Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 02.03.2024
Kiungo wa kati wa Arsenal na Italia Jorginho, 32, anazivutia Juventus, Lazio na Napoli anapoingia miezi michache ya mwisho ya kandarasi yake. (Standard)
Mkurugenzi wa Michezo anayekuja wa Manchester United Dan Ashworth amekutana na aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Brighton Graham Potter huku shinikizo zikizidi kuongezeka kuhusu meneja Erik ten Hag. (Sun)
Liverpool watamlenga kocha wa Brighton Roberto de Zerbi iwapo watashindwa kumteua mkufunzi wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp anayeondoka. (Guardian)
Burnley wanatarajiwa kumbakisha Vincent Kompany kuwa kocha hata kama klabu hiyo itashushwa daraja kutoka kwa Ligi ya Premia msimu huu. (Football Insider)
Barcelona wamemtafuta kocha wa Ureno Roberto Martinez kuhusu kumrithi Xavi kama meneja wa klabu hiyo ya Uhispania mwishoni mwa msimu huu. ( Football Transfers)
Huenda Aston Villa ikalazimika kuuza wachezaji msimu huu wa joto ili kuepuka kukiuka kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Premia, huku Newcastle ikimtaka kiungo wa kati Mwingereza Jacob Ramsey, 22 na Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 25. (Mail).
Chelsea, West Ham, Juventus, AC Milan, Nice na Lyon wanavutiwa na mlinzi wa kushoto wa Gent Mwingereza Archie Brown, 21. (Standard)
AC Milan wanamfuatilia mlinda lango wa Arsenal na England Aaron Ramsdale, 25, kama mbadala wa mlinda lango wa Ufaransa Mike Maignan, 28. (Ekrem Konur)
Zinedine Zidane hana nia ya kuinoa England kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kukubali ofa yoyote kutoka kwa Manchester United ikiwa watachagua kuchukua nafasi ya Ten Hag. (The I)
Liverpool wana imani kuwa beki wa kushoto wa Scotland Andy Robertson, 29, atasalia katika klabu hiyo msimu huu wa joto licha ya Bayern Munich kumuhitaji. (Football Insider)
Fulham, Everton na Southampton wanamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Coventry City, 25, Callum O'Hare. (Sun)
Maskauti kutoka Tottenham na Borussia Dortmund wamekuwa wakimtazama mshambuliaji wa Cercle Brugge na Togo Kevin Denkey, 23. (Foot Mercato)
Chelsea wanajipanga kuajiri makocha maalumu licha ya meneja Mauricio Pochettino kupuuza wazo hilo mwezi mmoja uliopita. (Telegraph)