Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.12.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Atletico Madrid itakuwa tayari kumuuza Joao Felix kwa euro 100m (£86m) baada ya kumsajili fowadi huyo wa Ureno, 23, kwa euro 126m (£113m) mwaka wa 2019. (AS – In Spanish ).
Manchester United wana nia, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain na Bayern Munich katika jitihada za kumnunua Felix mwezi Januari. (Mail)
PSG pia itampa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, nyongeza ya kandarasi rasmi baada ya Kombe la Dunia. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Al Hilal wanataka kuwashinda wapinzani wao wa Saudia Al-Nassr katika kumsajili Cristiano Ronaldo, 37, baada ya mshambuliaji huyo wa Ureno kuondoka Manchester United. (Express)
Chelsea inasalia kwenye mazungumzo na RB Leipzig kuhusu kumsajili Josko Gvardiol na beki huyo wa Croatia, 20, amesema "labda siku moja nitakuwepo". (Atheletic via 90 min)
Atletico Madrid wamefanya uchunguzi kuhusu kiungo wa kati wa Leicester Uturuki Caglar Soyuncu, 26. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurugenzi mtendaji wa Borussia Dortmund Carsten Cramer anasema wana "uhusiano mzuri" na kocha wa zamani na meneja wa sasa wa Liverpool Jurgen Klopp, lakini Reds hawatapata "zawadi" yoyote kama wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka klabu ya Ujerumani. . (Vietnam News)
Kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 23, ameashiria kuwa anataka kuondoka West Ham, akisema anataka kushinda mataji na kucheza Ligi ya Mabingwa. (Guardian)
Nottingham Forest imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Brazil Gustavo Scarpa, 28, kutoka Palmeiras. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea inashindana na Newcastle United kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 18, kutoka Vasco da Gama. (90 min)
Mchezaji wa Barcelona aliyesajiliwa majira ya kiangazi Franck Kessie hajisikii vizuri katika klabu hiyo, ambaye anaweza kufikiria kumuuza kiungo huyo wa kati wa Ivory Coast, 25, kwa kitita cha euro 10m (£8.6m). (AS – In Spanish)
Barcelona wanavutiwa na Mbrazili Endrick, 16, lakini hawatawasilisha ombi la kumnunua fowadi huyo wa Palmeiras msimu huu. (Marca In Spanish )

Chanzo cha picha, ENDRICK 11on Twitter
Liverpool wamefanya mazungumzo ya kusitisha mkataba wa mkopo wa msimu mzima wa Billy Koumetio na Austria Vienna huku wakimpa muda mchache wa kucheza beki huyo wa kati wa Ufaransa, 20. (Football Insider)












