Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Amasia: lini, wapi na jinsi gani bara jipya linalofuata litaundwa?
Mtindo mpya uliobuniwa na watafiti wa Australia unatabiri kwamba bahari ya Pasifiki itatoweka, na kuunganisha mabara yatakayounda bara jipya linaloitwa Amasia, karibu na ncha ya Kaskazini.
Lakini, kulingana na mpango huo, hilo halitafanyika hadi baada ya kipindi cha miaka mingine milioni 200 au 300.
Hali iliyokadiriwa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Curtin nchini Australia na Chuo Kikuu cha Peking nchini China inatabiri kwamba bara la Marekani litahamia magharibi na Asia kuelekea mashariki, Antaktika kuhamia Amerika ya Kusini, Afrika itaungana na Asia kwa upande na Ulaya kwa upande mwingine kuunda bara la Amasia.
Bara kubwa
"Matokeo yetu yanaonyesha kuwa kupoza kwa eneo la katikati ya dunia, nguvu ya jumla ya bahari inakuwa dhaifu, na Bahari ya Pasifiki itasinyaa vya kutosha na kuwa bahari ndogo kuliko Bahari ya Atlantiki na Hindi inayopanuka," anasema mwandishi mkuu wa utafiti, Chuan Huang , wa Kikundi cha Utafiti cha Curtin's Earth Dynamics na Shule ya Dunia na Sayansi ya Sayari.
Jina "Amasia" linatokana na imani kwamba Marekani itagongana na Asia.
Bara kuu la mwisho, linalojulikana kama Pangaea, liligawanyika kuwa mabara yapata miaka milioni 180 iliyopita.
Iilijumuisha karibu ardhi zote za Dunia na lilizungukwa na bahari ya kimataifa inayoitwa Panthalassa.
Kwa makadirio haya ya hivi karibuni, watafiti walitumia kompyuta kuu kuiga jinsi mabara makubwa yanavyoundwa.
Mifano ya kompyuta inaonyesha kuwa bahari ya Pasifiki tayari inapungua kwa sentimita chache kila mwaka.
Huang anatabiri kwamba Australia kwanza itagongana na Asia na hatimaye kuungana na Marekani baada ya Bahari ya Pasifiki kutoweka.
Matukio mengine
Katika siku za nyuma, watafiti wametabiri matukio matatu tofauti pamoja na Amasia: Novopangea, Pangea Ultima, na Aurica.
Utafiti huu unatia shaka juu ya uwezekano wa matukio mengine.
"Uhakika wa 100% ni maneno yenye nguvu sana ambayo hayatumiki sana katika sayansi, haswa tunapozungumza juu ya mwelekeo wa mabadiliko ya Mfumo tata wa Dunia ambao ndio tunaanza kuuelewa kwa ujumla," anaelezea Zheng-Xiang Li, mshiriki wa utafiti na mwandishi.
"Mitindo yote tofauti ambayo unaweza kuwa umesoma juu (pamoja na kazi yetu) ni dhana tu na utabiri wetu unategemea matokeo ya mfano wetu, ambayo kwa upande wake yanategemea maarifa yetu ya sasa na mawazo kadhaa (kama vile kazi zote za aina hii)".
Dunia inakadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.5.
Katika mzunguko wa kijiolojia wa Dunia, kusogea na kuvunjika kwa mabara hutokea mara kwa mara.
Ni harakati za sahani za tectonic chini ya bahari ambazo husogeza mabara.
"Tulibuni mfumo wa duara unaofanana na Dunia kwa kutumia kompyuta kuu, kuiga miundo ya ndani, sifa na michakato ya Dunia, kama vile tectonics za sahani na upitishaji wa vazi.
Kisha tukaendesha mfululizo wa mifano ili kuona ni sababu gani (s) zinaweza kudhibiti jinsi bara kuu linaundwa, "Li anasema.
Kusogea kwa chini ya bahari
Toleo la modeli lilifichua kwamba nguvu ya lithosphere ya bahari (ya ~ kilomita 100 ya tabaka dhabiti au bamba la tectonic chini ya bahari) inatoa ushawishi mkubwa zaidi juu ya jinsi bara kuu linaundwa.
Dunia inapopoteza joto lake la ndani polepole kwa mabilioni ya miaka, unene wa kilomita 7-8 wa sakafu ya bahari unaonekana kuwa mwembamba baada ya muda kutokana na kuyeyuka kidogo .
"Matokeo yetu ya kielelezo yanatabiri kwamba bara kuu la Amasia la siku zijazo lingeweza tu kuundwa kwa kufunga Bahari ya Pasifiki."
Uundaji na mgawanyiko wa bara kuu daima umekuwa na athari kubwa kwa hali ya hewa na mazingira.
Kwa ujumla, kundwa kwa bara kuu kungesababisha viwango vya chini vya bahari, kupungua kwa bayoanuwai, na sehemu kubwa ya ardhi kame katika eneo kubwa la ndani la bara hilo.
Kinyume chake, wakati wa kuvunjika kwa bara kuu, viwango vya bahari vingeongezeka, bioanuwai ingeboreka, na kungekuwa na rafu nyingi zaidi za kutegemeza maisha ya bara hilo.
"Ni ngumu kutabiri jinsi mwanadamu atakavyoonekana mamia ya mamilioni ya miaka kutoka sasa, lakini kama sehemu ya ulimwengu, mwanadamu angeendelea kubadilika kama maisha yamekuwa yakifanya kila wakati," Li anasema.
"Nina imani kuwa akili zetu za hali ya juu na uwezo wetu wa kiufundi utaturuhusu kuzoea mabadiliko ya siku zijazo kama tulivyokuwa huko nyuma."