Je, wafanyakazi vijana wanaweza kujieleza bila kumkasirisha 'bosi'?

Iliyochapishwa

Wafanyakazi wachanga wanataka sauti zao zisikike ofisini. Wakati huo huo, baadhi ya wafanyakazi wa vyeo vya juu wanafikiri wenzao wachanga wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu kwanza, ili kufikia fursa hii.

Nguvu kazi inazidi kutawaliwa na watu wa umri mkubwa. Pamoja na mabadiliko haya, kuna tofauti moja ambayo inazidi kuwa wazi ambayo inatofautisha kizazi hiki cha vijana na kizazi kilichopita.

Wafanyakazi vijana wanataka kusikilizwa mahali pao pa kazi, wakati wa kutoa maoni yao na kukuza uvumbuzi, kuuliza kuhusu mshahara na marupurupu mengine.

Hata wakati wa kujadili mada muhimu, kama vile maadili ya kampuni wanazofanyia kazi na maswala ya tofauti.

"Wafanyakazi hawa wanaonekana kuwa huru zaidi kuzungumza juu ya kubadilika kwa kazi, usawa wa maisha ya kazi, na juu ya matarajio ya maisha yao ya kazi, ikilinganishwa na vizazi vya zamani," Martin Kilduff, profesa ambaye ni mtaalamu wa tabia ya shirika katika Chuo Kikuu cha London London.

Alichosema Profesa Kilduff hata kilimtokea mfanyakazi wake mpya ambaye alimteua kama msaidizi wa utafiti.

"Wanazungumza zaidi - kwa njia chanya. Wanakuambia juu ya kile wanachofikiria."

Lakini wakati wafanyakazi vijana wanataka kusikilizwa, wanakabiliwa na kizungumkuti.

Licha ya hamu yao ya kuzungumza - na mara nyingi kuhimizwa na wakuu wao na wafanyakazi wenza kufanya hivyo - wanaona ni vigumu kueleza wasiwasi wao au kujitetea wenyewe.

Mara nyingi, wanakutana na wasimamizi wakubwa, ambao bado wanatarajia wafanyikazi vijana "kujitolea kwanza" kabla ya kuzungumza kwa sauti.

Pia wanatarajiwa kutofanya jambo lolote linalowasumbua au kuwaudhi wafanyakazi wengine ili kupata cheo cha juu.

Je, wafanyakazi vijana wanapaswa kukabiliana vipi na tofauti hizi - na je, wanaweza?

Ingawa zinaungwa mkono na idadi inayoongezeka, kanuni za zamani bado zinatumika mradi wako kwenye usukani wa kampuni.

'Wajibu wa kimaadili kuwa na maoni'

Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu za kazi zimebadilika sana, ikiwa ni pamoja na hamu ya kusikilizwa kwa wafanyikazi.

Hii si tamaa mpya kabisa. Katika utafiti wa 2011 wa wafanyakazi wa umri mkubwa - ambao wakati huo walikuwa kizazi cha chini kabisa mahali pa kazi - 90% waliamini kwamba viongozi wanapaswa kusikiliza mawazo yao.

Hili linadhihirika zaidi kadiri watu wengi wa umri mdogo  wanavyoingia kazini.

Wataalamu wanasema wafanyakazi vijana wanafuata nyayo za watu wazee ambao wanataka kusikilizwa. Katika baadhi ya matukio, wanatamani wangeweza kuzungumza kuhusu masuala zaidi, ikiwa ni pamoja na kubadilika, mshahara na maadili ya kampuni.

"Wafanyakazi vijana wanahisi kuwa kuongea ni wajibu wa kimaadili, na hiyo inaweza kuwashika watu wengine ikiwa hawajazoea kushughulika na siasa za ofisi," Haydn Shaw, mwandishi wa Sticking Points: Jinsi ya Kupata Vizazi 4 Vinavyofanya Kazi Pamoja. Maeneo 12 Yanajitenga.

Kuna sababu nyingi kwa nini wafanyikazi vijaan wanazidi kuwa na ari kuongea.

Kwanza, wanaleta maadili yao mahali pa kazi, wakisisitiza mambo kama maadili ya kampuni na msimamo wa kisiasa, pamoja na usawa na ushirikishwaji.

Utafiti pia unaonyesha kuwa wafanyakazi vijana, haswa wanataka kufanya kazi kwa kampuni ambazo zina wafanyikazi tofauti.

Hali za sasa za kiuchumi zinaweza pia kueleza ni kwa nini wana hamu sana ya kujitetea kwa njia ambazo vizazi vya zamani haziwezi kufanya, anasema Kyle Brykman, profesa msaidizi wa usimamizi katika Chuo Kikuu cha Windsor, huko Ontario, Kanada.

Wafanyakazi wanapojikuta katika nafasi nzuri zaidi katika soko la ajira katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mabadiliko katika vipaumbele ili wafanyakazi wa umri wote kuzingatia haki kama vile kubadilika ambapo hapo awali haikufanyika.

Wakati huo huo, wafanyakazi hawa wanafahamu kwamba wana matarajio mengine ya kazi, ikiwa wakubwa wao hawatasikia kuhusu hilo.

Kuiweka kwa njia rahisi kuwa na ujasiri wa kutetea, wakati wafanyakazi wanajua kwamba mtumwingine kuchukua nafasi yao itakuwa vigumu zaidi na gharama kubwa.

"Ni soko la muuzaji, sio soko la mnunuzi," Shaw alisema.

Kwa wafanyikazi wengine ambao wanataka kuwa katika nafasi ya ushawishi, wana bahati. Makampuni mengi yanakuza mazingira ambapo vijana wanahusika katika majadiliano, na wanahimizwa kikamilifu kutoa maoni yao.

Katika baadhi ya matukio, madai ya vijana sasa yanasukuma makampuni kuajiri wataalam wa anuwai na ujumuisho, na kutoa mafunzo juu ya upendeleo usio na fahamu.

Makampuni pia yanazidi kufanya kazi ili kuanzisha programu zinazoomba kwa uwazi sauti, mawazo na maoni kutoka kwa wafanyakazi vijana.

Juhudi hizo ni za manufaa kwa kampuni, ikizingatiwa kuwa mchakato wa kuajiri ni wa gharama kubwa, huku vipaji vikiwa haba, alisema Kilduff.

"Ni kwa maslahi ya makampuni kujua nini kinaendelea na vijana wanaowaajiri," alisema. "Kampuni inataka kuwaweka."

Kukaa kwenye kiti cha ziada

Ingawa baadhi ya makampuni yanaunga mkono wafanyakazi vijana, si wafanyakazi wote vijana wako katika mazingira ambapo sauti zao zinaungwa mkono au kukubalika.

Pengine hii ni kutokana na ukweli kwamba bado kuna kanuni na mitazamo mingi iliyojengeka katika sehemu za kazi, inayotokana na kizazi kilichopita, ambacho bado kiko madarakani.

Mara nyingi, wafanyakazi wakubwa wanatarajia kuona kizazi hiki kipya kikisubiri zamu yao ya kuzungumza.

"Vizazi vilivyotangulia vilifundishwa kuketi kwenye meza ya ziada kwenye chakula cha jioni cha familia, hadi ulipoalikwa kwenye meza kuu," anasema Shaw.

"Wazo la 'subiri zamu yako' kuzungumza hutawala maisha yote."

Utafiti kutoka kwa jukwaa la mitazamo ya wafanyikazi ulionyesha nusu ya wafanyikazi walio na umri wa zaidi ya miaka 45 wangependa kupiga marufuku mijadala ya siasa ofisini.

Wakati huo huo, chini ya wafanyikazi watatu, kati ya wafanyikazi 10 wachanga, walikubaliana na dhana hiyo.

Baadhi ya 'kanuni' za mahali pa kazi hapo awali zimekita mizizi katika maisha ya kila siku kama kawaida.

Wazee wanatarajia heshima kutoka kwa kizazi kipya

Hii inaathiri wafanyikazi vijana. Utafiti unaonyesha wafanyakazi wapya, kwa mfano, wana uwezekano mdogo wa kuzungumza kuliko wenzao wakubwa.

Wanapofungua sauti zao, mawazo yao yanahusishwa na watu wengine.

Hata hivyo, inaweza kuwa tatizo, hasa kwa makundi ambayo tayari yametengwa.

Utafiti umebainisha hali kama hiyo kwa watu wanaojitokeza katika ofisi, iwe kwa sababu ya umri, rangi, kabila, jinsia, au sababu nyinginezo.

Hii ni changamoto inayokua kwa sababu, nchini Marekani, wafanyakazi  vijana watakuwa kundi tofauti zaidi.

Tofauti isiyofaa

Lakini, sio wasimamizi wote wanaokataa kusikia kile ambacho wafanyikazi wachanga wanasema.

Sehemu ya tatizo la meneja, anasema Shaw, ni kwamba hakuna mtu anataka kuwa mtu mbaya na kukataa ombi au wazo.

"Siku zote hatuna majibu ambayo watu watafurahi," anasema.

Zaidi ya hayo, baadhi ya wasimamizi wakubwa hawana raha kushughulikia masuala ambayo wafanyakazi wachanga wanataka kuleta kazini, kwa sababu ya mgawanyiko wa vizazi.

"Kuonyesha hisia kazini ni mabadiliko makubwa. Na mawasiliano haya makubwa ya kihisia wakati mwingine ni zaidi ya tunavyotarajia, na wasimamizi hawajui jinsi ya kushughulikia hilo," Shaw alisema.

Je, wafanyakazi wachanga wanapaswa kuweka maoni yao kwao wenyewe kwa sasa? Jibu ni ndiyo na hapana.

Wafanyakazi wachanga wanaweza wasiweze kujitetea jinsi wanavyotaka kuwa - au kwa jinsi wenzao wakubwa wanavyoweza.

Hata hivyo, wanaweza kutafuta washirika wa kuwasaidia.

Kilduff anaamini kwamba kwa kutafuta washirika waandamizi zaidi, kuna uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kutokana na kuongeza "uhusiano wa karibu" na wafanyakazi waandamizi zaidi au washauri ambao wanaweza kusikilizwa sauti zao.

Kuajiri wataalamu wachanga ni ghali – inagharimu pesa nyingi kuwatafuta, kuwaajiri, kuwaleta na kuwafundisha,” alisema Kilduff.

"Ikiwa hawana furaha na hawakuambii, utapoteza uwekezaji wako."

Zaidi ya hayo, anasema Brykman, kuhitaji wafanyikazi kuwa na mtaji wa kijamii kabla ya kuzungumza kunaweza kuzuia utendaji wa shirika.

"Mawazo ya ubunifu na mapya yatatoka kwa wafanyakazi wapya. Tunaweza kukandamiza uvumbuzi kwa kuomba mtaji wa kijamii, kabla hawajazungumza."

Lakini wafanyakazi wachanga wanaweza kuishia kulazimika kuwa waangalifu zaidi wakati kizazi cha wazee bado kinadhibiti na kufuata kanuni fulani za mahali pa kazi.