Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini unaweza kuamka usingizini na kushindwa kutembea?
Usingizi wa kupooza kumeleta picha fulani na hadithi za kutisha. Sasa wanasayansi wanaanza kuelewa kwa nini watu huamka kutokana na ndoto lakini hawawezi kutembea - na kwa nini wakati mwingine wanaweza kuendelea na njozi.
Nilikuwa mtoto mdogo wakati ilinipotokea kwa mara ya kwanza. Ilikuwa ni asubuhi na mapema, saa kadhaa kabla sijaamka kwenda shuleni.
Niliamka na kujaribu kujigeuza kitandani, lakini mwili wangu haukuniruhusu - sikuweza kufanya chochote, nikama nilikuwa nimepooza kuanzia juu hadi kwenye vidole vyangu vya miguu.
Ingawa ubongo wangu ulikuwa una fahamu, bado misuli yangu ilikuwa imepooza au imelala. Niliingiwa na hofu. Hatimaye, baada ya sekunde 15 hivi, kupooza kuliondoka na kuwa sawa.
Baadaye, nilipata jina la kile kilichonipata: Usingizi wa kupooza au kupooza usingizini. Ni hali ya kushangaza ya kawaida wakati wa usiku ambapo sehemu ya ubongo wako huamka huku mwili wako ukiwa umepooza kwa muda.
Baada ya tukio hilo la kwanza la kutisha, likawa jambo la mara kwa mara, na ikawa inanitokea kila baada ya siku mbili au tatu. Kadiri ilivyokuwa, ndivyo ilivyozidi kutisha. Hatimaye ilianza kunisumbua.
Lakini kupooza usingizini kunaweza kuathiri zaidi maisha. Na kwa wengine, inakuja na mambo ya kutisha. Mgonjwa mmoja mwenye umri wa miaka 24 niliyezungumza naye, ambaye aliomba kutambuliwa kwa jina moja tu la Victoria, anakumbuka ilitokea usiku mmoja alipokuwa na umri wa miaka 18. “Niliamka na sikuweza kuamka kutembea,” asema. "Niliona sura ya kutishain ikijificha nyuma ya pazia langu. Iliruka juu ya kifua changu. Na jambo la kutisha zaidi ni kwamba sikuweza kupiga mayowe. Ilikuwa hatari."
Wanasayansi wanadhani tatizo hili la kupooza mwili ukitoka usingizi linajitokeza zaidi na kwa muda mrefu kama unakua umelala. Mary Shelley inaonekana alitiwa moyo kuandika tukio huko Frankenstein kwa mchoro unaoonyesha kipindi cha kupooza singizini. Lakini hadi hivi karibuni imekuwa utafiti mdogo.
"Limekuwa jambo lililopuuzwa ... lakini katika miaka 10 iliyopita kumekuwa na hamasa inayoongezeka," anasema Baland Jalal, mtafiti wa masuala ya usingizi katika Chuo Kikuu cha Harvard ambaye mnamo 2020 alikamilisha utafiti ambao unaweza kuwa wa kwanza wa kliniki katika njia tofauti za kutibu ugonjwa wa kupooza.
Hadi hivi majuzi, haikuwa bayana ni watu wangapi wanaopata au kupitia ugonjwa huu wa kupooza usingizini.
Je ni tatizo lenye tiba?
Kupooza usingizini kunaweza kuwa ishara ama dalili za ugonjwa unaoitwa narcolepsy - ugonjwa ambao ubongo hauwezi kudhibiti mifumo ya kulala na kuamka, na kusababisha mtu kulala kwa nyakati zisizofaa.
Madaktari wanasema kupooza kuna uwezekano mkubwa wa kutokea wakati unakosa usingizi, kwa sababu usanifu wako wa usingizi umegawanyika. Wagonjwa wengine pia wanaona kuwa kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kuupata wakati ukiwa wamelala chali, ingawa maelezo ya hii hayajathibitishwa.
Njia ya kawaida ya kutibu tatizo hili ni elimu: wagonjwa wanafundishwa tu kuhusu sayansi iliyo nyuma ya hali hiyo, na kuhakikishiwa kuwa hawako katika hatari. Wakati mwingine kupata muda wa 'kutafakari' ni njia inayokubalika. Lengo ni kupunguza hofu ya mgonjwa wakati wa kwenda kulala, na kuwafundisha kuwa watulivu wakati wanapopatwa na hali ya kupooza wanapotoka usingizini.
Wakati mwingine hali ikiwa mbaya zaidi, dawa zinaweza kutumika - ikiwa ni pamoja naserotonin reuptake reuptake (SSRIs), ambazo kwa kawaida hutumiwa kutibu msongo wa mawazo lakini zina athari.
"Unapokuwa na wasiwasi na mfadhaiko, usanifu wako wa kulala hautakuwa sawa, kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupooza," anasema. "Acha tuseme bibi yako anakuambia, 'Kiumbe kinaonekana hivi, kinakuja usiku na kukushambulia'. Na kwa sababu ya hofu hii, [una] sisimkwa, vituo vya hofu vya ubongo wako vinadaka hilo'.
"Inaonekana ni jambo la mazoea linaloweza kutengeneza athari hii ya kushangaza."