Jinsi ilivyoamuliwa kwamba Januari ndio mwezi wa kwanza wa mwaka

Iliyochapishwa

Kila mwaka tarahe kama hii watu kutoka kote duniani hukaribisha mwaka mpya kwa fataki, kupiga filimbi, pambaja na vinywaji.

Lakini kabla ya kuanza sherehe hizo je hujafikiria ni kwa nini tarehe mosi Januari ndio inayoadhimisha kuanza kwa mwaka mpya?

Kila kitu kinatokana na mila na tamasha za Roma, na kalenda iliyozinduliwa na Julius Caesar miaka 2000 iliopita.

Lakini pia huwezi kumwacha nje papa aliyejulikana kwa jina Gregorio wa kumi na tatu.

Hebu tuone ni kwa nini?

Kwa Waroma wa zamani, Januari ilikuwa muhimu kwa sababu ulikuwa mwezi uliotakaswa kwa Mungu Janus (hivyobasi ukaitwa Ianuarius, ikimaanisha Januari kwa kilatini}

"Inahusishwa na kuangalia mbele na nyuma," anaelezea Diana Spencer, profesa katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

"Kwa hiyo ikiwa kuna muda katika mwaka ambao unapaswa kuamua, huu ndiyo wakati tunapoanza tena." Ni mantiki kuwa hivi ".

Pia unafanana na muda kama ule wa Ulaya ambapo siku zinaanza kuwa ndefu baada ya msimu wa baridi.

"Waroma walihusishwa nao sana kwa sababu hutokea baada ya siku fupi, wakati ambapo dunia ina giza ,baridi na hakuna kitu kinachomea, kulingana na Professa Spencer.

''Ni Muda wa kupumua na kutafakari''.

Baada ya Waroma kuwa na mamlaka zaidi, walianza kusambaza kalenda yao katika ufalme wao mkubwa.

Kulingana na itikadi za Roma, Janus ni mungu wa nyuso mbili, mwanzo na mwisho .

Lakini katika miaka ya kati , baada ya kuanguka kwa ufalme wa Roma , Ukristo uliokuwa umejiimarisha hivyobasi tarehe mosi Januari ilionekana kuwa tarehe ya Kipagani.

Mataifa mengi yaliyotawaliwa na Ukristo yalitaka mwaka mpya kuadhimishwa tarehe 25, ambayo inaadhimisha tarehe ambayo malaika Gabrieli alijitokeza kwa bikira Maria mtakatifu.

''Ijapokuwa siku ya krismasi ni siku ya kuzaliwa kwa Yesu, tarehe muhimu ni wakati malaika huyo alipomwambia Mariam kwamba atajifungua mwana'', Spence aliiambia BBC.

Huo ndio wakati ambapo hadithi ya Yesu ilianza , hivyobasi ilikuwa na maana kuu kutaka mwaka mpya kuanza siku hiyo.

Hata hivyo Uingereza ambayo ilipinga amri ya papa na kuchukua dini ya Wapinzani wa papa waliendelea kusherehekea Machi 25 hadi mwaka 1752.

Mwaka huo sheria ya bunge la Uingereza ilioana na ile ya mataifa mengine ya Ulaya.

Leo, mataifa mengi huongozwa na kalenda hiyo ya Gregorian, na ndio sababu fataki hupigwa kote duniani ifikiapo tarehe mosi mwezi Januari kila mwaka.

Imechapishwa na Esther Namuhisa