Helikopta ya Uingereza ya miaka 40 inayopeperushwa Ukraine

th
Maelezo ya picha, Rubani wa Ukraine Vasil anasema helikopta ya Sea King ni "nzuri sana"
Iliyochapishwa

Helikopta ya kijeshi iliyotolewa kwa Ukraine na serikali ya Uingereza ilitumiwa katika mzozo wa Falklands zaidi ya miaka 40 iliyopita, BBC imefahamu. Licha ya umri wake, jeshi la Ukraine linasema ndege hiyo itasaidia katika vita dhidi ya Urusi.

Ikiruka chini angani juu ya kusini mwa Ukraine, helikopta hiyo inaruka na kugeuka, ikifuata mkondo wa ardhi. Kutoka kwa chumba cha marubani na mlango wa upande mmoja uliofunguliwa, wahudumu wanakagua sehemu zote za ardhini kwa umbali kugundua hatari yoyote inayoweza kutokea .

Tuko ndani ya mojawapo ya helikopta mbili za Sea King ambazo Uingereza imeipa Ukraine - Mara ya kwanza kwa chombo cha habari kuingia ndani tangu ziwasilishwe kwa Ukraine katika miezi ya hivi karibuni. Ndani, nyuso zina mkunjo hapa tishio la makombora ya Urusi haliko mbali.

Licha ya hayo, wafanyakazi wanne wanafurahia kuonyesha helikopta hiyo mpya. Wanatuambia jinsi ilivyo muhimu kwao kwenye uwanja wa vita, ambapo hutumiwa kuokoa majeruhi, kuwasafarisha askari, na kufanya uchunguzi.

Lakini kwa nini Uingereza inaipa Ukraine helikopta za zamani kama hizo, ambazo baadhi yake zimekuwa zikiruka kwa zaidi ya miongo minne?

Serikali ya Kyiv iliomba ndege za kisasa za kivita zilizo na makombora ya masafa marefu kusaidia katika mashambulizi mapya yaliyotarajiwa dhidi ya vikosi vya Urusi. Lakini Uingereza haijatoa ndege zake zozote za kivita za Typhoon kwa Ukraine - haina za ziada , na itachukua muda mrefu sana kuwafunza marubani wa Ukraine kuzitumia. Pia kuna hofu kubwa kwamba kutoa ndege za kivita kunaweza kuzidisha mzozo.

Badala yake, Uingereza iliamua kuwapa helikopta mbili ambazo hazibebi silaha yoyote au kuruka haraka sana, na ambazo hazitumiki tena na Jeshi la Wanamaji , ambalo lilistaafisha helikopta hizo za Sea King miaka kadhaa iliyopita. Moja ya ndege hizo ni ya kale sana na hata ilituiwa wakati wa mzozo wa Falklands, mnamo 1982, ambapo ilitekeleza huduma ya kihistoria .

Jibu la matumizi ya ndege hii pia linaweza kupatikana hapa nchini Ukraine. Wafanyakazi wana uchangamfu mkubwa kuhusu helikopta yao mpya. Rubani mwenza, Vasil, anasema Sea king ndio ndege ambayo Jeshi la Wanamaji la Ukraine lihitaji - ndege ya kweli na ya kutegemewa ambayo inaweza kufanya chochote

th
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Ninapenda helikopta hii kwa sababu ni nzuri sana kwa kuruka," Vasil anasema. "Ni mojawapo ya bora zaidi kwa operesheni za kivita, iwe ni kusafirisha vifaa au kufanya utafutaji na uokoaji. Ni rahisi kuruka hata katika mazingira magumu."

The Sea Kings zinatumiwa kuchukua majeruhi wanaohitaji usaidizi wa haraka wa matibabu, kuhamisha vikosi maalum katika uwanja wa vita, na kuchukua na kubeba vifaa.

Vasil anasema kazi moja kuu ni kutafuta marubani walioanguka, ambayo inaweza kuhusisha kuruka nyuma ya safu za adui. "Marubani wanapaswa kujiondoa," anasema. "Wanahitaji kuokolewa. Kwa hili, tunapaswa kufikia eneo ambalo pengine haliko chini ya udhibiti wa Ukraine."

Pia anasisitiza kwamba Sea Kings zina umri sawa na helikopta nyingine kadhaa zinazotumiwa na vikosi vya kijeshi vya Ukraine. Kwa hivyo, yeye na marubani wengine wanafahamu ndege za zamani, na kufanya mafunzo yao kuwa rahisi.

"Ni pana, ina uwezo mzuri wa kubeba mizigo ," Vasil anaongeza.

Jibu jingine kwa swali kuhusu umri wa ndege linaweza kupatikana, labda, katika kambi moja kusini mwa Uingereza, ambapo Sea King nyingine ya tatu , itakayobidhiwa Ukraine katika wiki zijazo, inatayarishwa. Hatuwezi kusema ni wapi kambi hiyo ipo kwa sababu za kiusalama, lakini tulizungumza na wahandisi wawili wa Kiukreni ambao wamekuwa hapo kwa muda wa miezi saba, kufanya mafunzo ya kuitengeneza na kuidumisha helikopta hiyo.

Mhandisi mmoja, Ihor, ananiambia kwamba Sea King kwa kweli ni ndege mpya ikiwa na sehemu chache sana na za ndege ya awali.

"Ni ndege kuu ," anasema, "lakini imeboreshwa , na tunaihitaji sana. Ninaamini huu ni mwanzo tu wa kazi yetu pamoja."

th

Ndege hizi zimetumia muda mwingi wa maisha yao kufanya shughuli za utafutaji na uokoaji - kwa raia na vile vile wanajeshi - na zimekuwa zikionekana mara kwa mara katika pwani ya Uingereza. Moja ya dnege hizo zilizo Ukraine ilipeperushwa na Ralph Wickes-Sneyd huko Falklands mnamo 1982 - alisimamia kikosi ambacho kilitumia ndege hizo. Rubani huyo mstaafu wa jeshi la wanamaji anasema helikopta hiyo ilitekeleza jukumu la kihistoria, kuruka kwenye dhoruba mnamo tarehe 14 Juni 1982 kumpeleka kamanda wa vikosi vya nchi kavu vya Uingereza - Jenerali Jeremy Moore - hadi Port Stanley ili aweze kukubali kujisalimisha kwa Argentina. Hakuna ndege nyingine ingeweza kuruka kutokana na hali mbaya ya hewa, anasema.

"Ilikuwa operesheni ya kipekee," Bw Wickes-Sneyd anaelezea. "Makubaliano ya kusistisha mapigano hayakuwa yametiwa saini hadi hatua hii, na kwa hivyo ndege ilikuwa ikiruka hadi Stanley ikishindana sio tu na hali ya hewa, lakini pia baadhi ya Waajentina ambao walikuwa maadui .

Rubani pia alifichua kwamba helikopta iliyopeperushwa wakati huo - ambayo sasa iko Ukraine - pia ilipeperushwa Falklands na Prince Andrew, wakati huo akihudumu kama rubani chipukizi wa majini.

"Aliipeperusha ndege hiyo mara kwa mara," Bw Wickes-Sneyd anasema. "Ilikuwa ni ziara yake ya kwanza. Kwa hiyo alifanya yale ambayo kila mtu alifanya, ambayo wakati mwingine yalikuwa ya kawaida sana, wakati mwingine ya kusisimua."

'Mwanzo tu'

Sea kings zinaweza kuwa ndege kuu na chache kuweza lkubadilisha hali ya vita Ukraine lakini jeshi la wanamaji nchini Ukraine linasema lina furaha kuwa nazo - na linataka zaidi.

th

Kuna helikopta nyingine za Sea King katika hifadhi nchini Uingereza, na ikiwa serikali itaamua kuzitoa kwa Ukraine, wafanyakazi na wahandisi tuliozungumza nao walisema watazipokea vizuri.

Rubani Vasil anasema kuwa kupata Sea King ni kama kubadilisha gari lako kuu na kuweka "gari la kigeni".

"Inatumika sana. Tungependa kupokea helikopta zaidi kama hizi," anasema.

Huko Uingereza, mhandisi Ihor anakubali ndege mpya labda ingekuwa bora, lakini anaongeza: "Ni bora kuliko kukosa chochote na ni mwanzo tu."