Kombe la Dunia 2026: Kwa nini kipigo cha England kimezidisha maumivu ya kusubiri kwa miaka 60?

Jude Bellingham looks dejected after England's World Cup semi-final defeat by Argentina in Atlanta

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jude Bellingham na wenzake wa timu ya taifa ya England walionekana kuvunjika moyo baada ya kipenga cha mwisho kupigwa
    • Author, Phil McNulty
    • Nafasi, Chief football writer in Atlanta
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Miaka ya kusubiri kwa England sasa itazidi 60, lakini kuadhibiwa kwao mwishoni na kufungwa na Argentina katika nusu fainali ya Kombe la Dunia huenda ndiko kulikoumiza zaidi kuliko yote.

Saa ndani ya Uwanja wa Atlanta ilionyesha kuwa England walikuwa wamebakisha dakika tano tu za muda wa kawaida kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kwa wanaume kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966, walipotwaa Kombe la Jules Rimet katika Uwanja wa Wembley.

Wachezaji wa England pamoja na kocha mkuu Thomas Tuchel walikuwa karibu kuandika historia walipoongoza kupitia bao la Anthony Gordon katika dakika ya 55.

Hata hivyo, matumaini yao yalianza kufifia kutokana na maamuzi mabovu ya Tuchel yaliyosababisha Argentina kuanzisha mashambulizi ya mfululizo yaliyoongozwa na Lionel Messi.

Bao la kusawazisha lilionekana kuwa suala la muda tu, na hatimaye Enzo Fernandez akafunga katika dakika ya 85.

Kisha, wakati England wakiwa wameyumba, Lautaro Martinez aliwazamisha kabisa kwa bao la kichwa katika muda wa majeruhi.

England hawakuweza kurejea mchezoni, hivyo taifa lililokuwa na matumaini makubwa linaamka likikabiliwa na maumivu ya karibu kufanikiwa tena kutoka kwa timu hii ambayo imeendelea kubaki karibu na mafanikio bila kuyafikia.

Tuchel ashindwa kuipa England ushindi

England head coach Thomas Tuchel on the touchline during the World Cup semi-final loss to Argentina

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa England Thomas Tuchel, anatarajiwa kuiongoza timu hiyo katika Euro 2028.

Sifa kuu iliyomtofautisha Thomas Tuchel alipomrithi Sir Gareth Southgate ilikuwa imani kwamba angeweza kushinda mechi ambazo mtangulizi wake alishindwa kushinda.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Southgate alikosolewa vikali aliposhindwa katika fainali mbili zilizopita za Euro dhidi ya Italia na Hispania, pamoja na nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2018 dhidi ya Croatia.

Maono yalikuwa kwamba Tuchel angeisaidia England kutwaa ushindi, ilhali Southgate alidaiwa kushindwa kufanya hivyo.

Shinikizo lilipozidi Tuchel alifanya kile kilichoonekana kama mbinu ya kujihami kupita kiasi na hatimaye akapoteza mechi hiyo jambo ambalo Southgate angekosolewa vikali kama lingetokea.

Sasa Tuchel anakabiliwa na lawama kwa uamuzi huo, na kwa wengi, lawama hizo ni sahihi.

Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) lilimteua Tuchel baada ya Euro ya mwaka wa 2024 kama suluhisho la haraka baada ya kuondoka kwa Southgate.

Walimleta kocha mwenye rekodi ya mafanikio, akiwa na jukumu moja tu, kuipa England ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka wa 2026.

Kufika nusu fainali pekee kunaweza kuonekana kwa mtazamo tofauti kama kushindwa kufikia matarajio, kwani aliajiriwa ili kuhakikisha England haikaribii kufanikiwa bali inafanikiwa.

Na kama ilivyokuwa kwa Southgate, Tuchel bado hajaiongoza England kushinda dhidi ya timu ambayo wengi hawakutarajia ingewacharaza.

Je, hiki kilikuwa kipigo chenye maumivu makubwa zaidi kwa England?

England wamepitia maumivu mengi kwa miaka mingi, lakini kwa mtazamo wa mwandishi aliyefuatilia Kombe la Dunia la saba, pamoja na fainali walizopoteza za Euro, hiki kilionekana kuwa kipigo chenye maumivu makubwa zaidi.

Si kwa sababu tu walifungwa na wapinzani wao wa jadi, Argentina, ambao historia yao na kumbukumbu zao za kipekee huibua hisia kali kwa wachezaji na mashabiki wa England.

Bali ni kwa sababu nusu fainali hii ya Kombe la Dunia itaendelea kukumbukwa kwa maswali mengi ya "ingekuwaje kama..." dhidi ya Argentina ambao wameonekana kushindwa katika mashindano haya, lakini wameendelea kukataa kushindwa.

Hii ilikuwa nusu fainali ya Kombe la Dunia, nafasi nyingine kubwa kwa England kupigania taji kubwa zaidi la soka duniani katika fainali iliyopangwa kufanyika New Jersey Jumapili.

England walikuwa zimebakisha dakika chache tu kuvuka kizingiti ambacho kimewashinda kwa zaidi ya miongo sita, lakini wakateleza tena.

Bao la Gordon lilionekana kuipa England udhibiti wa mchezo uliokuwa na ushindani mkali. Hata baada ya kupoteza umiliki wa mpira na udhibiti wa mchezo, walikuwa karibu kabisa na ushindi kabla ya kuporomoka mwishoni.

Kwa kuzingatia ukubwa wa mechi hiyo, hiki ni kipigo kitakachochambuliwa kwa kina zaidi kuliko vingine, na kuacha majuto makubwa kuliko vyote.

Sir Gareth Southgate after England's Euro 2024 final loss to Spain in Berlin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, England walipata kipigo cha pili mfululizo katika fainali za Euro chini ya kocha Sir Gareth Southgate mjini Berlin miaka miwili iliyopita.

England imejifunza nini kutoka kwa Kombe la Dunia?

England itabaki na kumbukumbu ya Uwanja wa Azteca jijini Mexico City, walipoonyesha umahiri wao kwa kuwafunga wenyeji Mexico mabao 3-2 katika hatua ya 16 bora.

Huo ulikuwa mmoja wa ushindi wao mkubwa katika historia ya Kombe la Dunia, ambapo Jude Bellingham alithibitisha uwezo wake wa kuchezea viwango vya dunia.

Aidha, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Thomas Tuchel pamoja na mbinu zake za kucheza zilionyesha kwamba ana mikakati ya kuisaidia England kutwaa ushindi.

Bellingham anaungana na Harry Kane katika kundi la wachezaji wa viwango vya juu. Hata hivyo, huenda ikawa kombe la dunia la mwisho kwake kushiriki kwani mshambuliaji huyo wa Bayern Munich atakuwa na umri wa miaka 36 ifikapo Kombe la Dunia msimu ujao.

Ila walivyopokea kipigo kizito kutoka kwa Argentina katika mchezo huu, imewaacha England na mashabiki wake wakijiuliza iwapo mkosi wao wa kushindwa kufanikiwa katika mashindano makubwa utawahi kuisha.

England italazimika kujipanga upya na kwa haraka, kwani mwezi Septemba itakuwa na mechi ya Ligi ya Mataifa ya UEFA dhidi ya Hispania, ambayo ilifika fainali ya Kombe la Dunia na pia iliifunga England katika fainali ya Euro 2024.