Jinsi hashtags, nyimbo na vichekesho vilivyokoleza maandamano ya Iran

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa zaidi ya mwezi mmoja, maandamano yameikumba Iran huku wanawake na wasichana wa shule wakiwa mstari wa mbele, wengine wakichoma hijabu zao au kupeperusha hewani huku wakipiga kelele "Mwanamke, Maisha, Uhuru".
Maandamano haya yalichochewa na kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 22 wa Kikurdi alipokuwa chini ya ulinzi wa 'polisi wa maadili' kwa madai ya kuvaa hijab yake (hijabu) "isiyofaa".
Lakini mara tu watu wanapoondoka barabarani na kurejea kwa usalama wa nyumba zao, maandamano yanaendelea mtandaoni kwenye mitandao ya kijamii, si nchini Iran pekee bali duniani kote.
Tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, Wairani wengi wameikimbia nchi, wakihama kutoka pande zote za dunia na mitandao ya kijamii imekuwa mahali pao pa kukutana na kushirikishana hisia za kijumuiya.
Majukwaa kama Twitter, Instagram na TikTok pia yamechukua jukumu kubwa katika wimbi la sasa la maandamano, licha ya juhudi za serikali kuzima mtandao na kufunga majukwaa ya mitandao ya kijamii.
Ujumbe unaosambaa kwenye mtandao wa Twitter

Chanzo cha picha, Getty Images
Kupata hashtag kwenye mtandao wa Twitter imekuwa mojawapo ya njia kuu za Wairani kupaza sauti zao kote ulimwenguni. Baada ya kifo cha Mahsa Amini, hashtag maarufu iliyoandikwa #mahsaamini ilitumwa kwenye Twitter na kurudiwa kusambazwa zaidi ya mara milioni 252 kwa lugha ya Kifarsi na mara milioni 57 kwa lugha ya Kiingereza katika mwezi mmoja kati ya 12 Septemba na 12 Oktoba.
"Watu wanaambiwa mara kwa mara kuwa upinzani dhidi ya mfumo huu haupo au kama utafanya hivyo basi utakuwa mdogo na utakandamizwa," anasema mwanaharakati wa Haki za Wanawake wa Irani Negin Shiraghaiee.
"Hashtag zina jukumu muhimu kwa watu kutafutana na kutambua nguvu zao." Katika enzi ya vuguvugu zisizo na kiongozi, Shiraghaiee anasema 'hashtag' zinaweza kuchukua nafasi ya viongozi.
"Watu wanataka nini kutoka kwa 'hashtag'? Matumaini, mwongozo na habari," anasema. "Hivyo ndivyo hashtag zimefanya kwa waandamanaji hadi sasa." Lakini hashtag kwenye Twitter ni baadhi tu ya njia ambazo Wairani huzitumia kuwasiliana na kuufanya ulimwengu kutambua.
Maandamano kwenye mtandao wa Instagram

Chanzo cha picha, Foroozan
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika miongo minne iliyopita wasanii ndani ya Iran wamepata njia za busara za kukwepa udhibiti wa Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu. Foroozan ni mtengenezaji wa kidijitali anayeishi Los Angeles. Katika wiki za hivi karibuni, amekuwa akitumia sanaa yake kuunga mkono maandamano ndani ya Iran kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Moja ya kazi zake inaonyesha taswira ya mwanamke kijana aliyesimama mbele ya Sio-se-pol huko Isfahan na kukata mkia nywele zake ndefu. Ni kitendo ambacho kimekuwa moja ya alama za maandamano hayo na wanawake duniani kote wamekuwa wakinyoa nywele zao ili kuonyesha mshikamano na wanawake wa Iran.
"Katika kazi yangu napenda kufikiria jinsi wahusika na watu wangekuwa kama hawangedhibitiwa. Kipande hiki ni ndoto niliyonayo ... labda kitu ambacho kitakuwa ibada ya kila mwaka kwa wanawake kwa heshima ya Mahsa Amini," Foroozan aliiambia BBC.
Afra ni mpiga picha anayeishi San Francisco ambaye pia ametiwa moyo na maandamano hayo. "Nilipoenda kwenye maandamano ya kwanza ya 'mshikamano wa kimataifa na Wairani' hapa, wanawake wengi walikuwa wakikata nywele zao," aliniambia. "Baadaye nywele zao ziliachwa tu chini na nilifikiri tunapaswa kufanya kitu na nywele hizi zote. Kwa hiyo nilichukua nywele na kuunda ishara ya 'Mwanamke, Maisha, Uhuru.'
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Unity for Freedom ni video fupi iliyoundwa na msanii ndani ya Iran anayeitwa Benyamin ambayo imesambaa kwenye mitandao tofauti ya kijamii. Inaonyesha mkono wa kikosi cha usalama uliobeba rungu, na kupiga mikono mingine iliyo karibu. Mpaka walipomshinda, na inamalizikia kwa mkono huo wa kujiunga na mikono mingine kuonyesha ishara ya ushindi.
'FreeIranianWomen2022' ni akaunti ya Instagram inayosambaza video fupi, sanaa na vichekesho kuhusu maandamano. Katika video moja msanii anatengeneza upya noti za Rial na kubadilisha sura ya Ruhollah Khomeini kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 na picha za waandamanaji wanawake.
Serikali inajua umuhimu wa mitandao ya kijamii katika harakati za kisiasa na kijamii za Karne ya 21. Wakati maandamano yalipozuka serikali ilizima mtandao na kuzuia Instagram na Whatsapp, lakini watu bado wanatafuta njia za kuchapisha.
Shirika la Haki za Kibinadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway linadai kuwa takriban waandamanaji 201 wameuawa, 23 kati yao wakiwa watoto. Lakini hata katika nyakati za giza kama hizi Wairani wamejaribu kutumia ucheshi kujipoza roho zao.
Baada ya taarifa ya habari za jioni kwenye runinga ya serikali kudukuliwa watu walichukua sura ya mtangazaji wa TV, na kumdhihaki kwa kuingiza uso wake kwenye video za Snoop Dog na mchekeshaji Kevin Hart wakicheka kwenye kipindi chao cha mazungumzo.
Nyimbo zinazovuma na kusambaa

Chanzo cha picha, Getty Images
Hijabu ya lazima na kile waandamanaji wanaona kuwa ni uingiliaji wa mara kwa mara wa sheria za Kiislamu katika maisha ya kila siku yamekuwa yakilengwa na ukosoaji mwingi kwenye mitandao ya kijamii.
Mapema katika maandamano hayo, Wairani walienda kwenye Twitter na Instagram kueleza sababu zao za kuandamana kwa idadi kubwa ya tweets au machapisho yanayoanza na 'For the sake of', au 'Baraye' kwa Kiajemi.
Muziki wa pop wa Magharibi na muziki wa pop wa Irani uliotayarishwa nje ya Iran umepigwa marufuku nchini humo na kwa miongo kadhaa viongozi walikuwa wakisimama na kupekua magari - na hata kuvamia nyumba - kutafuta kile walichokiita 'muziki usio na heshima.'
"Kwa ajili ya wasichana wote ambao wanapaswa kuzika ndoto ya kuwahi kwenda shule ya music wa kitaaluma, kwa ajili yangu mwenyewe," Ferferity alitweet.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kucheza hadharani nchini Iran ni marufuku, isipokuwa baadhi ya ngoma za kitamaduni ambazo zinaweza kuchezwa na wanaume. Wanawake hawana haki ya kucheza au kuimba hadharani, ingawa madarasa ya ngoma ya wanawake pekee yapo.
Mnamo mwaka wa 2017, serikali ilipiga marufuku madarasa ya mazoezi ya Zumba katika ukumbi wa mazoezi uliotengwa kwa jinsia na kuyaita 'yasiyo ya Kiislamu'. "Kwa lugha yangu mama," ilikuwa tweet iliyochapishwa na mtumiaji RMshii94.
Katika kipindi cha miaka 43 iliyopita, makabila madogo yamepigwa marufuku kufundisha lugha zao mashuleni. Zara Mohammadi, mwalimu wa lugha ya Kikurdi, kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kufundisha lugha yake ya mama. Makumi ya maelfu ya tweets kama hizo na machapisho ya Instagram yamechapishwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Video aliyoichapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram ilitazamwa mara milioni 40 ndani ya saa 48 za kwanza zilipoisha. "Baraye..." imekuwa wimbo wa maandamano na imekuwa ikichezwa kwenye maandamano kote ulimwenguni.
Hajipour alikamatwa tarehe 29 Septemba na kuachiliwa kwa dhamana tarehe 4 Oktoba. Baada ya kuachiliwa, Hajipour aliandika kwenye Instagram akisema anajuta kuwa wimbo wake ulikuwa unatumiwa na vikundi vya kisiasa nje ya nchi kwa "madhumuni fulani".
Haijabainika ni katika hali gani alichapisha ubatilisho huu - kama ulilazimishwa au kwa hiari yake mwenyewe, na kama ulirekodiwa wakati wa kuwekwa kizuizini kwa Hajipour baada ya kuachiliwa kwake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa katika kuzidisha maandamano ya Iran, kwa kuwapa Wairani ndani na nje jukwaa la kueleza hisia zao na kuwaruhusu wengine kote duniani kufuata kile kinachoendelea nchini Iran.
Negin Shiraghaiee anaamini kwamba pia inaziba pengo muhimu. "Ndoto ya mapema ya watengenezaji wa mtandao ilikuwa kwa kila mtu kuwa na jukwaa," anasema. "Tunachokiona nchini Iran ni kwamba katika nchi ambayo watu hawana vyombo vya habari, mitandao ya kijamii imekuwa njia ya watu. Ni vyombo vya habari vilivyogatuliwa ambavyo vinaruhusu watu kusikika na kuonekana."















