Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Kuishi na matiti makubwa kulinifanya nitamani kujificha'
Aibu na maumivu - ni maneno mawili tu ambayo wanawake wametumia kuelezea uzoefu wao wa kuwa na matiti makubwa.
Jackie Adedeji anafikiri kuwa na matiti makubwa zaidi sio jambo linalochukuliwa tatizo lenye uzito na anasema linachukuliwa tu kama jambo la "ya kuchekesha na ya kipumbavu" nchini Uingereza.
Anasema kutokana na ukubwa wa matiti yake kumemfanya atake kujificha katika nyakati fulani maishani mwake.
"Tangu niliwa na umri wa miaka 11 nakumbuka nikikutana na wanaume walionionyesha kuwa wakuwa na shauku ya kujamiiana nami, nakumbuka matukio ya wazi nilipokuwa nikitembea kwenda shule shule nikikutana na wanaume wakubwa wakinipita wakilamba midomo yao," aliambia BBC Newsbeat.
"Mimi pia nimekuwa kwenye mikutano, ambapo wenzako wanakukodolea macho, na kukufanya uhisi kama uko hapa kuwa chombo cha ngono."
Jackie, ambaye amechunguza masuala haya katika filamu mpya ya Channel 4 ya hali halisi ya My Big Boobs: UNTOLD, anasema amejifunza kuukubali mwili wake kulingana na umri.
Lakini kuna wanawake wengi ambao hufanyiwa upasuaji wa matiti, na ni jambo ambalo linazidi kuwa la kawaida.
Chama cha Uingereza cha Madaktari wa Urembo wa Plastiki (BAAPS) kinasema kupunguzwa kwa matiti ni utaratibu wa pili maarufu wa urembo nchini humo.
Kinasema kulikuwa na matukio 5,270 ya kupunguzwa kwa matiti miongoni mwa wanawake mnamo 2022, kiwango hiki kikiwa ni hadi 120% kutoka mwaka uliotanguliwa wa 2021 na idadi hiyo ilikuwa ni ya juu zaidi kabla ya janga la Covid.
Jackie anasema hadhani kama watu huelewa "inavyotesa kiakili" kuwa na matiti makubwa.
"Watu wenye matiti makubwa hujihisi kuwa na aibu, kwa sababu watu wengi wanahisi umiliki wa matiti yako, wanapokuwa wakubwa, wanaonekana kama mali ya umma," anasema.
Na amepata shinikizo za kitamaduni pia - alikulia katika nyumba ya kidini ambapo kulikuwa na matarajio ya unyenyekevu.
"Unastahili kuwa mrembo na zaidi ya hayo, kama mwanamke mweusi, daima unataka kukutana kwa njia chanya iwezekanavyo na mara nyingi nilihisi kuwa matiti yangu hayakuonekana kama kitu kizuri."
Mwacheni
Amber aliamua kuishi maisha ya faragha mwanzoni mwa 2022,
Baada kuishi miaka mingi ya maisha ya maumivu ya kiakili na kimwili kutokana na ukubwa wake wa matiti, upasuaji alihisi upasuaji ulichukua muda mrefu
“Nilikuwa nikiteseka tangu nilipoacha shule, lakini baada ya kumnyonyesha binti yangu uchungu ulifikia hatua ya kutembea kwa shida bila kuumia,” anasema, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26.
Mwanzoni, alijaribu kupata upasuaji katika taasisi ya afya ya Uingereza NHS lakini walimkatalia mara kadhaa.
"Mimi na mume wangu tulikuwa na mazungumzo ya muda mrefu, na tukaamua kuchukua mkopo," anasema Amber, ambaye hatutumii jina la ukoo kwa ombi lake.
"Ingawa matatizo ya kifedha yalikuwa tatizo kubwa, operesheni ilikuwa uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya."
Huduma ya kupunguza matiti si jambo la kipekee la kuwa vigumu kupata katika NHS na kama opera zingine, nilisubiri kwa muda mrefu.
Hatahivyo Rachael mwenye umri wa miaka 28, alifanikiwa kupata huduma ya kufanyiwa upasuaji wa kupunguza matiti katika NHS.
Lakini hiyo ilikuwa miaka 10 baada ya kumwendea daktari wake akiwa na maumivu ya mgongo na wasiwasi kwa sababu ya kutaniwa kuhusu matiti yake.
Rachael aliambiwa apunguze uzito, licha ya kuwa na uzazi wa kawaida wam wili- BMI unaotakikana kiafya, na ndipo alipogundulika kuwa na maumivu ya mgongo ya muda mrefu ndipo alipohisi kuwa suala lake lilichukuliwa kwa uzito.
"Nilijaribu dawa za kutuliza maumivu kwa miezi sita kabla ya kuwekwa kwenye orodha ya wanaosubiri upasuaji na kutoka hapo ilichukua miaka miwili," anasema.
Rachael - ambaye hatutumii jina la ukoo – anasema kuwa alikwua mwenye bahati sana na anasema maisha yake baada ya upasuaji wa kupunguza matiti yake yamekuwa bora zaidi.
"Kabla ya upasuaji, sikuweza kukimbia bila kuwa na maumivu makali. Kwa hivyo hiyo ni moja ya faida kubwa. "Kwa hakika ninahisi mwili wangu uko vizuri zaidi kuliko nilivyokuwa."
Rachael anasema kuambiwa kula chakula alipokuwa na umri wa miaka 16 kulisababisha matatizo mengi ya kisaikolojia.
Kwa nini wanawake wengi hupunguzwa matiti?
Makamu wa rais wa cha madaktari wa upasuaji wa urembo- BAAPS Nora Nugent anaamini ni kwa sababu upunguzaji ni utaratibu mzuri wenye manufaa ya kiutendaji na ya urembo.
"Inasaidia katika suala la starehe ya kimwili, muonekano wa mwili, na vitendo, hata vitu kama vile mavazi ya kufaa," aliambia BBC.
Daktari wa upasuaji wa plastiki pia anaamini kuwa utaratibu huo unazidi kuwa mwiko.
"Kwa muda mrefu upasuaji ulikuwa na usiri unaohusishwa nao na ingawa kupunguzwa kwa matiti sio urembo, ulihusishwa katika hili.
"Kwa hivyo watu hawakuzungumza juu yake. Sasa, upasuaji huu uko wazi zaidi."
Taasisi ya huduma za afya nchini Uingereza -NHS England ilituambia kuwa amana za watu binafsi hutunza kupunguzwa kwa matiti - na hiyo inajumuisha jinsi wanavyoamua ni nani anayeweza na asiyeweza kufanyiwa upasuaji.
Utaratibu huanza na ushauri wa daktari ambapo wagonjwa hutathminiwa tathminiwa kulingana na matatizo waliyonayo kama vile maumivu ya mgongo na shingo na vile vile maswala ya afya ya akili.
Ikiwa daktari anafikiri kuwa unafaa, utawekwa mbele ili uangaliwa na daktari wa upasuaji wa matiti lakini unaweza kusubiri kwa muda ili kupata tathmini.
Uamuzi wa mwisho hufanywa na timu ya madaktari.
Kwa Jackie, anajua filamu yake ya hali halisi haitapunguza muda wa kusubiri lakini matumaini yake ni kwamba itawahamasisha watu kuwa na huruma zaidi kwa watu wenye matiti makubwa zaidi.
"Ningependa kuona huruma zaidi kwa wanawake walio na matiti makubwa, kwa sababu ninataka watu wafikirie ikiwa watawahi kuona mwanamke akitembea barabarani na ana matiti makubwa, anaendelea na maisha yake mwenyewe, waachane naye."