.
Watafiti wamepata taarifa kuhusu ongezeko la mapacha kutoka mataifa 165 kwa mwaka 2010 mpaka 2015, ukilinganisha na kiwango cha mwaka 1980 mpaka 1985.
Idadi ya maelfu ya mapacha wanaozaliwa ni kubwa kwa sasa barani Ulaya na Marekani Kaskazini - na duniani kwa ujumla imeongezeka kwa mapacha tisa mpaka 12 kwa watoto 1,000 wanaozaliwa.
Lakini idadi ya mapacha barani Afrika huwa iko juu na haijabadilika sana kwa miaka hiyo 30 iliyopita, hii inawezekana ni kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
Kwa sasa 80% ya mapacha wote duniani wanatokea barani Afrika au Asia.
Prof Christiaan Monden, mwandishi wa utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford, amesema kuna sababu ya kuwa hivyo.
"Idadi ya mapacha barani Afrika iko juu haswa mapacha wanaozaliwa na mayai mawili tofauti ," he said.
"Inawezekana ni sababu za kijenetiki kati ya idadi ya watu wa Afrika na maeneo mengine duniani."
Kiwango cha mapacha barani Ulaya , Marekani ya Kaskazini na mataifa yalioko maeneo ya bahari kumekuwa na ongezeko kwa kutumia teknolojia mpya za kitabibu tangu mwaka 1970 na hiyo ndio sababu kuu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Teknolojia kukua kumeongeza watoto kuzaliwa mapacha kwa wingi.
Wanawake wanaoamua kuanza familia kwa kuchelewa , wanaongeza idadi ya wanaotumia dawa za kujikinga na mimba na idadi ya wanaozaa kuwa ndogo, utafiti unasema.
Lakini suala linalosisitizwa sasa ni kupata mimba ya mtoto mmoja, anasema Prof Monden.
"Hili ni muhimu kuhusisha ongezeko la vifo vya watoto na wajawazito kupata matatizo wakati wa kujifungua au hata baada ya kujifungua," amesema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapacha husababisha matitizo zaidi wakati wa kujifungua , watoto kuzaliwa kabla ya muda au kuzaliwa na uzito mdogo .















