Uchunguzi wa BBC: Madaktari wa kigeni Uingereza 'wananyonywa' na kuhatarisha afya za wagonjwa

Madaktari walioajiriwa kutoka baadhi ya nchi maskini zaidi duniani kufanya kazi katika hospitali za Uingereza wanasema wananyonywa .
Madakatari hao wanaamini pia kuwa wanapewa kazi nyingi kupita kiasi wakihofia kuhatarisha zaidi afya za wagonjwa.
Uchunguzi wa BBC umepata ushahidi kwamba madaktari kutoka Nigeria wanaajiriwa na kampuni ya afya ya Uingereza na wanatarajiwa kufanya kazi katika hospitali za binafsi chini ya masharti ambayo ni kinyume na utaratibu wa Mamlaka ya Huduma ya Kitaifa ya Afya (NHS)inavyotaka.
Jumuiya ya Madaktari ya Uingereza (BMA) imeelezea hali hiyo kama "ya kushtua" na inasema sekta hiyo inahitaji kufuata msingi na utaratibu wa utoajihuduma za afya chini ya NHS.
BBC imezungumza na madaktari kadhaa wa kigeni - ikiwa ni pamoja na daktari mdogo kutoka Nigeria ambaye alifanya kazi katika Hospitali binafsi ya Nuffield Health Leeds mwaka 2021.
Augustine Enekwechi anasema masaa yake ya kazi yalikuwa mengi kupita kiasi – unakua zamu kwa saa 24 kwa siku kwa wiki nzima - na haikupaswa kuondoka katika mazingira ya hospitali. Anasema kufanya kazi huko ni kama uko "gerezani".
Uchovu ulikuwa mkali sana, anasema, kuna nyakati alikuwa na wasiwasi asingeweza kufanya kazi ipasavyo.
Augustine si peke yake aliyekumbwa na tatizo hilo. BC imefanikiwa kupata dodoso la maswali kwa madaktari188 kutoka BMA na kundi la shawishi kutoka cha Chama cha Madaktari. Madaktari hao wengi waliajiriwa na NES lakini baadhi walikuwa na waajiri wengine.
Iligundua kuwa 92% walikuwa wameajiriwa kutoka Afrika na wengi - 81% - walikuwa kutoka Nigeria. Wengi walilalamikia saa nyingi za kazi na kukatwa mishahara isivyo haki.
Madaktari wanafikaje nchini Uingereza kufanya kazi?

BBC ilisafiri hadi Nigeria kushuhudia upande mwingine wa simulizi hii yenye kusumbua.
Katika jumba la kufanyia mitihani huko Lagos, jiji kubwa zaidi nchini humo, tulikuta mamia ya madaktari wakiwa kwenye foleni kufanya mtihani wa Bodi ya Tathmini ya Kitaalamu na Lugha - au PLAB 1.
Mtihani huo unaandaliwa na Baraza Kuu la Madaktari huko London na ni hatua ya kwanza inavyotakiwa na mamlaka ya matibabu ya Uingereza kupata leseni ya kufanya kazi nchini Uingereza.
Madaktari tuliozungumza nao walisema walivutiwa na kiwango kikuwa cha mishahara ya na mazingira bora ya kazi.
Tukio hilo lilikuwa likisimamiwa na wafanyakazi kutoka British Council - shirika linalofadhiliwa na Ofisi ya Mambo ya Nje.
GMC pia inafanya hivyo kwa nchi zingine kama Ghana, Sudan, Pakistan na Bangladesh.

Dk Femi Johnson alipelekwa kufanya kazi katika hospitali tofauti na Augustine, lakini anasema alitakiwa kufanya kazi masaa 14 hadi 16 kwa siku na kisha kuwa zamu kwa njia ya simu usiku kucha.
"Nilikuwa hoi," anasema. "Nilikuwa nimechoka, nilihitaji kulala. Haiwezekani kibinadamu kufanya hivyo kila siku kwa siku saba."
Lakini alipohitaji mapumziko kwa sababu alikuwa amechoka sana asingeweza kuendelea na kazi, NES ilikuwa na haki ya kumkata mshahara wake. Kampuni hiyo inasema hiyo ni kulipia gharama ya kupata daktari mbadala, lakini Femi anasema inawaacha madaktari wa NES katika hali mbaya sana na njia panda.

Baadhi ya madaktari wa NES wamekuwa wakisaidiwa na Dk Jenny Vaughan kutoka kwa Chama cha Madaktari. Anapokea malalamiko mengi kutoka kwa Maafisa wa Afya Wakaazi na anasema mfumo wa huduma ya afya wa Uingereza umekua katika ngazi mbili - moja kwa madaktari wa NHS, nyingine kwa waajiri wa kimataifa wanaofanya kazi katika sekta binafsi.
Madaktari wa NHS wanaweza tu kupangiwa kufanya kazi kwa saa 48, na wakiomba, hadi saa 72 kwa wiki.
"Hakuna daktari kutoka NHS anayefanya kazi zamu ya usiku kwa siku nne mfululizo kwa sababu tunajua kwamba si salama," anasema Dk Vaughan.
"Kazi hii ni aina ya kitumwa... (kufanya kazi ) masaa mengi, nilidhani (utumwa) umepita miaka 30 iliyopita.
"Haikubaliki kwa wagonjwa kwa sababu za usalama wa mgonjwa. Haikubaliki kwa madaktari."

Tulizungumza na na naibu mwenyekiti wa BMA, Emma Runswick. Alituambia kuhusu tulichogundua, akasema hali hiyo ni "aibu kwa sekta ya afya ya Uingereza".
"(Madaktari) wenzetu wa kimataifa wametoka mbali sana kuja Uingereza, na wamegundua kuwa hali ni ya kinyonyaji."
NES Healthcare ilituambia kwamba "maoni yetu kuhusu uzoefu wa madaktari" na kampuni yalikuwa "chanya sana".
Inasema kwa ujumla inawapa madaktari "njia salama katika kupitia sekta ya Huduma ya Kitaifa ya Afya, na katika mfumo wa huduma ya afya ya Uingereza, na kwamba kazi yao ni ya "faida kubwa kwa umma wa Uingereza."












