Jinsi maputo yalivyotumika kwa ujasusi wa kijeshi kwa karne nyingi

Iliyochapishwa

Na Frank Ledwidge, The Conversation*

Mojawapo ya vita vya Afghanistan vya hivi majuzi ni puto zilizofungwa (pia zinajulikana kama "aerostats") zikielea juu kwenye kambi za vikosi vya kimataifa.

"Mifumo hii inaweza kugundua tishio kutoka kwa adui" ilikuwa na seti ya kamera za digrii 360 ambazo zilikuwa na uwezo wa kuona kila kona - kwa umbali wa hadi kilomita 160 - wa maeneo yanayozunguka.Na timu za ulinzi za Marekani ziliweza kuona kupitia vifaa vyenye ulinzi mkali.

Sakata la hivi majuzi kuhusu maputo anayodaiwa kuwa ya kijasusi kutoka China kuchunguza siri za nyuklia za Marekani ni ukumbusho kwamba teknolojia za zamani bado zinatengenezwa kwa ajili kuleta ya athari za kijeshi leo.

Puto zimekuwa zikitumika kwa huduma za kijeshi kwa muda mrefu zaidi hata kabla ya jeshi la anga kuwepo. Alikuwa ni mhandisi Mfaransa mahiri Jean-Marie-Joseph Coutell (mwanzilishi wa Kikosi cha Anga cha Ufaransa) ambaye alikuwa wa kwanza kuonesha uwezekano wa kutumia puto kutazama misimamo ya adui.

Mnamo Juni 1794, Coutell kwenye Vita vya Fleurus (Ubelgiji ya sasa) alitumia puto na kuripoti namna vikosi vya Austria vilivyojipanga, na kutuma ujumbe zinazoelezea mienendo na misimamo ya vikosi hivyo kutoka kwa puto lake, huku maadui waliokuwa na bunduki, kwa kiasi fulani wakishangaa, na walijaribu kumtandika risasi bila mafanikio.

Matumizi yake yalipunguzwa katika Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Amerika na Vita vya Franco-Prussia. Lakini katika Vita vya Kwanza vya Kidunia, aerostats zilichukua nafasi zaidi. Ndege, maarufu kama Zeppelins - zilikuwa na jukumu la muda mfupi la kulipua.

Walakini, jukumu la maputo kwenye uwanja wa vita lilikuwa na matokeo ya haraka zaidi.

Yalitumika kama jukwaa madhubuti kuhusu uwanja wa vita ukoje ambapo yaliweza kuchunguza misimamo ya adui na kuelekeza milio ya risasi dhidi yao.

Kikwazo, bila shaka, ni kwamba adui aliweza kuyaonea kwa urahisi na adui. Hakukuwa na jitihada zozote za kuyaangusha, kwa hiyo kuwa kwenye vikosi vya maputo ilikuwa jambo hatari sana.

Wakati wa Vita vya pili vya dunia

Ukubwa na utunzaji duni wa maputo ikilinganishwa na ndege za kijeshi, zilizifanya pendekezo lisilowezekana kama majukwaa ya uchunguzi katika Vita vya pili vya dunia.

Hata hivyo, yalitoa huduma muhimu, katika ulinzi wa anga, na kutengeneza "vizuizi" visivyo na rubani, hasa nchini Uingereza, ambako walipeleka msputo hayo kwenye miji na maeneo muhimu lengwa.

Nyaya zilizofungwa na kuning'nia chini zilikuwa hatari kwa ndege iliyokuwa ikiruka chini chini, ambapo ililazimika kuruka juu a maputo kuyazunguka. Maputo haya yalikuwa maarufu kwenye tukio la Blitz, mlipuko ambao nchi hiyo ilikumbana nao wakati wa Vita vya pili vya dunia mikononi mwa Jeshi la Nazi.

Hayakuleta matunda sana kwene jaribio la Japani la kutia hofu kwa wakazi wa Marekani kwa kutuma maelfu ya mabomu yaliyopeperushwa na maputo (yajulikanayo kwa Kijapani kama "Fu-Go") kwenye bara la Amerika.

Watu sita walikufa huko Oregon, waathirika pekee wa hatua hii ya adui katika bara la Amerika wakati wa mzozo huo.

Matumizi makubwa yaliyofuata ya kijeshi ya maputo yalikuja wakati wa Vita baridi, kupitia mpango wa Amerika ulioitwa "Moby Dick" ulisababisha mamia ya maputo kutumwa kupeleleza Muungano wa Sovieti.

Ni ya kawaida lakini yenye ufanisi

Maputo hayo yanaweza kuonekana kuwa kama dhana zisizotarajiwa kwa upelelezi wa mbali kama ule ambao China inadaiwa kuwa ilijaribu hivi majuzi kwa Marekani.

Yanaweza tu kuongozwa kwa kubadilishwa uelekeo, kwa kutumia mikondo ya hewa inayobadilika kubadilisha muelekeo.

Wiki iliyopita, matumizi yaliyopangwa kwa ustadi wa mikondo ya hewa ilielekeza puto la uchunguzi juu ya eneo nyeti zaidi la jeshi la Marekani: kambi za kombora za balestiki za Montana.

Idara ya Ulinzi ya Marekani ilisema kwamba "kesi za aina hii ya shughuli za maputo zimezingatiwa katika miaka ya hivi karibuni."

China inaripotiwa kukanusha kuwa puto hilo lilifanya shughuli za uchunguzi, na inashikilia kwamba ilikuwa ikikusanya data za hali ya hewa na ilikuwa imepoteza uelekeo kutoka kwenye njia yake.