Mtu aliyevumbua umeme: Jinsi Nikola Tesla alivyofanya maisha yetu kuwa rahisi

Nikola Tesla with an early Tesla coil

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

"Namuona Tesla sio tu kama baba wa umeme au mawasiliano duniani," mwanahistoria na mtengenezaji wa filamu Michael Krause anaiambia BBC.

"Alikuwa na mawazo ambayo yalikuwa kabla ya wakati wake - alikuwa mwenye maono ambaye alitoa mchango wake katika mageuzi ya wanadamu."

Lakini mwishoni mwa miaka ya 1890, Tesla alipokuwa akizunguka jukwaa katika Chuo cha Columbia cha New York akiwa ameshikilia mirija inayong'aa mikononi mwake ili kutambulisha transfoma yake mpya iliyovumbuliwa, dunia bado ilikuwa gizani.

"Umeme ulikuwa jambo la siku za usoni na watu wengi walilazimika kutembelea maeneo ambayo ulionyeshwa ili kuiona ikitekelezwa," mwanahistoria Iwan Rhys Morus anaeleza katika kitabu chake 'Nikola Tesla and electrical future'. Lakini hayo yalikuwa yabadilike hivi karibuni.

Taa angavu

Mvumbuzi Nikola Tesla (1856-1943) katika hotuba ya Paris

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mvumbuzi Nikola Tesla (1856-1943) katika hotuba ya Paris

Nikola Tesla alizaliwa mnamo 1856, katika Milki ya Hapsburg ya Austria (mji wake wa Smiljan sasa ni Croatia, ingawa familia yake ilikuwa ya Serbia), lakini angeondoka akiwa kijana kwenda kwenye taa angavu za jiji kuu la Ulimwengu Mpya.

Alipofika New York mnamo 1884, ilikuwa amfanyie akazi kwa mvumbuzi maarufu na mfanyabiashara Thomas Edison.

"Alitoka katika ulimwengu wa kale na akawa mmoja wa wahusika wakuu wa nyakati za kisasa," Krause alisema.

Alipokanyaga ardhi ya Marekani, mhandisi wa umeme na mitambo - na futurist - alikuwa na senti chache tu katika mifuko yake na hesabu ya mashine ya kuruka, kulingana na mwandishi mwingine wa wasifu, Inez Whitaker Hunt.

Lakini haikuwa mashine ya kuruka iliyomfanya Tesla kuwa maarufu. Kwa miaka mingi, alikuwa akikamilisha injini za sasa zinazobadilika.

Naye alifika Marekani kwa wakati ufaao kabisa, kama vile pambano kati ya aina mbalimbali za mkondo wa maji lilivyozua maishani.

Kueneza umeme duniani

Tesla akiwa ameketi katika maabara yake ya Colorado Springs na "Magnifying transmitter" mnamo 1899.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tesla akiwa ameketi katika maabara yake ya Colorado Springs na "Magnifying transmitter" mnamo 1899.

Dunia ilikuwa ikiendelea na ilihitaji nishati zaidi, kwa hiyo kulikuwa na mbio za kutafuta njia bora zaidi ya kuzalisha na kusafirisha umeme kwa mashine za nguvu na kuwasha taa.

"Kulikuwa na mifumo miwili shindani ya usambazaji wa umeme," Morus aliiambia BBC. Vita vilikuwa kati ya mfanyabiashara na mhandisi wa Marekani, George Westinghouse, na bosi wa Tesla Thomas Edison, kubaini kama mkondo wa kubadilisha (AC) au mkondo wa moja kwa moja (DC) utatumika kwa usambazaji wa umeme.

Kampuni ya Thomas Edison ilikuwa inawekeza katika nguvu ya umeme ya moja kwa moja, ambayo inapita tu katika mwelekeo mmoja na kwa umbali mfupi, kwa voltage moja.

Lakini mtiririko wa nguvu ya meme inaosambaa pande tofauti, unaweza kufikia umbali mrefu na kiwango (voltage) kinaweza kuongezwa au kupunguzwa. Kwa kuwa inaweza kusafiri zaidi, huleta nguvu kwa maeneo zaidi.

Makumbusho ya Nikola Tesla, Belgrade

Chanzo cha picha, Makumbusho ya Nikola Tesla, Belgrade

"Ni kama kulinganisha farasi na gari na kasi ya ndege," mwandishi wa wasifu wa Tesla Mark Cypher aliambia podcast ya historia ya Mashahidi wa BBC.

Tesla alipofika New York, tayari alikuwa na 'ndege aina ya jet' mfukoni mwake - alikuwa akifanya majaribio ya AC alipokuwa akifanya kazi huko Ulaya na alitengeneza injini yake ya kwanza mnamo 1883.

Lakini kama Edison alisisitiza juu ya uhamishaji wa moja kwa moja wa nguvu za umeme, wawili hao walitengana na hivi karibuni Westinghouse ilinunua haki miliki ya mfumo wa Tesla wa transfoma za kubadilisha- nguvu za nishati na magari.

Muundo wa Tesla uliweza kusambaza nishati kwa gharama nafuu kwa umbali mkubwa, na bado inatumika leo.

Tesla gwigi wa maonyesho

Sanamu ya Tesla katika kituo chake cha zamani cha utafiti katika jimbo la New York

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sanamu ya Tesla katika kituo chake cha zamani cha utafiti katika jimbo la New York
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Bado tunatumia umeme unaosambazwa kupitia mifumo tofauti, na mchakato wa uzalishaji na usafirishaji wa nishati ya umeme bado unategemea mawazo ya Tesla," Ivana Zoric, mtunzaji katika Jumba la Makumbusho la Nikola Tesla huko Belgrade, aliiambia BBC.

Hakika, mfumo wa Tesla bado ni njia inayoongoza kwa uzalishaji, maambukizi na usambazaji wa nishati ya umeme na vifaa vingi vya umeme vya leo hutegemea uvumbuzi wake mwingine.

"Vifaa vy akutumia nguvu ya umeme kwenye magari viliundwa kwa ubunifuwa hali ya juu sana na hadi wa leo bado zinatumika katika tasnia na katika vifaa vingi vya nyumbani - hata kwenye magari ya umeme," Zoric alisema.

Alivumbua coil ya Tesla, kifaa ambacho hutoa mikondo mizuri ya nishati ya umeme, mnamo 1891 katika jaribio la kusambaza umeme bila waya.

Pia bado inatumiwa leo katika redio na televisheni na vifaa vingine vya kielektroniki.

Miaka miwili baadaye, Tesla na Westinghouse walishinda ombi la kufanya Maonyesho ya Kimataifa ya Columbian huko Chicago wakisherehekea kumbukumbu ya miaka 400 ya uvumbuzi wa Ulaya na Marekani, na Tesla akawa nyota.

"Watu walipogundua ukubwa wa uvumbuzi huo, Tesla alipata kazi ya kujenga kiwanda cha kuzalisha umeme katika Maporomoko ya Niagara," Zoric alisema.

Ulikuwa mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme wa maji duniani na Tesla ilimiliki hati miliki 9 kati ya 13 zilizotumiwa kuijenga.

"Watu walijua Bwana Tesla alikuwa nani, na alitumia ujuzi huo kwa umahiri sana kuendeleza mambo mengine," Morus alisema.

Hivi karibuni alianzisha maabara yake mwenyewe na kuanza majaribio katika uwanja wa mawasiliano yasiyounganishwa kwa waya na nishati huru na anajinadi kama mtu ambaye atafanikisha ndoto hiyo siku zijazo.

Pia alifungua milango yake kwa umma, akionyesha uelewa wake mzuri wa maonyesho, kulingana na Morus.

Siku za usoni bila nyaya

Wakati ulimwengu ulitegemea kutuma ujumbe kwa kusambaza kwa waya, Tesla alianza kujaribu upitishaji wa mawimbi ya bila kutumia waya.

Lakini alihitaji ufadhili ili kufanya majaribio yake yote mapya. Na ufadhili huo aliweza kuupata mwanzoni mwa miaka ya 1890 kutoka kwa mfadhili wa Marekani J.P. Morgan, na akaanza kujenga mnara wake wa utangazaji wa dunia usiotumia waya katika Long Island.

Lengo lake kuu lilikuwa kufikisha mawasiliano kote duniani - mfumo usiotumia waya ambao ungewezesha mawasiliano ya papo hapo ya video na sauti ya kimataifa, ambapo habari zingepatikana kutoka kwa mtu yeyote, popote. Lakini baadaye Morgan aliondoa msaada wake.

"Kwa bahati mbaya, ndoto yake kubwa, mfumo wa kimataifa wa kuwapatia watu umeme na mifumo ya mawasiliano haikufanikiwa kwa sababu alikuwa hayupo au teknolojia haikuwepo," Klause alisema.

Tesla aliendelea kufanya kazi katika miradi mbalimbali, lakini mara nyingi hakuwa na fedha na mawazo yake mengi yalibakia tu katika maelezo yake, kwani alishindwa kuelewa kwamba sayansi na uhandisi ni mchakato wa ushirikiano mkubwa unaohusisha watu wengi.

"Tesla alifanya makosa makubwa. Kwa kweli alifikiri na ni yeye pekee ndiye angeweza kutengeneza siku zijazo za umeme.

Hakuwa na nia ya kushirikiana na kufanya kazi na mtu mwingine yeyote," alisema Morus.

Alipata umaarufu kama mtu asiye na msimamo, mtu aliyetawaliwa na hofu, ambaye uvumi wake kuhusu kuwasiliana na sayari nyingine ulikosolewa vikali.