Simulizi ya Mfalme wa Uingereza aliyeachia ufalme kwa ajili ya mapenzi
Na Walid Badran, BBC

Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe 14 Februari kila mwaka, mamilioni ya watu duniani kote husherehekea Siku ya Wapendanao.
Na siku hii ina jina "Valentine" ikihusisha mtakatifu aliye na jina hili ambaye anachukuliwa kuwa ndiye mlinzi wa wapenzi duniani. Februari 14 (tarehe ambayo aliuawa mnamo 269 BK) imechukuliwa kama sikukuu kwa wapenzi katika nchi nyingi kama sehemu ya kumbukumbu ya alichokifanya kuhusu mapenzi ama upendo.
Sherehe ya Siku ya Wapendanao ilianza kusheherekewa tangu katikati ya karne ya kumi na tisa, wakati wafanyabiashara wa Marekani walibadilisha utamaduni maarufu wa kidini kumkumbuka Mtakatifu Valentine kuwa tukio la kisasa.
Masimulizi mengi ya hivi karibuni yanayosambazwa sana yanaonyesha kwamba Valentine alikuwa kuhani au askofu aliyeishi Roma wakati wa karne ya tatu BK, na alikamatwa na Mfalme wa Kirumi wakati wa mateso ya kidini ya Ukristo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tovuti za Wakatoliki hupokea simulizi kulingana na ambayo uhalifu wa wapendanao ulikuwa ndoa ya wapenzi wa Kikristo, kinyume na maagizo ya Mfalme Claudius II, ambaye alikataza ndoa za hivyo kwa sababu aliamini kwamba ndiyo sababu ya kusita kwa vijana kutumikia jeshi.
Lakini Mtakatifu Valentine alisisitiza kwamba ndoa ni mojawapo ya sheria za Muumba duniani, na aliasi amri za Mfalme na kufanya ndoa za siri. Mfalme alipopata habari hiyo, alimfunga gerezani na kuamuru auawe.
Wakati wa kifungo cha Valentine, alipendana na binti wa jela. Na siku ya kunyongwa kwake, mnamo Februari 14, alimtumia barua ya upendo binti huyo iliyosainiwa "Kutoka kwa Valentine", ambayo ni ishara ambayo ulimwengu leo umeibeba na kujenga utamaduni wa wapenzi kupeana kadi.
Mwaka wa 1380, Chaucer, kwa heshima ya Richard II, Mfalme wa Uingereza, katika uchumba wake wa kwanza na Anne kutoka Ufalme wa Bohemia, alisema: "Siku ya Mtakatifu Valentine ... wakati kila ndege anakuja kutafuta mechi yenyewe, mwanzoni mwa chemchemi ya Kiingereza..... lilikuwa shairi na Wasomaji wa shairi hilo walidhani kimakosa kwamba Chaucer alikuwa akirejelea tarehe 14 Februari kama Siku ya Wapendanao.
Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa hapakuwa na uhusiano wowote kati ya Mtakatifu Valentine na mapenzi ya kimahaba, kabla ya marejeleo ya Chaucer.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kuchapishwa kwa shairi lake, watu walianza kutumiana barua za mapenzi, mnamo Februari 14, na Mtakatifu Valentine, ambaye alikua mtetezi wa mapenzi ama upendo, alitangaza malalamiko yake juu ya mateso juu ya upendo na kujitenga kwa wapendanao.
Kufikia karne ya kumi na tisa, wapenzi walikuwa wameachana na kuandikiana barua zilizoandikwa kwa mkono hadi kubadilishana kadi zilizosheheni mashairi ya mapenzi, yaliyochochewa na alama za Kirumi kuonyesha upendo na uzuri katika simulizi za Kirumi, na ishara zingine.
Na desturi ya kubadilishana kadi za salamu ilienea hadi Marekani.
Edward wa VIII alikuwa nani hasa?
Jina lake kamili ni Edward Albert Christian George Andrew Patrick David, na alizaliwa mnamo Juni 23, 1894, Richmond, huko Surrey, Uingereza, na alikufa mnamo Mei 28, 1972, huko Paris, Ufaransa.
Alikuwa Mwanamfalme wa Wales kuanzia 1911 hadi 1936, na Mfalme wa Uingereza kuanzia Januari 20 hadi Desemba 10, 1936, alipojiuzulu ili kufunga ndoa na mtalaka wa Marekani Wallis Simpson.
Alikuwa mfalme pekee wa Uingereza kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe

Chanzo cha picha, Getty Images
Baba yake, Mfalme George V alifariki mnamo Januari 20, 1936, na Edward akatangazwa mfalme.
Baada ya kifo cha George V, mfalme huyo mpya alikutana na tatizo kubwa.
Na tatizo hilo lilihusiana na upendo wake kwa Wallis Simpson, kwani yeye, kama mfalme hakupaswa kuoa mwanamke aliyeachika, hivyo ilimbidi kuchagua kati ya nchi yake na upendo wake.
Akiwa mfalme, mnamo Novemba Edward VIII alifungua Bunge na kisha akazuru Wales kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri Mkuu wa wakati huo, Stanley Baldwin, alijaribu kumshawishi Mfalme juu ya hatari kwa uadilifu wa kifalme kwa sababu ya urafiki wake maalum na Simpson au mapenzi yake kwa mwanamke huyo.
Suala hilo likaanikwa kwenye vyombo vya habari na kuzungumzwa bungeni tarehe 3 Desemba, na siku iliyofuata habari ya Mfamle kuachia kiti cha enzi zililionekana kwenye magazeti kwa mara ya kwanza.
Kwa hivyo mfalme alifanya uamuzi wake wa mwisho na akajiuzulu mnamo Desemba 10, 1936.
Kuachia ngazi huko kuliidhinishwa na Bunge mnamo Desemba 11 mwaka huo.
Mnamo Juni 3, 1937, Edward na Wallis walifunga ndoa, kwa baraka ya kasisi wa Kanisa la Uingereza, huko Château de Candy, Ufaransa.














