Jinsi mfumo mpya wa kulinda anga ya Ukraine utakavyofanya kazi

Iliyochapishwa

Katika kipindi cha siku chache zilizopita tumesikia silaha zinazoelezewa kama mifumo ya ulinzi ya anga ya IRIS-T air defense system , mifumo yenye nguvu ya  kukabiliana na makombora ya anga ambayo Ukraine iliipokea kutoka kwa Ujerumani wiki hii.

 Kupelekwa kwa silaha hizo kulifuatia ombi la Ukraine kwa washirika wake ambayo iliwataka waipatie msaada zaidi baada ya Urusi kuipiga mabomu miji kadhaa siku ya Jumatatu , ikiwa ni pamoja na mji mkuu  Kyiv,  

 Baada ya mkutano katika makao makuu mjini brassels, nchi 50 wanachama wa wa Muungano wa NATO zenye ushirika na Ukraine, zilitangaza kutuma mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga nchini Ukraine.

 Silaha ambazo nchi ziliahidi kutoa kama  Uingereza, Canada, Ufaransa na uholanzi ni pamoja na makombora na rada kwa ajili ya mawasiliano, Marekani ilitoa ahadi saw ana hizo .

Lakini bila shaka, mfumo huo wa teknolojia ya hali ya juu ambao Ujeumaini inautuma ni moja ya  msaada unaozungumziwa zaidi kwasababu ni moja ya silaha za kisasa zaidi duniani.   

  'Enzi mpya ya ulinzi'

 

Ujerumani imeahidi kutuma mifumo hii ya ulinzi wa mashambulio ya anga minne iliyotengenezwa hivi karibuni , ingawa kwanza Kyiv itatakiwa kusubiri kwanza hadi mwaka ujao kusafirisha mingine mitatu iliyosalia. 

 Kulingana na serikali ya Ujerumani, silaha hii ndio ya kisasa zaidi ya mfumo wa ulinzi wa anga katika Ujerumani. 

 Mifumo ya mashambulizi ya anga hutumiwa kuwakinga watu, majengo muhimu, vitu na wanajeshi waliopo ardhini dhidi ya mashambulizi kutoka angani. 

Inafanya kazi vipi?

Mifumo ya IRIS-T imeundwa kwa ajili ya kulinda mji mdogo. Unaweza kudungua ndege, makombora yanayoongozwa kulenga au vitu fulani, na ndege zisizo na rubani.  

IRIS-T SL, ambayo ni aina ya hivi karibuni zaidi ya mfumo huu, ‘’ulifanikiwa’’ kufanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika mwaka  2014 mbele ya wawakilishi wa kimataifa.   

 Diehl Defense, ambao ni watengenezaji wa teknolojia hii, wanasema kwamba mfumo huu " una uwezo wa kutoa ulinzi wa muda mrefu wa eneo."

 "Kutokana na kwamba hutengenezwa na rada mbali mbali na mifumo ya kuongoza mapigano, IRIS-T ina uwezo na faida ya mfumo wa kisasa wa ulinzi wa mashambulio ya anga," anaongeza Diehl.

 Kulingana na gazeti la Ujerumani  Der Spiegel, mfumi huu " umeundwa kwa magari matatu: eneo ambalo roketi kusimamishwa wakati wa kufyatuliwa kwenye lori la kijeshi lenye uwezo wa kufyatua makombora manane, gari la rad ana gari la kuongoza mashambulizi ."

"Makombora ya kuzuia mashambulio ya anga yanaweza kupiga eneo lililopo hadi umbali wa kilomita 20 hadi 40," linasema gazeti la  Der Spiegel.

Kwa upande wake, shirika la utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle dlinaelezea kwamba makombota ya IRIS-T hutumia kutambua maeneo yanayolengwa na kwamba inaweza kuwekwa  nyuzi 360 kuzingira kifaa cha ufyatuzi.

Idhaa ya BBC ya Kirusi pia imeelezea kwamba rada ya  mfumo huo ni ina uwezo wa haraka wa ung’amuzi na hilo linaiweziesha kung’amua kwa urahisi makombora yanayopaa kwa kasi ndogo. Zaidi ya hayo, ina uwezo wa kuwinda wakati wote na kuangamiza  makombora mengi kwa wakati mmoja.

Je silaha hii ina maana gani kwa Ukraine? 

Kwa miezi michache iliyopita, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewaomba washirika wake wampatie mifumo ya ulinzi yenye uwezo wa kubuni  "ngao ya mashambulio ya anga"  kwa Ukraine.

 Jeshi la Ukraine linasema IRIS-T itailinda Ukraine  "dhidi ya gaidi".

 Akizungumza na Deutsche Welle, mtaalamu wa ulinzi Baraza la uhusiano wa kigeni la Ulaya Rafael Loss alisema mifumo hii "itaboresha pakubwa ulinzi wa Ukraine, wakati mifumo zaidi itakapopelekwa huko."

 Hatahivyo alionya kuwa kwa sasa haamini kuwa ‘’ haijaleta mabadiliko makubwa ambayo baadhi ya Waukraine wamekuwa wakiyasifia", ingawa inaongeza fursa kwamba "maeneo machache ya raia na wanajeshi yatapigwa".

Zelensky mwenyewe aisema siku ya Alhamisi, tarehe 13 Oktoba, kwamba Ukraine kwa sasa ina "10% ya kile inachokitaka " kwa ajili ya ulinzi wa mashambulio ya anga.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, anakadiria kuwa anahitaji silaha zaidi kuhakikisha ulinzi wa anga wa nchi yake. 

Ukraine bado ina mifumo ya enzi ya  usovieti  ya kukabiliana na mashambulizi ya anga ambayo sasa inataka kuifanya kuwa ya kisasa zaidi kwa msaada kutoka kwa washirika wake. 

 Hatahivyo, jeshi la Ukraine limeweza kuvizuia vikosi vya Urusi kupata mafanikio katika kipindi cha miezi minane ya vita, kulingana na Idhaa ya BBC ya Kirusi.

"Kwa mfano, wakati wa mashambulio mengi tarehe ya tarehe 10 -11 Oktoba ,mifumo ya ulinzi ya Ukraine ilidungua karibu 60% ya makombora ya Urusi ," wanaripoti.

 Hapana shaka kwamba mfumo wa ulinzi wa ang awa Ujerumani IRIS-T na silaha nyingine ambazo  wajumbe wa NATO waliahidi kuzitoa zitaimarisha uwezo wa Waukraine wa kuzuia mashambulizi ya Urusi, lakini wataalamu na Zelensky mweneyewe wanasema, wataendelea kuhitaji silaha zaidi kutoka kwa washirika wao.