Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi biashara za Urusi zinavyogharamika kutokana na usajili wa wanajeshi wa ziada
Usajili wa wanajeshi wa ziada nchini Urusi ulileta pigo kubwa katika biashara.
Wajasiriamali wanapoteza wafanyakazi, makampuni yanasimamisha michakato ya kazi, na wakati mwingine yanalazimika kufunga.
Idhaa ya BBC Urusi ilizungumza na wawakilishi wa biashara ndogo na za kati kuhusu jinsi usajili wa wanajeshi wa ziada nchini Urusi umeathiri kazi zao.
Alexey Goryachev, mwanzilishi wa kampuni ya samaki ya Moto Samaki, alielezea changamoto wanazopitia katika mtandao wa Facebook mapema mwezi Oktoba akisema mfanyabiashara anajiweka kama kisiasa.
“Nje ya siasa ni wakati unashughulika na mchakato wa biashara ili kusiwe na wakati wa gumzo lisiloisha,”alielezea katika moja ya machapisho.
Hata hivyo, katika maoni na kwenye baadhi ya machapisho yake ni wazi kwamba bado ana msimamo wa kisiasa.
Kwa mfano, mnamo Agosti, Goryachev alichapisha chapisho akisema kwamba maisha yanaendelea, aliandika Mimi *** (temeni) vikwazo vyenu.’’
Katika wiki za hivi karibuni, machapisho ya Goryachev, ambayo yeye huchapisha kila siku, yamezidi kuwa ya kukatisha tamaa.
‘’Walipunguza kila kitu na kila kitu!’’ Goryachev aliandika.
Katika hali ya sasa ya biashara, nitafunga karibu mwanzo wa Novemba.
Kila mtu ameshtuka,” mfanyabiashara huyo aliandika.
BBC haikuweza kujua kama maoni ya Goryachev yalibadilishwa na matatizo ya biashara – kwasababu alikataa kuzungumza na BBC.
Hali ya Goryachev ni mfano wa biashara zilivyo nchini Urusi: makampuni na jinsi yanavyoathirika na kushuka kwa mauzo na inakuwa vigumu pia kwa wao kuajiri wafanyakazi wenye ubora wa juu.
Biashara zadidimia
Kinyume na hali ya nyuma ya usajili wa wanajeshi wa ziada, hali ya kihemko sasa imebadilika.
Mwanzilishi wa kikundi cha Hurma cha kampuni Dmitry Levitsky anasema.
‘’Kuna hofu kati ya wafanyikazi: wengi wao ni chini ya miaka 35, na, kwa kweli, mtu akipigiwa simu, anaogopa kuipokea, mtu aliondoka, akaacha kazi na sasa anataka kuchukuliwa tena bila kusajiliwa jimboni’’.
‘’Kuna wasiwasi sana makazini – watu hawana mwelekeo kazini,‘’ Levitsky anaelezea hali hiyo.
Sekta ya vito imedidimia kabisa, anasema Eduard Utkin, mkurugenzi mkuu wa Chama cha Vito nchini Urusi.
Mbali na kupoteza wafanyikazi, sekta hii inakabiliwa na kushuka kwa kasi kwa mauzo. Usajili wa wanajeshi wa ziada umeathiri sana biashara ndogo za utengenezaji, anasema Utkin.
Huko, kama sheria, mtu mmoja tu aliye na taaluma ndogo tu, hufanya kazi katika kila eneo.
‘’Ikiwa hata mtu mmoja atachukuliwa vitani, shughuli zote zinasimama,’’ anasema Utkin.
Na pia, kupata mbadala wa mtu kama huyo ni shida, na uzalishaji hukwama kabisa,’’
Kati ya wafanyikazi takriban 1800 wa kampuni ya samani, watu 30 walikwenda vitani, anasema mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Maxim V.
‘’Hawana pa kwenda. Hawataenda vijijini - wana familia, wazazi, na mikopo.’’
‘’Hadi kufikia sasa, hali sio mbaya sana kibiashara, lakini ikiwa hasara ya wafanyakazi itaendelea, basi matokeo yake yatakuwa kupungua kwa viwango vya uzalishaji’’, mfanyabiashara anaongeza,
Hasara ya wafanyakazi wenye ujuzi maalum inaweza kuonekana.
Kwa wataalamu kama hao, kampuni inajaribu kupata wafanyakazi wa akiba kupitia tawala za mitaa, kwa sababu ni vigumu sana kupata mbadala wake.
Usajili wa wanajeshi wa akiba, utazidisha hali kuwa mbaya zaidi katika kazi za mikono, kama vile usimamizi au kazi za ofisini, Mikhail Burmistrov, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Infoline-Analytics, anaamini.
Tofauti kati ya wimbi la sasa la usajili wa wanajeshi wa ziada ni katika mgawanyiko wake wa matabaka, mtaalam anaongeza.
Watu matajiri zaidi wameondoka Urusi, na hilo linathibitisha moja kwa moja kushuka kwa mahitaji ya bidhaa katika sehemu ambazo bei za bidhaa huwa juu – majumba, magari na vifaa.
“Watu wanaolipwa pesa nyingi sana wanaondoka nchi, ikiathiri pamoja na kodi, nu kuajiri idadi kubwa ya watu wengine,’’ anasema Maxim Mironov, profesa wa fedha katika Shule ya Biashara ya IE.
Kupungua kwa watu na mapato
Kuondoka kwa wanaume kwenda vitani au kuelekea nchi nyingine kumeathiri mahitaji ya bidhaa na huduma.
Mmiliki wa mgahawa Dmitry Levitsky anakadiria kushuka kwa mapato katika sekta hiyo kwa asilimia 20.
Watu wanafuta uhifadhi wa ukumbi kwa ajili ya sherehe ambazo zilipangwa muda mrefu kabla ya usajili wa wanajeshi wa akiba kutangazwa.
Mbali na 10% ya wafanyikazi, kampuni kubwa ya TopGun imepoteza karibu nusu ya wateja wake, anasema mwanzilishi wa biashara Alexei Lokontsev.
Biashara ililenga wanaume pekee na sasa tunapitia wakati mgumu sana.
Lokontsev anakadiria mapato ya mwezi yamepungua kwa karibu 20%.
‘’Siku zote tuko katika hali ya kutarajia yasiyojulikana siku za usoni,’’ anasema.
Sekta ya mazoezi ya viungo vya mwili ni nyeti sana na daima huakisi hali ilivyo, anasema Elena Silina, rais wa Jumuiya ya Kitaifa ya Usawa.
Wiki moja baada ya kutangazwa kwa usajili wa wanajeshi wa ziada, mapato katika sekta hiyo yalishuka kwa wastani wa 25%, na mwezi wa Oktoba ulimalizika ukishuhudia matokeo hasi ya 35% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Wakati huo huo, katika mikoa inayopakana na Ukraine, kupungua huko kwa mapato kulifikia 70%.
“Kunapokuwa na kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika kwa biashara, ni vigumu sana kufikiria kuhusu mkakati.
Kuchoka sana na kuanza wasiwasi - hii inaweza isiwe na matokeo chanya katika timu,’’ anasema Egor Evlannikov, rais wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Equium.
Equium ilianzishwa na mfanyabiashara Igor Rybakov na huleta pamoja wajasiriamali na kati ya wakazi wa mradi huo ni waanzilishi wa ushauri wa kisheria, ofisi za usanifu, kuanza kwa teknolojia, viwanda na makampuni mengine.
Mwanzoni mwa shughuli ya usajili wa wanajeshi wa ziada, sheria ya Urusi ilikataza wanajeshi kujihusisha na ujasiriamali.
Mnamo Oktoba 18, Jimbo la Duma liliidhinisha katika usomaji wa kwanza wa mswada ambao utaruhusu wafanyabiashara waliosajiliwa vitani kuendelea kusimamia kampuni kupitia wawakilishi.
Serikali iliahidi kuwapa wafanyabiashara muda wa kujiweka sawa kabla ya wanaume kwenda kujiunga na vita.
Hapo awali, Waziri Mkuu Mikhail Mishustin alizungumza kuhusu siku tano, lakini mswada uliowasilishwa kwa Jimbo la Duma unarejelea kucheleweshwa kwa siku saba.
Biashara zina wasiwasi - bado huo ni muda mfupi sana kujipanga.
Hatua zilizopendekezwa na mamlaka zinachukuliwa na wajasiriamali kuwa hazitoshi.
Mishustin alifuatwa na vyama kama vinne vya biashara - Muungano wa Wanaviwanda na Wajasiriamali wa Urusi, wakiwa na ombi la kuahirisha wito huo wa usajili wa wanajeshi kwa makampuni.
Wakuu wa kampuni hizo waliomba kujiwekea akiba kutokana na usajili wa wanajeshi wa ziada ya 30-50% ya wafanyikazi, bila kujali eneo la kampuni, na pia kuwapa ahueni ya kujiondoa kwa waanzilishi na wakurugenzi wakuu.
‘’Kwa hisia zangu, mjasiriamali mmoja kama wa kibinafsi, kwenda vitani kutakuwa na manufaa kidogo kwa nchi ikilinganishwa na kufanya kazi kama mkurugenzi mkuu,’’ anasema Yegor Evlannikov.
“Akitoa hata kazi kumi ili familia ziweze kujikimu, anahakikisha kuwa watu hawa hawategemei serikali’’.
Wakati makampuni yana shughuli nyingi kujaribu kupata akiba ya wasimamizi na wafanyakazi, ni vigumu kutathmini athari za usajili wa wanajeshi wa ziada katika uchumi, anabainisha Maxim Mironov.
‘’Lakini athari katika suala la kuathirika kwa uchumi hasa katika bajeti itaanza kushuhudiwa mapema mwaka ujao,’’ mwanauchumi anasema.
‘’Uchumi sio chanzo cha habari zinazobadilisha mkondo wa vita hivi, lakini utabadilika baada ya muda,’’ mwanauchumi anabainisha.
Madhara yatatokea mwaka wa 2023, na kabla ya hapo kutakuwa na habari nyingi ambazo zitaathiri hali hiyo.
Mgogoro mkali utatokea kwa wakati mmoja - utaleta athari zake kwa miaka mingi ijayo.
‘’Wiki iliyopita, Vladimir Putin, alitangaza usajili wa wanajeshi wa ziada wa watu 222,000, aliahidi kwamba mchakato huo utakamilika ndani ya wiki mbili - yaani, mwisho wa Oktoba’’.
Hakuna cha ziada kilichopangwa.