Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi yafanya mashambulizi makubwa Ukraine kote leo, ikiutaka mji wa Bakhmut
Urusi imeipiga Ukraine kwa mashambulio mengi ya makombora siku ya Alhamisi wakati wanajeshi wake wakitaka kusonga mbele kuelekea mashariki, Kyiv alisema, huku washirika wa Magharibi wakiahidi kuongeza misaada ya kijeshi kwa ajili ya mashambulizi yaliyokusudiwa dhidi ya Ukraine.
Kufuatia mtindo wa mashambulizi makubwa ya mabomu katika uwanja wa vita Ukraine, Urusi ilirusha makombora 32 mapema leo, Jeshi la Anga la Ukraine lilisema.
Nusu ya makombora hayo yalidunguliwa.
Miongoni mwao, ni makombora manane ya Kalibr yaliyorushwa kutoka kwa meli katika Bahari Nyeusi, maafisa wa Ukraine walisema.
Makombora mengine yalipiga kaskazini na magharibi mwa Ukraine pamoja na maeneo ya kati ya Dnipropetrovsk na Kirovohrad.
Kwa kawaida Urusi imekuwa ikifanya mashambulizi yake mazito zaidi nyakati za mchana, ikilenga vituo vya nishati. Lakini maafisa wa Ukraine walisema shambulio hilo la usiku, moja halikuwa na athari kubwa kwenye ye nishati ya umeme.
Ukraine inaamini kuwa Moscow imefanya marekibisho ya mkakati, ikiwa ni pamoja na kutumia maputo ya hewa kufanya uchunguzi.
"Warusi wamebadilisha mbinu zao kwa kiasi fulani. Wanafanya uchunguzi wa kina, wanatumia malengo ya uwongo," Andriy Yermak, mkuu wa wafanyakazi wa rais wa Ukrain, aliandika kwenye programu ya ujumbe wa Telegram.
Ukraine haikusema kwa nini makombora machache yalirushwa kuliko kawaida lakini hapo awali imeripoti viwango vya chini vya ufanisi wakati Urusi iliporusha makombora ya Kh-22 ya enzi za Soviet.
Ikiimarishwa na makumi ya maelfu ya askari wa akiba, Urusi imezidisha mashambulizi ya ardhini kote kusini na mashariki mwa Ukraine katika wiki za hivi karibuni, na mashambulizi makubwa mapya yanaonekana kujitokeza wakati kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wake wa Februari 24 ikakaribia.
Mzozo huo umeua makumi ya maelfu ya watu, ukisambaratisha miji ya Ukrain, ukiyumbisha uchumi wa dunia kama vile ulivyokuwa ukiimarika kutokana na janga la COVID, na kuwakimbiza mamilioni ya watu kutoka kwenye makazi yao.
Ikionyesha ukubwa wa maafa ya kibinadamu, Ujerumani ilisema watu milioni 1.1 waliwasili nchini humo kutoka Ukraine mwaka 2022, na kuzidi wimbi la wahamiaji ambalo halijawahi kushuhudiwa lililowahi kutokea katika miaka ya 2015-2016.
Urusi haikutoa maoni yake mara moja kuhusu mashambulio haya mapya ya usiku wa kuamkia leo, ingawa siku ya Jumatano ilikuwa ikipigia debe vikosi vya Ukraine kuondoka katika sehemu za mkoa wa mashariki wa Luhansk.
Mapambano kuwania Mji wa Bakhmut
Mikoa ya Luhansk na Donetsk inaunda Donbas, kitovu cha viwanda katika nchi Ukrainia, ambacho kwa sasa kinakaliwa na Urusi. Inataka udhibiti kamili wa Donbas na lengo lake la sasa ni kuzunguka na kuchukua mji mdogo wa Bakhmut huko Donetsk.
Kutekwa kwa Bakhmut kungeipa Urusi hatua ya kusonga mbele katika miji miwili mikubwa, Kramatorsk na Sloviansk magharibi zaidi katika Donetsk, ili kufufua kasi ya Moscow kabla ya maadhimisho ya Februari 24. Ukraine na washirika wake wanasema kuchukua Bakhmut itakuwa ushindi mkubwa kutokana na miezi ambayo imechukua na kile wanachodai ni hasara kubwa ya maisha wakati wa mawimbi ya mashambulio ya Urusi.
Huku Ukraine ikipiga kelele kutaka kwa haraka silaha nguvu vikiwemo vifaru na ndege za kivita, mataifa ya muungano wa NATO yanaongeza uzalishaji na kuahidi zaidi kusaidia.
Jeshi la Rais Volodymyr Zelenskiy limepokea msaada mkubwa, hasa kutoka Marekani ambayo imetoa zaidi ya dola bilioni 27.4 tangu mzozo huo uanze.