Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Garnacho akataa kuhamia klabu ya Al Nassr
Winga wa Manchester United Alejandro Garnacho amekataa kuhamia klabu ya Al Nassr, ya Saudia huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 akipendelea kuhamia Ulaya. (Telegraph)
Bayern Munich inatarajiwa kuelekeza mawazo yake kwa mshambuliaji wa Arsenal na Ubelgiji Leandro Trossard, 30, ikiwa haitafanikiwa kumsajili winga wa Liverpool Luis Diaz, 28. (Bild - kwa Kijerumani)
Mshambuliaji wa Brighton Evan Ferguson amekubali kuhamia Roma, huku klabu hiyo ya Italia ikiwa kwenye majadiliano kuhusu ada ya mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 20. (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano)
West Ham imekubali mkataba wa kumsaini beki wa Senegal Slavia Prague, 20 El Hadji Malick Diouf. (Footmercato - kwa Kifaransa)
Nottingham Forest itakabiliana na ushindani kutoka kwa vilabu vya Ulaya kumsajili winga wa PSV Johan Bakayoko. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ndiye alikuwa chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Anthony Elanga ambaye alisajiliwa na Newcastle wiki iliyopita. (Nottinghamshire Live)
Mawakala wa mshambuliaji wa RB Leipzig Benjamin Sesko, 22, wamewasiliana na Liverpool ili kutathmini nia yao ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia kufuatia uamuzi wa Arsenal kuelekeza nguvu zao kwa usajili wa Viktor Gyokeres wa Sporting Lisbon. (TBR Football)
Manchester United bado inamsaka mlinda lango lakini kipaumbele ya klabu hiyo ni kuimarisha kikosi chake, huku mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana, 29, akitarajiwa kuendelea kushikilia nafasi yake kama chaguo la kwanza. (i paper)
Everton imeungana na Roma katika mbio za kumsajili Neil El Aynaoui wa RC Lens licha ya kiungo huyo wa kati wa Morocco mwenye umri wa miaka 24 kufikia makubaliano ya awali na klabu hiyo ya Serie A. (Teamtalk)
Kipa wa Brest Marco Bizot, 34, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Aston Villa na atasafiri hadi Uingereza kukamilisha mchakato huo. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Rangers iko mbioni kumsajili winga wa Crystal Palace Jesurun Rak-Sakyi, 22, kwa mkopo lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu kadhaa. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi